SoC04 Tanzania tuitakayo itatimia na mfumo bora wa elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mr Mwanzo

Member
Joined
May 3, 2024
Posts
9
Reaction score
110
ELIMU: MSINGI, KING'AMUZI NA KICHOCHEZI CHA MAENDELEO KATIKA NYANJA ZOTE AMBAZO TUNAHITAJI ZIJENGEKE.
Screenshot_20240626-203346.png

Chanzo: Google Help
Screenshot_20240626-193028.png

Nchini Tanzania, suala sio kutoa elimu juu ya umuhimu wa elimu, Wala kuelekeza nguvu kubwa katika kunadi sera za elimu pekee, bali tunahitaji kufanya mchanganuo na uchambuzi yakinifu kuhusu jitihadi zilizofanywa, nguvu iliyoelekezwa kwa mda wote mrefu, matokeo yake na uwiano katika matarajio ambayo aidha serikali imekuwa ikiyaweka kila mwaka na nini kifanyike ili kuleta mapinduzi ya kweli.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuisukuma Tanzania kupiga hatua ya maendeleo katika nyanja zingine zote ambazo elimu ni nguzo mama;

1. Uwekezaji katika utoaji elimu bora
Hapa nchini, elimu bora inatolewa na uwekezaji unaendelea kufanyika. Ukweli ni kwamba licha ya juhudi hizo bado Kuna haja ya kuongeza ufanisi katika kufikia Ile hatua ambayo katika uhalisia tunatamani kufika hapo. Tunafanyaje kufikia haya? Ni Kama ifuatavyo;

Miundombinu Rafiki na wezeshi. Watoto hujifunza jambo na kuliweka akilini mapema kupitia kuona, kufananisha na kutofautisha. Majengo mazuri, upatikanaji lukuki wa vifaa vya kujifunzia na ambavyo humuwezesha kusoma/kujifunza bila shaka Wala ukakasi ni muhimu.

maxresdefault.jpg

Chanzo: Retrieved from From "mwananchi digital" via www.mwananchi.co.tz

2017-02-crd-tanzania-photo-01-1024x576.jpg

Chanzo: Learn more about a web page - Google Search Help

Ukitazama picha hizi mbili hapo juu ni wazi kwamba mazingira na miundombinu Rafiki Ina mchango mkubwa katika elimu kwa mwanafunzi.

Teknolojia: Vifaa vya kielectroniki vya kujifunzia havitoshi, hata vilivyopo havinufaishi hata nusu ya matarajio. Miongoni mwa sababu ni; walimu hawana utaalamu wa kutosha, walimu hugeuka kuwa wanufaika, ufuatiliaji wa taasisi ya elimu juu ya maendeleo hayo unahitaji kuongezeka zaidi.

tehama-pic.jpg

Elimu ya tehama shuleni, tujifunze kutoka nchi jirani. Source: www.mwananchi.co.tz

Vilevile, sera za elimu zinapaswa kutekelezwa kimikakati zaidi. Mfano, wanafunzi wenye uelewa mkubwa zaidi na vipaji wanapaswa kufahamu mapema maelekezo kwa vitendo. Suala la mwanafunzi kufeli ndipo anapelekwa kwenye mafunzo kwa vitendo (VETA) ni kudhoofisha utaalam na kuwapoteza wataalam wenye vipaji.

KIPAJI NA ELIMU ni sera nzuri kwa mtazamo wangu. Ili kuwezesha hili ni Lazima kutengeneza mazingira sahihi ya kung’amua vipaji hivyo na kuviendeleza na si vinginevyo.

e579906a394d715b.jpg

Screenshot_20240626-205041.png

Chanzo: Google Help

2. Kuiga kwenye faida
Nchi ambazo zimepiga hatua kubwa za maendeleo ni kutokana na mafanikio ya mikakati ya elimu kombozi, chochezi na yenye tija kwenye kuharakisha maendeleo. Hivyo Kama nchi, tunapaswa kuhakikisha tunaunda tume na mabalozi ambao watafanya kazi kwa kuzingatia viapo, uzalendo na kujitoa kutafuta namna sahihi ya kuleta mafanikio ndani ya miaka 5, 10, 15 au 20 kupitia elimu.
Mfano, kwanini nchi Kama china, nchi nyingi za ulaya, marekani zimefanikiwa kutengeneza wabobezi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa Taifa na hili linatokeaje.

Kusomesha na kusoma kwa kutanguliza uzalendo kwa maneno na vitendo. Kwamfano, wanafunzi wenye vipaji vikubwa kupewa (scholarship) kwenda kuchukua ujuzi na kuja kukutumia Tanzania pekee na sio kubaki ughaibuni kwa kigezo Cha maslahi.

MUHIMU: Kuna ulazima wa kuongeza maslahi kwa watu tajwa hapo juu kwani wapo watanzania wengi wataalam ambao wametapakaa nchi mbalimbali na wanatumiwa ipasavyo, hivyo mchango wao ni mkubwa kwenye kuchochea maendeleo ya nchi hizo ambayo sisi wenyewe tunayatamani sana.

3. Wanafunzi wanapaswa kuandaliwa kwa namna ya kufahamu malengo na namna ya kuyafikia
Pengine chini ya 20% ya wanafunzi nchini tanzania hawasomi kwa malengo yenye kuakisi uhitaji wa Taifa kupitia kutengeneza waleta maendeleo. Zaidi ya 80% ukiwauliza malengo watakwambia ni kufaulu. Kufaulu katika jambo gani kielimu ni swali gumu mno. Kuna haja ya kufuatilia uwezo wa Kila mwanafunzi na vipaumbele vyake mapema iwezekanavyo. Hii italeta tija. Yafuatayo ni muhimu katika kufanikisha hili;

Iandaliwe mitaala na vitabu vyenye kutoa picha na mwanga kwa watoto kuhusu kazi mbalimbali za kujenga Taifa. Mfano, urubani, uanasheria, uratibu kilimo, utaalamu wa teknolojia (IT), siasa, utawala wa umma, uhandisi, uinjinia (engineering) na mengine lukuki.

Screenshot_20240521-193513.png

Chanzo: www.universitiesblog.com

Sambamba na hilo hapo juu, Lazima kuwepo utaratibu wa kuchunguza mara kwa mara kipendeleo/vipendeleo vya mwanafunzi mmoja baada ya mwingine. Lengo ni kutengeneza wasifu (profile) ambayo itakuwa inafuatiliwa Kila ngazi ya elimu Hadi pale mwanafunzi atapojipambanua juu ya umuhimu wa kufanikisha Hilo na namna ya kufanikisha. Mfano, kutambua masomo ambayo yanahusika zaidi kwenye ndoto yake n.k

a-teacher-helping-1.jpg

Chanzo: Learn more about a web page - Google Search Help

4. Jamii husishwi (uhusishwaji wa jamii)
Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. Mfano, Lazima kuwepo na mawasiliano na ufuatiliaji kwa ukaribu baina ya mwanafunzi, mzazi, mlezi, mwalimu na viongozi wa ngazi zote kuhakikisha kila mmoja anawajibika (Checks and balances). Suala hili ni hafifu zaidi katika shule za vijijin na kata ukilinganisha na shule binafsi na zile za vipaji maalumu. Kuna haja ya kutengeneza sheria, Kanuni na miongozo katika kuhakikisha ukaribu baina ya mnyororo huu unafanya kazi ipasavyo.

Screenshot_20240626-194324.png

Chanzo: Learn more about a web page - Google Search Help

thumb_1243_800x420_0_0_auto.jpg

Chanzo; Mwanzo. DC SHIMO AITAKA JAMII KUWEKA ULINZI KWA WATOTO ILI KUDHIBITI UKATILI KWA WATOTO

5. Sheria ya elimu iangaliwe upya
Kwa kuboresha na hata kuweka ulazima wa uwajibikaji kwa Kila anayehusika na elimu kuanzia kwa mzazi/mlezi, mtoto Hadi viongozi wa juu. Hii itasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza uzembe wa makusudi.

Mfano: Sheria ya Elimu [sura ya 353 marejeo ya 2002] inampa mamlaka waziri wa ELIMU mwenye dhamana kusimamia na kuratibu masuala ya elimu ili kuhakikisha utoaji wa ELIMU Bora nchini Tanzania.
Kifungu cha 4(1) na (2) kinasema;
Screenshot_20240626-184353.png

Kifungu cha 5(e) na (f);
Screenshot_20240626-184423.png

KUMBUKA: Hayo yote yaliyoainishwa juu yanahitaji usimamizi wa sheria ili yaweze kumuwajibisha Kila anayehusika (binding and enforceable).
Miradi mbalimbali itajengwa na kuendelea kuimarishwa na wasomi. Mifano ni Kama ifuatavyo;
Mwl Nyerere hydro-electric power:
Screenshot_20240626-195808.png

Kuandaa Wataalamu wa viwanda:
Screenshot_20240626-200721.png

Chanzo: Google Help

Elimu yenye kuleta wabobezi wa masuala ya kilimo na mifugo:
Picha-na.-1-2-scaled.jpg

Chanzo: Google Help

Elimu ni muhimu katika nyanja ya madini;
DSC_6666.jpg

Chanzo: Google Help

HIVYO: Miundombinu & ujenzi, usafirishaji, utawala, sheria, mipango miji, mikakati, uandaaji na utekelezaji sera, shughuli zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii hutegemea uandaaji mzuri wa wataalamu ili kufanya kazi hizo.
 
Upvote 142
MUHIMU: Kuna ulazima wa kuongeza maslahi kwa watu ambao nimewataja hapo juu kwani wapo watanzania wengi wataalam ambao wametapakaa nchi mbalimbali na wanatumiwa ipasavyo, hivyo mchango wao ni mkubwa kwenye kuchochea maendeleo ya nchi hizo ambayo sisi wenyewe tunayatamani sana
Muhimu hii, ni kwamba soko la nyumbani la vipaji hivyo likiwa bora kiotomati wasomi watalivagaa. Tena haitakuwa wale wa nchini tu. Tufikie kiwango cha kuwavutia hadi wale wa nchi nyingine kama sasa wetu wanavyovutiwa huko.

Kuna haja ya kujifunza kama ulivyosema kwa walioweza. Mfano wa CHINA: Nadhani kijana maomi wa China alirudi nchini kwake kwa hamu kubwa maana anao uhakika kuwa atasaidiwa na serikali kuanzisha kampuni ya ujuzi aliosomea huko nje. Tena atapatiwa fungu la kutosha kuwaajiri marafiki zaje aliosoma nao nje ambao wao hawatataka kurudi nchini nwao bali waende uchina.

Na sasa, 'here is the catch'😄, serikali ya China ina hamu kubwa ya kumpatia hiyo mipesa yote na mafungu kwa sababu inajua itaenda kufanya kazi inayotakiwa. Na inajua kabisa fika kwamba, kama huyo kijana akizingua.. ... itamla kichwa, literally🤣🤣🤣🤣

KUMBUKA: Hayo yote yaliyoainishwa juu yanahitaji usimamizi wa sheria ili yaweze kumuwajibisha Kila anayehusika (binding and enforceable
Uwajibikaji, ndio neno msingi. Ahsante.
 
Muhimu hii, ni kwamba soko la nyumbani la vipaji hivyo likiwa bora kiotomati wasomi watalivagaa. Tena haitakuwa wale wa nchini tu. Tufikie kiwango cha kuwavutia hadi wale wa nchi nyingine kama sasa wetu wanavyovutiwa huko.

Kuna haja ya kujifunza kama ulivyosema kwa walioweza. Mfano wa CHINA: Nadhani kijana maomi wa China alirudi nchini kwake kwa hamu kubwa maana anao uhakika kuwa atasaidiwa na serikali kuanzisha kampuni ya ujuzi aliosomea huko nje. Tena atapatiwa fungu la kutosha kuwaajiri marafiki zaje aliosoma nao nje ambao wao hawatataka kurudi nchini nwao bali waende uchina.

Na sasa, 'here is the catch'😄, serikali ya China ina hamu kubwa ya kumpatia hiyo mipesa yote na mafungu kwa sababu inajua itaenda kufanya kazi inayotakiwa. Na inajua kabisa fika kwamba, kama huyo kijana akizingua.. ... itamla kichwa, literally🤣🤣🤣🤣

Uwajibikaji, ndio neno msingi. Ahsante.
Kabisa
 
2. Kuiga kwenye faida.
Nchi ambazo zimepiga hatua kubwa za maendeleo ni kutokana na mafanikio ya mikakati ya elimu kombozi, chochezi na yenye tija kwenye kuharakisha maendeleo. Hivyo Kama nchi, tunapaswa kuhakikisha tunaunda tume na mabalozi ambao kazi yao sio kuzurura tu na kuingia katika historia, ni wale ambao watafanya kazi kwa kuzingatia viapo, uzalendo na kujitoa kutafuta namna sahihi ya kuleta mafanikio ndani ya miaka 5, 10, 15 au 20 kupitia elimu.

Hili ni sahihi mno kwa Tanzania yetu
 
Nchini Tanzania, suala sio kutoa elimu juu ya umuhimu wa elimu, Wala kuelekeza nguvu kubwa katika kunadi sera za elimu pekee, bali tunahitaji kufanya mchanganuo na uchambuzi yakinifu kuhusu jitihadi zilizofanywa, nguvu iliyoelekezwa kwa mda wote mrefu, matokeo yake na uwiano katika matarajio ambayo aidha serikali imekuwa ikiyaweka kila mwaka na nini kifanyike ili kuleta mapinduzi ya kweli.
Nimeipenda hii sentensi ilivyokaa. Ki Kaizen yaan kila siku tunafanya viziluri zaidi, tunatafiti na kufanyiabkazi matokeo. Continuous improvements

Vilevile, sera za elimu zinapaswa kutekelezwa kimikakati zaidi. Mfano, wanafunzi wenye uelewa mkubwa zaidi na vipaji wanapaswa kufahamu mapema maelekezo kwa vitendo. Suala la mwanafunzi kufeli ndipo anapelekwa kwenye mafunzo kwa vitendo (VETA) ni kudhoofisha utaalam na kuwapoteza wataalam wenye vipaji. KIPAJI NA ELIMU ni sera nzuri kwa mtazamo wangu. Ili kuwezesha hili ni Lazima kutengeneza mazingira sahihi ya kung’amua vipaji hivyo na kuviendeleza na si vinginevyo.
Kweli asee, hata mi ninataka boda yangu ikatengenezwe na fundi mwenye akili na uelewa wa juu kuhusiana na vyombo vya moto ikibidi hata jiniazi kabisa. Kama tu ninavyopenda nitibiwe na daktari jiniazi, nifundishwe na mwalimu jiniazi. Nzuri
 
Mfano, kwanini nchi Kama china, nchi nyingi za ulaya, marekani zimefanikiwa kutengeneza wabobezi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa Taifa na hili linatokeaje.
China wanafundisha kwa vitendò sana kuliko maneno na mwanafunzi anaandaliwa kuwa mzalendo unadhani kwetu inawezekana au tufanye nini??
 
Kama nchi tunapaswa kuandaa misingi ya elimu kwa vitendo. Hili linahitaji mabadiliko makubwa na maboresho ya mfumo mzima wa ELIMU, Kuna umuhimu wa kumuandaa mwanafunzi kubobea taaluma mahusisi kutoka hatua za awali kabisa. Ndio maana wanafunzi wengi Hadi wanafika kidato Cha nne na sita hawajui wasome nn na Kwa lengo gani badala yake wanafany multiple choice ilimladi tu naye aende chuo. Hii haijakaa sawa
 
Maendeleo ni mchakato unaohitaji muda. Na muda ni jambo muhim sana. Tukitumia vibaya hatuwezi kufaulu, tunahitaji mshikamano na juhudi kubwa sana. Kuna namna ambavyo elimu imeachwa kwa viongozi na walimu, wananchi tunajisahau sana
 
Thanks for your nice compliment
 
ELIMU: MSINGI, KING’AMUZI NA KICHOCHEZI CHA MAENDELEO KATIKA NYANJA ZOTE AMBAZO TUNAHITAJI ZIJENGEKE.

Nchini Tanzania, suala sio kutoa elimu juu ya umuhimu wa elimu, Wala kuelekeza nguvu kubwa katika kunadi sera za elimu pekee, bali tunahitaji kufanya mchanganuo na uchambuzi yakinifu kuhusu jitihadi zilizofanywa, nguvu iliyoelekezwa kwa mda wote mrefu, matokeo yake na uwiano katika matarajio ambayo aidha serikali imekuwa ikiyaweka kila mwaka na nini kifanyike ili kuleta mapinduzi ya kweli.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kuisukuma Tanzania kupiga hatua ya maendeleo katika nyanja zingine zote ambazo elimu ni nguzo mama;

1. Uwekezaji katika utoaji elimu bora
Hapa nchini, elimu bora inatolewa na uwekezaji unaendelea kufanyika. Ukweli ni kwamba licha ya juhudi hizo bado Kuna haja ya kuongeza ufanisi katika kufikia Ile hatua ambayo katika uhalisia tunatamani kufika hapo. Tunafanyaje kufikia haya? Ni Kama ifuatavyo;

Miundombinu Rafiki na wezeshi. Watoto hujifunza jambo na kuliweka akilini mapema kupitia kuona, kufananisha na kutofautisha. Majengo mazuri, upatikanaji lukuki wa vifaa vya kujifunzia na ambavyo humuwezesha kusoma/kujifunza bila shaka Wala ukakasi ni muhimu.

View attachment 2996210
Chanzo: Retrieved from From "mwananchi digital" via www.mwananchi.co.tz

View attachment 2996212
Chanzo: Learn more about a web page - Google Search Help

Ukitazama picha hizi mbili hapo juu ni wazi kwamba mazingira na miundombinu Rafiki Ina mchango mkubwa katika elimu kwa mwanafunzi.

Teknolojia: Vifaa vya kielectroniki vya kujifunzia havitoshi, hata vilivyopo havinufaishi hata nusu ya matarajio. Miongoni mwa sababu ni; walimu hawana utaalamu wa kutosha, walimu hugeuka kuwa wanufaika, ufuatiliaji wa taasisi ya elimu juu ya maendeleo hayo unahitaji kuongezeka zaidi.

View attachment 2996220
Elimu ya tehama shuleni, tujifunze kutoka nchi jirani. Source: www.mwananchi.co.tz

Vilevile, sera za elimu zinapaswa kutekelezwa kimikakati zaidi. Mfano, wanafunzi wenye uelewa mkubwa zaidi na vipaji wanapaswa kufahamu mapema maelekezo kwa vitendo. Suala la mwanafunzi kufeli ndipo anapelekwa kwenye mafunzo kwa vitendo (VETA) ni kudhoofisha utaalam na kuwapoteza wataalam wenye vipaji.

KIPAJI NA ELIMU ni sera nzuri kwa mtazamo wangu. Ili kuwezesha hili ni Lazima kutengeneza mazingira sahihi ya kung’amua vipaji hivyo na kuviendeleza na si vinginevyo.

View attachment 2996216

2. Kuiga kwenye faida
Nchi ambazo zimepiga hatua kubwa za maendeleo ni kutokana na mafanikio ya mikakati ya elimu kombozi, chochezi na yenye tija kwenye kuharakisha maendeleo. Hivyo Kama nchi, tunapaswa kuhakikisha tunaunda tume na mabalozi ambao kazi yao sio kuzurura tu na kuingia katika historia, ni wale ambao watafanya kazi kwa kuzingatia viapo, uzalendo na kujitoa kutafuta namna sahihi ya kuleta mafanikio ndani ya miaka 5, 10, 15 au 20 kupitia elimu.

Mfano, kwanini nchi Kama china, nchi nyingi za ulaya, marekani zimefanikiwa kutengeneza wabobezi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa Taifa na hili linatokeaje.

Kusomesha na kusoma kwa kutanguliza uzalendo kwa maneno na vitendo. Kwamfano, wanafunzi wenye vipaji vikubwa kupewa (scholarship) kwenda kuchukua ujuzi na kuja kukutumia Tanzania pekee na sio kubaki ughaibuni kwa kigezo Cha maslahi.

MUHIMU: Kuna ulazima wa kuongeza maslahi kwa watu ambao nimewataja hapo juu kwani wapo watanzania wengi wataalam ambao wametapakaa nchi mbalimbali na wanatumiwa ipasavyo, hivyo mchango wao ni mkubwa kwenye kuchochea maendeleo ya nchi hizo ambayo sisi wenyewe tunayatamani sana.

3. Wanafunzi wanapaswa kuandaliwa kwa namna ya kufahamu malengo na namna ya kuyafikia
Pengine chini ya 20% ya wanafunzi nchini tanzania hawasomi kwa malengo yenye kuakisi uhitaji wa Taifa kupitia kutengeneza waleta maendeleo. Zaidi ya 80% ukiwauliza malengo watakwambia ni kufaulu. Kufaulu katika jambo gani kielimu ni swali gumu mno. Kuna haja ya kufuatilia uwezo wa Kila mwanafunzi na vipaumbele vyake mapema iwezekanavyo. Hii italeta tija. Yafuatayo ni muhimu katika kufanikisha hili;

Iandaliwe mitaala na vitabu vyenye kutoa picha na mwanga kwa watoto kuhusu kazi mbalimbali za kujenga Taifa. Mfano, urubani, uanasheria, uratibu kilimo, utaalamu wa teknolojia (IT), siasa, utawala wa umma, uhandisi, uinjinia (engineering) na mengine lukuki.

View attachment 2996227
Chanzo: www.universitiesblog.com

Sambamba na hilo hapo juu, Lazima kuwepo utaratibu wa kuchunguza mara kwa mara kipendeleo/vipendeleo vya mwanafunzi mmoja baada ya mwingine. Lengo ni kutengeneza wasifu (profile) ambayo itakuwa inafuatiliwa Kila ngazi ya elimu Hadi pale mwanafunzi atapojipambanua juu ya umuhimu wa kufanikisha Hilo na namna ya kufanikisha. Mfano, kutambua masomo ambayo yanahusika zaidi kwenye ndoto yake n.k

View attachment 2996213
Chanzo: Learn more about a web page - Google Search Help

4. Jamii husishwi (uhusishwaji wa jamii)
Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. Mfano, Lazima kuwepo na mawasiliano na ufuatiliaji kwa ukaribu baina ya mwanafunzi, mzazi, mlezi, mwalimu na viongozi wa ngazi zote kuhakikisha kila mmoja anawajibika (Checks and balances). Suala hili ni hafifu zaidi katika shule za vijijin na kata ukilinganisha na shule binafsi na zile za vipaji maalumu. Kuna haja ya kutengeneza sheria, Kanuni na miongozo katika kuhakikisha ukaribu baina ya mnyororo huu unafanya kazi ipasavyo.

View attachment 2996203
Chanzo; Mwanzo. DC SHIMO AITAKA JAMII KUWEKA ULINZI KWA WATOTO ILI KUDHIBITI UKATILI KWA WATOTO

• Uwepo wa ripoti za ufuatiliaji wa wazazi na walezi na kuwajibishwa ikibainika mzazi hatekelezi wajibu wake
• Ripoti za ufuatiliaji wa mwalimu wa darasa kwa darasa analopewa kusimamia na viongozi wote wa shule.
• Ripoti za watendaji wa elimu, mfano maafisa elimu na waratibu

5. Sheria ya elimu iangaliwe upya
Kwa kuboresha na hata kuweka ulazima wa uwanibikaji kwa Kila anayehusika na elimu kuanzia kwa mzazi/mlezi, mtoto Hadi viongozi wa juu. Hii itasaidia kuongeza uwajibikaji na kupunguza uzembe wa makusudi.

KUMBUKA: Hayo yote yaliyoainishwa juu yanahitaji usimamizi wa sheria ili yaweze kumuwajibisha Kila anayehusika (binding and enforceable).

HIVYO: Miundombinu & ujenzi, usafirishaji, utawala, sheria, mipango miji, mikakati, uandaaji na utekelezaji sera, shughuli zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii hutegemea uandaaji mzuri wa wataalamu ili kufanya kazi hizo.

MUWASILISHAJI: MWANZO HALFANI ABEDI
Safe sana ndug
 
Superb
 
Suala la kupambania elimu Bora Huwa ni jukumu letu sote
 
Thank you
 
Endeleza uzalendo
 
Back
Top Bottom