Tanzania: The Sleeping Giant

Ofcourse, TISS sometimes is misused.
It was supposed to stand for the interest of the country and not the interest of un-patriotic leaders.
 
Well said Mkuu.
Thanks for your eye opening response
 
Nakuelewa Mkuu,, uko sahihi pia. Japo kujikumbusha pia ni muhimu.
Hatuwezi kunyamaza tu kimya hata kama tunaona tupo sehemu ambayo hatukustahili kuwa.
Ahsante
 
Nachangia kidogo hapa.

Miaka ya ujamaa tuliaminishwa serikali inafanya kila kitu, kosa la kwanza, lakini linarekebishika.

Baadae na sasa tunaaminishwa, wawekezaji wa nje ndio suluhu. Hii lugha inatumika hadi vijijini, mfadhiili, mwekezaji atafanya hivi atafanya vile

Mbaya zaidi mwekezaji anaye fikiriwa hapa ni watu kutoka nje ya nchi.


Nikiangalia nchi nzima wazawa wenye viwanda na mashamba makubwamakubwa ni wale tunasema watanzania wenye asili ya mabara mengine.

Kwanini? Au hatuna maarifa, au mifumo ya ukopeshaji haipo kwa kila raia wa asili au husuda tu.

Wenye mamlaka ya idhini, ruhusa nk ni wachache wapo kusaidia mtanzania mwenzake kwa haki. Yaani wengi wapo siku ipite, hajali impact ya huduma yake kwa nchi.

Leo hii akitokea kiongozi mtanzania kuonekana mkaki kidogo utasikia mwamba huyo, jiwe nk. Hujitambui
hadi usukumwe? Si uwe mwamba mwenyewe mambo yakunyookee?

Mtanzania akipata sababu ya kumchelewesha mwenzie wala hasiti kufanya hivyo. Kukatishana tamaa na maelezo mengi bila suluhu imekuwa jadi.

Tutaendekea kujishangaa sana lakini baadhi ya sababu za kushindwa kwetu ni sisi wenyewe na tabia zetu.

Nini kifanyike?

Ubongo wa sisi watanzania unahitaji ku- format. Ni kwa njia ya kutengeneza mitaala ya elimu yakujibu zaidi changamoto zetu.

Elimu ipewe kipaumbele kwa bajeti na ubora. Walio faulu vizuri ndio wawe waalimu sio kinyume chake.

Hawa wabunge walazimike mara moja kwa mwaka kukutana na wawakilishi wa wananchi jimboni kwa idadi itakayo pangwa toka nyanja mbalimbali.

Kila wakirudi bungeni wasimuliane juu ya matakwa ya wananchi na moto walio washiwa.

Hii habari ya vikao vya kichama ni mkakati wa kulindana zaidi kuliko uwazi.

Bunge sawa ni aina ya uwakilishi lakini kuhodhiwa na chama kimoja ni upungufu mkubwa sana.

Kuwe na mkakati wazi na hata usio wazi kuwezesha raia asili kuwa wawekezaji wakubwa, kiteknolojia, biashara, uzalishaji nk.

Watanzania walio wengi wamewekeza kwenye kutengeneza mikate, kusaga unga labda malori na mabasi.

Tumeandaliwa tu kuwa waajiriwa na vibarua. Tulijengwa hofu ya kuwa tajiri au kumiliki mali na vitu.

Sasa Kuna kazi ya kuhamisha watu kutoka tabia za wivu, uoga, kutojiamini, majungu na husuda na kuwa watu wa malengo ya muda mrefu na kufanyia kazi.

Hiyo katiba mpya kama itaandaliwa isikose kibano, kitu kitakacho lazimisha chama chochote tawala kutekeleza mipango msingi ya muda mrefu.

Kumewahi kuundwa tume mbalimbali huko nyuma kwa mambo mbalimbali. Na sasa tuunde timu ya kitaifa ije na majibu ya tunabadilikaje na kuwa kweli nchi ya asali na maziwa kama tunavyochagizana.

Nadhani Japan, China nk hazikubadilika kimiujiza. Tume ije na majibu na tufanye utekelezaji kwa dhati, vinginevyo turidhike na kilichopo na tulivyo.
 
You are right 100%. Wenye maslahi binafsi wataanza kupiga kelele sababu serikali imebinasishwa sasa ni kama familia na ukoo wa familia washkaji kama kumi hivi Wana control Watanzania milioni 600 na chawa wao.

Kuondoa uozo, ufisadi, uhuni unahitwji mkono wa chuma.
 

Correct 100%.
 
Inasikitisha sana Mkuu..
Lakini iko siku huenda mambo yatakaa vizuri.
Hatuwezi kuendelea hivi hivi milele.
 
Mkuu hili andiko limekaa vizuri sana.
Ni andiko la kizalendo.
Bila shaka ndugu zetu wanaotutangulia (viongozi), watalichukua, walifanyie kazi.
Maendeleo siyo jambo rahisi hata kidogo.
Ni suala ambalo linakuhitaji utoe jasho, machozi na damu!
Kwa bahati mbaya, Watanzania wengi sisi ni wavivu kwa almost nyanja zote.
Wavivu wa kujifinza, wavivu wa kufuatilia mambo, wavivu wa kufanya kazi, wavivu wa kufikiri, wavivu wa kuweka malengo yawe ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, wavivu wa ......n.k..
 
Point of correction Mkuu, tuko almost milioni 60 kwa mujibu wa sensa ya mwaka jana.
Bado hatujafika milioni 600.
 
Mkuu mrangi , kila ukitaka magorofani Drive In, napata kumbukumbu nzuri ya those good old days!.

Tanzania ni inchi iliyobarikiwa almost everything but...

P
😁😁😁😁😁😁
Funguka tu Mkuu, najua kuna madini unaogopa kuyatema hapa!
Please be open for the betterment of our country.
 
Impressive content but you still need to polish your English language proficiency grammar and vocabulary! It’s like a high school debating language level [emoji4]
Mwenzako anajiona akiandika kwa Kiingereza (hata kama ni cha ugoko) ndio ataonekana wa maanaπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…