realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
TANZANIA TUITAKAYO IJIKITE ZAIDI KWENYE ELIMU YA VITENDO.
Tanzania kama ilivyo kuanzia ilikotoka hadi sasa iliandaliwa kwa misingi bora na imara ingawa kuna watu wachache wasio waadilifu wanaharibu misingi hiyo.
Yafuatayo ni mambo ya Muhimu yanayoweza kujenga Tanzania iliyo bora endapo yatazingatiwa.
Kwanza; Kuwajengea watoto wadogo nidhamu katika kila kitu wakati wa Makuzi yao. Kwa Mfano kuwajengea nidhamu ya kushirikiana katika kila kitu wanachokifanya nyumbani.
Kugawana vitu wanavyopewa na wazazi wao na majirani wengine, wazazi kuwalea watoto kwa usawa bila upendeleo. Kuwafundisha kutosheka na kuridhika lakini pia kutokuwa waharibifu wa Chakula,pesa na vitu vingine.
Hii itawasaidi kuondoa ubinafsi katika maisha yao,na hata wakikua wakipata madaraka hawatakua wenye kujipendelea wenyewe.
Haya mambo yanaweza kuanza kutekelezeka kuanzia sasa hadi miaka 25 ijayo.
Pili; Jamii ishirikishwe kikamilifu katika kuwaandaa na kuwatambua viongozi watakaoweza kuwaongoza Vema katika mafanikio kuanzia Ngazi ya Kijiji/Mtaa, kitongoji,Kata,Tarafa hadi Wilaya.
Nasema hivyo kwa sababu kwa sasa hivi ushirikishwaji ni mdogo sana kwani wanaoshirikishwa ni watu walio ndani ya Chama,wasanii lakini kundi kubwa limeachwa nyuma.
Tatu; Elimu itolewe kwenye Jamii kuhusu Uongozi ,Uadilifi,Weledi na mambo kama hayo.
Ukichunguza kwa undani watu wengi Hawana elimu yoyote Bali wanaoshi kwa mazoea tu na ndio maana kila mtu anaishi au anaongoza kwa kumuiga kiongozi fulani na sio kama yeye.
Mimi ni Mwandishi ninayefanya vipindi vya watoto kwa ubunifu mkubwa baada ya kugundua kuwa watoto wengi hawawezi kujieleza wenyewe nikaamua kubuni kipindi cha kuwapeleka maeneo ya viwandani, Bungeni, Mabaraza ya Madiwani ili waone Shughuli zinavyofanyika na kuwauliza nini wamejifunza.
Lakini pia huwa nazungumza na Viongozi wa Shule namna wanavyotambua nafasi zao hapo Shuleni lakini wengi hushindwa kujieleza.
Hili ni tatizo kubwa Hivyo Elimu inahitajika kuanzia sasa ili tuwe na Tanzania tutakayo kwa miaka 25 ijayo.
Nne; Kujiamini hii Inamaanisha kuondoa nidhamu ya woga kwa watu wowote wale ndani ya Jamii.
Bali watu waishi kwa kujiamini na kujiona kuwa unastahili kuwepo mahala fulani kwa sababu una elimu ya kutosha na sio kupendelewa hii itasaidia kuharakisha maendeleo.
Tano; Ubunifu
Watu wengi wanafanya vitu kwa mazoea na kwa kuiga na ndio maana hakuna maendeleo yoyote katika Taasisi, Mashirika au idara mbalimbali.
Watu wamekaa wakisubiri mishahara isome.
Hatuwezi kuwa na Tanzania tuitakayo endapo hakutakuwa na ubunifu wa aina yeyote ile. Watu wajitume na kufanya kazi.
Mfano mimi huwa sisubiri fursa inifuate Bali huwa naitengeneza mwenyewe.
Nimefanikiwa kufanya vitu vingi kupitia vipindi vya watoto na Tuzijue Sheria kwa kufanya vipindi vyenye ubunifu na kumvutia Msikilizaji na kupata elimu pia.
Mfano Niliandaa safari za wanafunzi wa Shule za Msingi za serikali kutembelea Bungeni kutoka Kilimanjaro hadi Dodoma kwa shida sana. Kwani kwa kawaida tu ni Shule za Binafsi ndio hutembelea Bunge mara nyingi.
Niliandaa ziara ya wanafunzi wa Shule za Msingi kutembelea Mpaka wa Kenya na Tanzania na kujionea kwa macho yao mipaka iliyowekwa na wakoloni ambayo wanaisoma kwenye Ramani tu.
Na ziara nyingi Muhimu na ukizingatia hata Michango kwa Shule za Serikali ni ya shida sana.
Aidhaa niliandaa ziara ya wanafunzi Shule za Msingi na kuwapeleka Mirerani na kujionea namna Madini yanavyochimbwa.
Vilevile niliwapeleka kwenye kiwanda kinachosafisha Dhahabu na mambo mengine kama hayo.

Upvote
3