SoC04 Tanzania tuitakayo inatokana na watanzania tuwatakao!

SoC04 Tanzania tuitakayo inatokana na watanzania tuwatakao!

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 20, 2024
Posts
6
Reaction score
2
Je! watanzania tunaowataka ni wa aina gani?

Majibu mepesi ni kwamba tunahitaji Watanzania wazalendo, wachapakazi, waadilifu na wenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwajili ya afya ya taifa lenye maendeleo.

Watanzania tunaowahitaji lazima wawe na afya bora, elimu na miundombinu rafiki kwenye nyanja zote ili kuwezesha utendaji wao.

Sio kweli kwamba Watanzania wote hatupati huduma bora za kijamii japo wapo wanaozikosa kabisa, lakini ni kwa kiasi gani wanaozipata huduma bora za kijamii wanakua Watanzania tuwatakao wakiwa wazalendo,wachapakazi na waadilifu ili wawe na maendeleo?

Ni kweli kuna changamoto za ajira kwa vijana lakini vipi waliozipata wameifikisha wapi Tanzania yetu? Je ni kweli uwezo wao umeishia hapo kwenye kujijenga wao na Tanzania kwa ujumla?

Uchunguzi usio rasmi unaonesha kua Watanzania wengi wanapenda sana starehe na viburudisho! Hapa inajumuisha wote kwa viwango vya mapato yao, kwa elimu zao, kwa umri wao, kwa nyadhifa zao, kwa jinsia, kwa dini zao na kadhalika.

Kila mmoja anahitaji kustarehe kwa viburudisho mbalimbali hata visivyo ndani ya uwezo wao. Mfano mzuri ni siku kadhaa zilizopita tulimsikia mbunge mmoja akizungumzia matumizi mabaya ya fedha za kujikimu wanazopewa wanachuo(boom) hasa kwenye starehe mbalimbali ikiwemo pombe!

Watanzania wanatumia gharama kubwa kwenye huduma za intaneti ili kuingia kwenye mitandao kujiburudisha kwa habari zisizo rasmi, sanaa mbalimbali, uzushi, udaku na umbea na sio kupata vitu bora!

Serikali na Taasisi binafsi zinatumia nguvu nyingi sana kwenye maeneo mengi sana lakini tatizo linaanzia hapa Watanzania wengi wanateseka kwenye saikolojia zao na hajui namna ya kutatua changamoto hizo na wengi wanadhani ni hali ya kawaida kwani sehemu kubwa ya jamii ipo hivo! Hii imesababisha utendaji kazi kua hafifu na watu hutamani sana starehe na viburudisho.

Hili limetokana na vitu kadhaa; kama changamoto za kifamilia, ndoa, ugumu wa maisha, mahusiano na jambo kubwa zaidi ni malezi kwa watoto. Watoto wamekua wakirithi migogoro na matatizo ya vizazi vilivyopita na kusababisha kua na msongo wa mawazo na kukosa utulivu wa akili.

Mambo hayo kadhaa ndio mwanzo wa Watanzania wengi kukosa utulivu wa akili,kupata misongo ya mawazo,sonona na kuchanganyikiwa, jambo ambalo husababisha wengi kuishia kwenye kutafuta viburudisho kama pombe, madawa ya kulevya, bangi, ukahaba, michezo ya kubahatisha na vingine vingi ambavyo ni adui wa maendeleo kwani vinapunguza umaridadi na utendajikazi!

Mpango mkakati wa miaka 5-25 ni upi?
Serikali na mshirika binafsi viwekeze kwenye utoaji wa elimu ya afya ya akili na kujitambua kwa makundi yote ili kuwafanya watu waweze kupata utulivu wa akili na hisia.

Hii itasaidia sana vizazi vinavyokuja kwani vitapata malezi bora kutoka kwa wazazi wenye utulivu wa akili na hisia jambo ambalo litatufanya kuwapata Watanzania tunaowataka kwaajili ya Tanzanania tuitakayo!

Kutoka Dar es Salaam Tumaini University(DarTu)
Bachelor Degree of Mass Communication(1st year)
Email:chazdismassagdai@gmail.com
Contacts: 0675063150
Asante!
 
Upvote 6
Back
Top Bottom