Tanzania to build Region's largest Gas-fired Power Plant; Export Power by 2017

siku sio nyingi tulimsikia waziri akisema mazungumzo ya kununua umeme ethiopia yanaendelea na yamefikia sehemu nzuri,sasa sijui itakuwaje kwakua walisema wametangaza tenda ya kumpata mkandarasi atakayejenga miundo mbinu ya kusafirisha huo umeme kutoka ethiopia kuja Tanzania.Ngoja tuone
 
ukiwa hujui kitu nakushauri usiwe unaongea
hizo data zako ni za uongo
hivi unajua hata Tanzania wanazalasha megawatt ngapi?

Hua naongea kwa fact sitoi data kichwani.
Sasa fungua hizi links za Wikipedia zinaonyesha List of power plants in Nigeria na South Africa na amount ya power wanayogenerate. Kama huamini Wikipedia basi nenda ukaamini story za vijiweni.

Alafu huo ushauri wako, "Ukiwa hujui kitu nakushauri usiwe unaongea" naomba nikupe wewe mwenyewe

Nigeria - https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_power_stations_in_Nigeria
South Africa - https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_power_stations_in_South_Africa
Tanzania - https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_power_stations_in_Tanzania
 

Sasa nawe umeenda kukosoa lakini sasa hizo Unit ulizotuwekea sijui ndio madudu gani.
 
Sasa nawe umeenda kukosoa lakini sasa hizo Unit ulizotuwekea sijui ndio madudu gani.

Naona hujapitia vizuri kusoma posts.. Nimeshasema K inamaanisha "Kilo" 3.9K maana yake 3,900. 50K - 50,000.
Sasa 3.9KMW maana yake 3,900 Mega Watts...
Jifunze mambo uelimike kidogo
 
Mnawachanganya wananchi.tumeambiwa kuna mpango wa kununua Umeme kutoka Ethiopia hapa mnatuambia tutauza Umeme nchi za jirani.hii mipango yenu ikoje? Btw mw 600 ni Umeme kidogo sana kuweza kuuza nje.hebu msije kuingia mikataba ya kilaghai jamani.watu wapo kibiashara zaidi shauri yenu.
 
Vichekesho kweli... Vi Megawatt 600 tunavipigia hesabu ya kuuza wakati hata hapa kwetu umeme haujatosha??

Ile sera ya Magufuli ya Viwanda tutaitekeleza kwa Umeme upi??
Nilidhani ni typing error labda ni Megawati 6000, kama ni 600 huu ni utani kwa serikali hii ya Magufuli!Hawa ni majipu ya kutumbua, waende zao wapuuzi hawana nia njema na nchi!Serikali iwekeze yenyewe
 

Kwa nini usilinganishe Gas Fired Plant na Gas Fired Plant, Ethiopia walinganishe na mambo ya mtera Dam kumbuka tabia nchi na uzururaji wa wafugaji katika kuzalisha majangwa kila wanapotimba. Kama imefikia 600MW ukilinganisha na songosongo basi bongo itasogea ado ado na kama walivyokwambia hapo juu fursa bongo zipo kuanzia makaa, nuclear mpaka renewable energy. Wengine wakienda liganga wakapiga 1000MW mpaka Namptumbo kutoa 100,000MW kutoka katika vinu vya kinyuklia inawezekana.

Tabia yenu ya kutopenda vyenu na kuthamini vya nje ni sheeda, mbona husemi Ethiopia wanatoa ngapi katika GAs.
 
Wakenya mnaweza kujilinganisha kuishinda Tanzania kibiashara si zaidi ya miaka 20 ijayo .vinginevyo mhesabu maumivu, Tanzania in baba Lao EAC nchi hii ilikosa uongozi bora Lakini with abundant natural resource, lakini with WhatWouldMagufuliDo subirini maumivu, Yule Msukuma halembi Yuko kikazi zaidi na ni scientist aliyekamilika.
 
Nilidhani ni typing error labda ni Megawati 6000, kama ni 600 huu ni utani kwa serikali hii ya Magufuli!Hawa ni majipu ya kutumbua, waende zao wapuuzi hawana nia njema na nchi!Serikali iwekeze yenyewe
Nasikia Muhonga ananunua Megawatt 400 Ethiopia...

Wakati tuna uwezo wa kuzalisha zaidi ya Gigawatt 6 Bonde la Mto Rufiji..
 
Hizo ni siasa tu kila mwaka ni hadith za miradi ya kufikirika tu, malizeni kwanza kinyerezi umeme mlioahidi kuwa historia uwake halafu ndo mlete hizo longo longo.
 
Nigeria inazalisha megawatt 50,000 kwa mwezi na bado haziwatoshi, South Africa megawatt 100,000 kwa mwezi bado haziwatoshi. Sisi megawatt 600 na tunawaza kuuza umeme. Daah ngoja tuone
Nadhani baada ya kuona na kutosheleza mahitaji ndipo suala la kuuza nje umeme litafikiriwa.. maana kuuza umeme nako kunahitaji maandalizi na miundombinu.
 
Juzi Ethiopia wamezindua power plant yenye uwezo wa kuzalisha more than 3000MW wewe unaongea kuhusu 600MW as the biggest in Africa? Umelogwa?
Amesema" in the region" that statement didn't mention any other countries besides zile ambazo zimetajawa kwamba zitauziwa umeme ambazo ni Mozambique, Zambia , Malawi , Rwanda na Burundi. Ikumbukwe huo ni mradi moja bado mengine ipo na Investors wengine wapo. Kwa hiyo uwezekano wa kuuza umeme mkubwa tu.
 
  1. Nakumbuka kuna wakati aliyekuwa kiongozi wetu alitoka Marekani kujadiliana na hao hao wawekezaji na akatangaza mgao wa umeme ungekuwa historia!
  2. Makala ya Wikipidia inadai kwamba robo ya umeme wote unaozalishwa Tanzania hupotea kwenye njia mbovu za usambazaji. Uzalishaji mpya uendane na uimarishaji wa njia za kusambaza umeme.
  3. Siku chache zilizopita Waziri Muhongo alisikika kwenye vyombo vya habari akisema ili tuwe na uchumi wa kati itabidi tuzalishe angalau 10,000MW. Kwa hali hiyo hizo 600MW sio nyingi sana.
  4. Kwa sasa, ni asilimia 20 tu ya Watanzania wameunganishwa kwenye gridi ya umeme. Inawezekana kufikisha gridi ya umeme nchi nzima, kama alivyofanya Rawlings huko Ghana alipokuwa Rais.
  5. Wawekezaji wengi hutaja kiasi kikubwa cha gharama kwani wataruhusiwa kurudisha gharama yote kabla ya kulipa kodi na kugawana "faida". Miaka mingi wametumia rushwa kupata viongozi wanaokubaliana na hivyo viwango vya uongo.
  6. Tusipoangalia, gesi itazalishwa kwetu, umeme utafuliwa kwetu na kuuzwa, na fedha zote zitatolewa nje. Sisi tutabaki na moshi wa kiwanda tu.
 
Majuzi waziri wa umeme wa jamhuri alilalamika kwamba SIMBION wameandaa mabilioni ili kuua harakati za Serikali kupitia TANESCO kujitoshereza kwa umeme kwa TANESCO kuwekeza kwenye Uzalishaji.

Yaani Simbion inataka kuhodhi biashara ya uzalishaji umeme kwa kuwahonga wabunge fulani fulani mabilioni.

Leo simbion nao wapo hewani.

Kweli hapa kunakitu kinakuja, si haba,
 
600 Mw kwa matumizi ya ndani hazitoshi sembuse kuuza nje ya nchi. symbion wanadhihirisha Ni kampuni ndogo kwa masuala ya nishati.
kule kwao inaweza kuwa Ni kampuni ya kuzalisha umeme eneo kama la kinondoni tu.
hawa symbion inawezekana walipigwa tafu na serikali ya America kwakuwa wao ndiyo watoaji WA ela za mcc
 
Last edited:
Hata 50% ya watanzania hawana umeme ila wanawaza kuuza umeme nje.

Hahahahahahaha
 

Kuna shida kubwa na hawa wamarekani... wanatumia serikali kudalalia mambo!! They are vuvuzelazing this project wakati we (Tanzania) could do it bila kelele

Ile issue ya MCC na Symbion ni shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…