Tanzania tuige mfano wa Uganda kuwajengea DRC barabara Ili kufungua biashara

Tanzania tuige mfano wa Uganda kuwajengea DRC barabara Ili kufungua biashara

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Hello members.

Hivi karibuni nchi ya Uganda imeanza ujenzi wa barabara za kimkakati zinazolenga kukuza biashara baina yake na nchi ya DRC Congo..

Barabara hizo zinajengwa ndani ya Mipaka ya DRC kwa makubaliano maalumu na kuharakisha kukuza biashara na uchumi.

Kwa mtizamo wangu ,hili ni wazo zuri na la kiubunifu wamefanya Uganda badala ya kusubilia DRC wajenge wenyewe.

Hii ni mbinu nzuri ya kibiashara ambaya Tanzania tunaweza kuiga na kujenga barabara na hata bandari zinazoweza kukuza biashara na kuimarisha usalama baina ya Tanzania na nchi jirani hususana DRC,Msumbiji na Burundi..

Kwa sababu unakuta kuna maeneo tumefikisha barabara lakini upande wa pili wao sio kipaombele au hawana pesa ni vyema tukawajengea kwa makubaliano maalumu.Wakati wanatulipa taratibu basi na biashara zinasonga.

Mfano Serikali imejenga bandari nyingi Sana tena kwa mabilioni ya Shilingi Ziwa Tanganyika na baadhi ya barabara za lami kufika kwenye hizo bandari .Bahati mbaya upande wa pili hakuna cha barabara wala bandari za maana mwisho wa siku miradi yetu inageuka kuwa tembo mweupe.

Tukitumia hii mbinu ya Africa kwa Afrika itasaidia Sana kutufikisha kwenye maendeleo ya fasta.Hongera Uganda kwa kuonyesha njia.

👇

Screenshot_20211206-220031.png


Screenshot_20211206-220041.png
 
😄😄 unamjua M7 kwa uongo mzee?Hapo haijengwi barabara hata ya 1/4 km ,tulimpa bandari pale Tanga Ni miaka na miaka Sasa hajawahi kuifanyia chochote kile.

Juzi M7 amesema anaenda Congo kupigana na ADF, karusha makombora wee ndani ya siku 5 tu Operation imesimamishwa eti wanaenda kufuata magreda maana barabara hazipitiki.😄😄 Hapo Ni Mbao zinaenda kuibwa kutoka Congo to Uganda.Barabara zinawekwa tayari.

M7 kwa uongo uongo hapa EA hakuna anaemfikia.Hata hili bomba la hoima sijui tu.
 
Kweli kabisa Africa tufanye mambo kama haya kwa vitendo,japo rasimali za Congo zikitumika vema wenyewe wanaweza kujenga barabara.
Shida si bado Wana fight mambo ya usalama,so kuwasaidia ni pamoja na kujenga miundombinu na huduma zingine itasaidia usalama na biashara.

Kikubwa mnafanya kwa makubaliano ya kulipa mdogo mdogo, ukisema usubirie ni expensive.
 
😄😄 unamjua M7 kwa uongo mzee?Hapo haijengwi barabara hata ya 1/4 km ,tulimpa bandari pale Tanga Ni miaka na miaka Sasa hajawahi kuifanyia chochote kile...
Vifaa viko site mkuu sio porojo nadhani hata ujenzi umeanza.

Msukumo mkubwa kwa wao ni kupata njia ya kuifokia DRC directly badala ya kupitia Rwanda.

Toka Wana mgogoro na Rwanda wanajaribu kupata njia mbadala,hata upande wa Tzn na Burundi wanampango wa kujenga barabara za kimkakati yaani zinabypass Rwanda.So wako serious.
 
Ataachaje kujenga wakati nusu ya mbao na magogo kutoka congo ni mali ya waganda ambao huecport china na ulaya na kuvuna mabilioni ya mapesa, hakuna wanajeshi matajiri kama wanajeshi wa Uganda hapa afrika mashariki maana wameiba congo hadi wamechoka
 
Ataachaje kujenga wakati nusu ya mbao na magogo kutoka congo ni mali ya waganda ambao huecport china na ulaya na kuvuna mabilioni ya mapesa, hakuna wanajeshi matajiri kama wanajeshi wa Uganda hapa afrika mashariki maana wameiba congo hadi wamechoka
😄😄 Chini ya Gen. Saleh magogo yanasafirishwa tu.
 
Back
Top Bottom