#COVID19 Tanzania tuifuate dunia kwenye kupigana na Covid 19

Tuna yakwetu ya kitaalam yaliyofanikiwa pia
 
nani anatupiga vita vya kisaikolojia? maana dunia nzima wanahaha, wanaugua, wanakufa na wamevaa barakoa. Ni taifa gani linalotupiga vita vya kisaikolojia ambalo kwao hakuna corona? wacha ukasuku
 
ni kweli mkuu, lakini haimaanishi kua kisa miongozo ya mwanzo walituletea tukaitumia, haimaanishi ndo kila kitu sasa, we are okay as we are! they are not okay as they are!, we good they aint good, so why would we tryna actin we aint good just cuz they aint good, while actually we good pal?.

We are just trying to play on our own ways! If they care, they should respect that, dont u think!?
 
I agree wit what y'r saying. But no single man can go against the world's direction and order, cos the world is a web like thing interlinked and interconnected. If the entire world believes the earth is sniping from east to west who are you arguing it without a robust research to negate the fact? Our arguments about covid that God has cured it are only good for allaying anxiety purposes among our own people, but not that of the world's people.

The world needs and works on a scientific argument, not just prayers worked. Prayers which did not work to th Israel and Saud Arabia where ALL the prophets came from are questionable to believe in.
 
fuata
 
Usiopoifuata kwa hiari utaifuata kwa shuruti. Tanzania ni mali ya dunia sio yetu pekee. Bahari, madini, mlima, ardhi na masitu ni mali ya dunia, tunaitunza tu kwa kwa niaba ya dunia. Dunia Ina maslahi yake Tanzania.
 
Endeleeni kushupaza shingo nyie si kisiwa bwana..lakini soon mtajua hamjui..cha msingi kila moja ajilinde na kulinda familia yake..this shit is real!
 
nani anatupiga vita vya kisaikolojia? maana dunia nzima wanahaha, wanaugua, wanakufa na wamevaa barakoa. Ni taifa gani linalotupiga vita vya kisaikolojia ambalo kwao hakuna corona? wacha ukasuku
Vaccine kwa sasa haikwepeki, lazima ukweli huu usemwe.
 
Endeleeni kushupaza shingo nyie si kisiwa bwana..lakini soon mtajua hamjui..cha msingi kila moja ajilinde na kulinda familia yake..this shit is real!
Afya na uhai ni mali binafsi ya mtu, usisubiri mtu akuambie nini ufanye au usifanye ili uwe hai, changanya na akili zako kisha chukua hatua, kaa mbali na mikusanyiko isiyo ya lazima, usisafiri kama sio lazima sana kusafiri, takasa mikono, fanya mazoezi, kula vizuri, vaa barakoa na nenda hospitali mapema.

Kama una wasiwasi za zilipo nyeti za kuku subiri upepo uvume.
 
Vaccine kwa sasa haikwepeki, lazima ukweli huu usemwe.
Huu ni wimbo wa dunia kila mmoja lazima auimbe japo kibwagizo/chorus chake hata kama hajisikii kuimba. Wewe ni nani usiimbe? Watakuimbisha tu wenye wimbo wao kwa nguvu ni heri ujifunze mwenye taratibu kuuimba.
 
Wewe si ni CCM mnaopinga kucha kuchwa??
 
Sasa ndio naanza kuona picha jinsi Mussa alivyopata shida ktk kuwaongoza wana wa Israel kwenda Kanani kwa miaka 40! Binadamu ni pasua kichwa! We omba visa wafuate na ukafanye kama wanavyofanya! Na usitumie Tanzania wala watanzania! Fanya kivyakovyako tu!
 
Nia ni njema kivipi?
Ni njema kwakuwa anataka watu wake wasiwe na hofu kubwa mno iliyopitiliza, taifa halina uwezo wa kuwagawia chakula watu waliojifungia ndani, miradi inayoendelea isisimame, na watu waendelee kulipa kodi ili serikali iendelee kutoa huduma. Hii inachagizwa na hamu ya kufanya vizuri kwnye uchumi na upatikanaji wa chakula usiyumbe.

Lakini ubaya wake tunasahau kuwa ugonjwa huu unaua wote, haubagui rangi, jinsia, kabila, cheo, wapanga sera na mipango wala wapangiwa mipango. Ugonjwa huu unaweza kubakisha mahame tu watu wa familia nzima wakiwa wamekufa kwa muda mchache kabisa.

Kama sio lazima sana kwenda kijijini kwenu tafadhali usiende huko jamani ili kuepuka kusafirisha ugonjwa hadi kwaa mama na baba yako, shangazi, mjomba, ndugu na jamaa zako huko kijijini ambako hakuna miundombinu na huduma za afya za kutosha. Baki mjini bhana, wewe watumie hela tu kwenye simu, usiende jamani huko waache wacheze harusi wenyewe, wacha wazike wenyewe na wacha wauguze wengine.
 
Safi sana, kama shida ni kuogopa kufanya lock down, kuna shida gani kuwaambia wananchi jamani huu ugonjwa upo, hatuwezi kulock down, lakini mnatakiwa kufuata masharti haya, kama ilivyokuwa mwaka jana, baada ya hapo yeye, waziri , katibu mkuu na serikali nzima iongee lugha moja. Shida iko wapi?
 
hata mm kero yangu imejikita hapohapo pa kusema Tz hakuna korona kabisa, maombi yamefanya muujiza wa kuangamiza corona sasa inakoromea kwingine huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…