#COVID19 Tanzania tuifuate dunia kwenye kupigana na Covid 19

#COVID19 Tanzania tuifuate dunia kwenye kupigana na Covid 19

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tanzania sio kisiwa, tunahitaji nchi nyingine kwenye mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na michezo, na kiusalama.

Kwakuwa Tanzania ni sehemu ya dunia, Afrika, SADC, na Afrika Mashariki basi kinachoikumba dunia, Afrika na East Afrika pia kinaikumba Tanzania na utatuzi wake lazima ufananefanane kote.

Dunia inasemekana kwa mujibu wa WHO shirika ambalo linaaminika duniani kote kuwa imekubwa na ugonjwa wa corona wanasayasi wamesema na wametoa njia ya kupambana na ugonjwa huo kama vile walivyoshauri kwa magonjwa mengine kama TB, HIV, Malaria, magonjwa ya moyo, kipindupindu, surua, kifaduro, pepopunda, ndui, nk ambayo hakuna MTU wala taifa linabishana juu ya namna ya kuyatibu na kuyakinga.

Ni kweli kuwa njia ambazo zimependekezwa safari hii na WHO ni njia ngumu sana kuzifuata kutokana na hali za kiuchumi za wananchi na mataifa yao, lakini kwakuwa Tanzania sio kisiwa tunategemea nchi nyingine kwa masoko, usalama, michezo, elimu, na fedha hatupaswi kuchukua njia tofauti kabisa na wenzetu wa dunia na wanaotuzunguuka katika kukabiliana na ugonjwa huu na pengine hata kukataa kuwa ugonjwa huu haupo Tanzania kutokana na maombi huku tukijua kuwa hata huko Israel na Maka ilikotoka mitume na dini hawasemi hakuna covid 19.

Inajulikana kuwa mataifa karibu yote hayatoi takwimu za kweli kuhusu covid 19 lakini angalau wanakubali kuwa covid 19 iko na watu wanaugua na wengine wanakufa.

Kusema kwetu kuna surua nadhani sio dhambi wala aibu bali ni njia njema ya kukinga watoto wenzako wasipate maambukizi kwa kuepuka kuja kucheza na we we nyumbani. Lakini kuficha watoto wenzako kuwa kwenu kuna surua ni kutaka waje kwenu au wewe uende kwao ili nao waambukizwe surua. Watoto wenzako hawatakukubali na watakuchukia sana kama wakijua kwenu kuna surua lakini unaficha. Na ndio maana dunia inalia na China ikidhani labda ilificha uwepo wa corona.

Ni kweli nia ni njema ya kuwatoa watu hofu dhidi ya korona, lakini njia hiyo inakubalika kwa majirani, Africa na dunia? Je, ni kweli maombi yameiondoa covid-19 Tanzania, je ni kweli Tanzania sasa hakuna corona?

Madhara yake makubwa ya kufanya hivi ni kwamba tutaonekana kuwa ni waongo hata kwa mambo mengine yasiyo ya covid 19 huko mbeleni. Ni vema kuwa na mkakati wa pamoja wa kikanda kama vile East Africa, SADC au afrika kuliko kila nchi ikaogelea kivyake.
 
Kuna kichwa kibovu kinatuongoza tuwe makini.
Nia yake ni njema kwetu Watanzania lakini inaweza isiwe njema kwa mahusiano ya kidunia ambayo sisi ni sehemu yake na tunayahitaji pia.
 
Nia yake ni njema kwetu watanzania lakini inaweza isiwe njema kwa mahusiano ya kidunia ambayo sisi ni sehemu yake na tunayahitaji pia
Nia njema kwa yeye kupata chanjo kisha kugoma kuleta chanjo ili wananchi wanyonge wasipate.
 
HAPANA! hapana! Hapanaaaaaa!

¤tunaweza kuishi bila wao.

¤tena laha mustarehe!

Kwani wao ndo akina nani bwana?

¤wajaribu kutuacha kivyetu alafu tutajua hapohapo namna ya kujitegemea.

¤Najua kuwa mwanzoni itakuwa ni vigumu ila baada ya mda tutazoea tu.

Nasi TANZANIA tutakuwa ni dunia ya pekee yetu isiyofungama na upande wowote ule kwani kuna ubaya?
 
HAPANA! hapana! Hapanaaaaaa!

¤tunaweza kuishi bila wao.

¤tena laha mustarehe!

Kwani wao ndo akina nani bwana?

¤wajaribu kutuacha kivyetu alafu tutajua hapohapo namna ya kujitegemea.

¤Najua kuwa mwanzoni itakuwa ni vigumu ila baada ya mda tutazoea tu.

Nasi TANZANIA tutakuwa ni dunia ya pekee yetu isiyofungama na upande wowote ule kwani kuna ubaya?
Hata pesa zetu wanatuchapishia wao, na watalii wanatoka kwao, madini yetu tunawauzia wao, hivyo sisi ndiye tunaewahitaji wao zaidi.

Nadhani tutumie ushawishi wetu kwenye East Africa na SADC ili tuwe na njia inayofanana ya kupambana na covid -19. Wahenga wanasema kama unataka kwenda haraka nenda peke yako lakini kama unataka kufika mbali zaidi nenda na wenzio.
 
Kwa mzee huyu meko ninadhani usijisumbue hamna litalobadilika mpaka damu zitakapo tutoka masikioni
 
ifuate hujakatazwa kila mtu apambanie uhai wake aseeee
Sio suala la kila ntu apambane na hali yake, bali lazima tufuate inavyotaka dunia (protocol) juu ya namna ya kushughulikia corona, vinginevyo dunia na majirani watatutenga kwenye mahusiano, kwenye michezo, kwenye uchumi, nk. Mfano, timu zetu zinahitaji kwenda kujumuika na timu nyingine kwenye mashindano ya ndani na nje ya nchi na ni lazima wapimwe corona, sasa itakuwaje kama sisi tunasema Tanzania hakuna corona, je, vijana wetu wakikutwa na corona huko tutawaambia nini wenzetu na dunia?.

Vinginevyo Tanzania isimamishe kwanza mambo yote yanayohitaji watu wetu kusafiri nje
 
HAPANA! hapana! Hapanaaaaaa!

¤tunaweza kuishi bila wao.

¤tena laha mustarehe!

Kwani wao ndo akina nani bwana?

¤wajaribu kutuacha kivyetu alafu tutajua hapohapo namna ya kujitegemea.

¤Najua kuwa mwanzoni itakuwa ni vigumu ila baada ya mda tutazoea tu.

Nasi TANZANIA tutakuwa ni dunia ya pekee yetu isiyofungama na upande wowote ule kwani kuna ubaya?
Eti LAHA MUSTAREHE
Kiswahili chenyewe hukijui.
 
Timu zetu kama simba, Namungo hazina budi kuwafungia ndani (isolate) wachezaji na viongozi wao kama wanataka kuendelea kushiriki mashindano ya kimataifa, la sivyo vipimo vya nje ya nchi vitawachanganya sana. Inabidi hata kwenye ligi ya vodacom, wachezaji wapimwe kabla ya mechi ili kuepusha kuwaambukiza wachezaji wenzao na pengine wale wanaoshiriki mashindano ya kimataifa.
 
Hao unaotaka kuwafata ili wasikutenge, walijipga lockdown na kujikinga kwa kila namna na sisi tukajiachilia kwa kila namna! kama wanayoyasema ni uhalisia zaidi kuliko porojo, siasa na vitisho vya huo ugonjwa basi hapa bongo tungekua tushadondoka wengi kama kuku mdondo!, kariakoo ingekua wanaokotwa watu kama 200 hvi kila siku, hosptali zingeja.

corona ipo ila wanaitumia kutupiga vita vya kisaikilolojia, its overated!
 
Jiwe anataka dunia ndio infuatishe yeye kweli haya maajabu
 
Tusipende kuigaiga kila kitu
Huku sio kuiga, bali ni makubaliano ya kitaalam yaliyofikiwa juu ya kupambana na corona, sawa na yale yaliyofikiwa juu ya namna ya kupambana na kaswendwe, gonoria, surua, malaria, mabusha na matende, kipindupindu, upungufu wa damu, magonjwa ya moyo, nk. Huwezi kusema kutumia panadol kupunguza maumivu ni kuigaiga, hiyo panodol haikugunduliwa Tanzania tumeiiga tu kama tulivyoiga na dawa na matibabu mengine yote kutoka nje ya nchi.
 
Hao unaotaka kuwafata ili wasikutenge, walijipga lockdown na kujikinga kwa kila namna na sisi tukajiachilia kwa kila namna! kama wanayoyasema ni uhalisia zaidi kuliko porojo, siasa na vitisho vya huo ugonjwa basi hapa bongo tungekua tushadondoka wengi kama kuku mdondo!, kariakoo ingekua wanaokotwa watu kama 200 hvi kila siku, hosptali zingeja.

corona ipo ila wanaitumia kutupiga vita vya kisaikilolojia, its overated!
Hayo ni kweli lakini dunia imetoa utaratibu wa namna ya kushughulikia corona, TB, mabusha, ngiri kavu, moyo mkubwa, nk. Hatuwezi kukubaliana na mengine halafu tukaacha mengine kwakuwa Tz sio kisiwa, tunaihitaji dunia kwa mambo mengi sana kuliko dunia inavyotuhitaji sisi. Mfano, naambiwa kuwa wachezaji wetu wa Namungo wamekwama huko Angola kwasababu ya protocol za kukabiliana na covid 19 zinavyotaka, sasa hapo utasema wameonewa?
 
139194874_3549010688549524_3774973619276164682_n.jpg
 
Back
Top Bottom