Nachangia kidogo hapa.
Miaka ya ujamaa tuliaminishwa serikali inafanya kila kitu, kosa la kwanza, lakini linarekebishika.
Baadae na sasa tunaaminishwa, wawekezaji wa nje ndio suluhu. Hii lugha inatumika hadi vijijini, mfadhiili, mwekezaji atafanya hivi atafanya vile
Mbaya zaidi mwekezaji anaye fikiriwa hapa ni watu kutoka nje ya nchi.
Nikiangalia nchi nzima wazawa wenye viwanda na mashamba makubwamakubwa ni wale tunasema watanzania wenye asili ya mabara mengine.
Kwanini? Au hatuna maarifa, au mifumo ya ukopeshaji haipo kwa kila raia wa asili au husuda tu.
Wenye mamlaka ya idhini, ruhusa nk ni wachache wapo kusaidia mtanzania mwenzake kwa haki. Yaani wengi wapo siku ipite, hajali impact ya huduma yake kwa nchi.
Leo hii akitokea kiongozi mtanzania kuonekana mkaki kidogo utasikia mwamba huyo, jiwe nk. Hujitambui
hadi usukumwe? Si uwe mwamba mwenyewe mambo yakunyookee?
Mtanzania akipata sababu ya kumchelewesha mwenzie wala hasiti kufanya hivyo. Kukatishana tamaa na maelezo mengi bila suluhu imekuwa jadi.
Tutaendekea kujishangaa sana lakini baadhi ya sababu za kushindwa kwetu ni sisi wenyewe na tabia zetu.
Nini kifanyike?
Ubongo wa sisi watanzania unahitaji ku- format. Ni kwa njia ya kutengeneza mitaala ya elimu yakujibu zaidi changamoto zetu.
Elimu ipewe kipaumbele kwa bajeti na ubora. Walio faulu vizuri ndio wawe waalimu sio kinyume chake.
Hawa wabunge walazimike mara moja kwa mwaka kukutana na wawakilishi wa wananchi jimboni kwa idadi itakayo pangwa toka nyanja mbalimbali.
Kila wakirudi bungeni wasimuliane juu ya matakwa ya wananchi na moto walio washiwa.
Hii habari ya vikao vya kichama ni mkakati wa kulindana zaidi kuliko uwazi.
Bunge sawa ni aina ya uwakilishi lakini kuhodhiwa na chama kimoja ni upungufu mkubwa sana.
Kuwe na mkakati wazi na hata usio wazi kuwezesha raia asili kuwa wawekezaji wakubwa, kiteknolojia, biashara, uzalishaji nk.
Watanzania walio wengi wamewekeza kwenye kutengeneza mikate, kusaga unga labda malori na mabasi.
Tumeandaliwa tu kuwa waajiriwa na vibarua. Tulijengwa hofu ya kuwa tajiri au kumiliki mali na vitu.
Sasa Kuna kazi ya kuhamisha watu kutoka tabia za wivu, uoga, kutojiamini, majungu na husuda na kuwa watu wa malengo ya muda mrefu na kufanyia kazi.
Hiyo katiba mpya kama itaandaliwa isikose kibano, kitu kitakacho lazimisha chama chochote tawala kutekeleza mipango msingi ya muda mrefu.
Kumewahi kuundwa tume mbalimbali huko nyuma kwa mambo mbalimbali. Na sasa tuunde timu ya kitaifa ije na majibu ya tunabadilikaje na kuwa kweli nchi ya asali na maziwa kama tunavyochagizana.
Nadhani Japan, China nk hazikubadilika kimiujiza. Tume ije na majibu na tufanye utekelezaji kwa dhati, vinginevyo turidhike na kilichopo na tulivyo.