Ibun Mallik
Member
- Dec 18, 2017
- 41
- 11
Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yanakuwa kwa kasi sana duniani na ni sekta muhimu sana katika maendeleo ya taifa lolote lile, Tanzania nayo kama nchi inayohitaji maendeleo lazima kuendana na kasi ya maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Yafuatayo yakifanyika tutafikia Tanzania tuitakayo kwa miaka ya mbele.
1. Kufanya Mabadiliko katika Mitaala ya Elimu kwenye Somo la TEHAMA. Ili kuendana na kasi ya Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano lazima Mitaala katika Somo la Tehama ifanyiwe marekebisho katika Shule, Vyuo vya kati na Vyuo Vikuu, mabadiliko hayo ikiwemo. I) Somo la Tehama kuwa lazima katika Ngazi zote za Elimu, II) kuandaa Vitabu vya Kiada na Ziada vya Somo la Tehama, III) kuandaa Walimu wabobezi katika Somo la Tehama, IV) kujenga Shule maalumu kwa Wanafunzi za Tehama V) kuandaa Michepuo ya Masomo ya Tehama kama ilivyo kwa Masomo ya Arts au Sayansi.
2. Kuimalisha na kusambaza Mkongo wa Mawasiliano ya Taifa. Ili kuendana na Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano duniani lazima kuimalisha na kusambaza Mkongo wa mMwasiliano wa Taifa ili kila eneo la Tanzania kupatikane mtandao ili kutimiza hilo lazima kufanya I) kusambazwa kwa Minara ya Mawasiliano Tanzania mzima, II) kuhakikisha huduma ya Mtandao wa kasi ya 4G inapatikana Tanzania mzima, III) kuimalisha Mkongo wa Mawasiliano wa baharini, IV) kupunguza bei za vifurushi vya data, V) kufunga huduma za mtandao bure katika taasisi.
3. Kuandaa Mashindano ya kitaifa ya ubunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Serikali ili kufikia maendeleo ya kasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano lazima kuandaa Mashindano ya Ubunifu kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa, Kanda hadi Kitaifa kama inavyofanywa katika sekta ya Michezo mfano Umisenta. Katika kufanikisha hili serikali inapaswa kufanya yafuatayo I) kuibua vipaji, II) kuendeleza vipaji vinavyoibuliwa, III) kuandaa zawadi kwa Washindi kama Motisha, IV) kuendeleza Ubunifu ulioibuliwa katika Ngazi zote, V) kuwazamini kimasomo Washindi katika Nchi bobezi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
4. Serikali kuiongezea Bajeti Wizara husika. Ili kufikia lengo maendeleo ya kasi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Serikali inapaswa kufanya uwekezaji miongoni mwa uwekezaji ni pamoja na kuweka bajeti kubwa katika Wizara husika, bajeti hiyo itawezesha I) ununuzi wa vifaa husika katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, II) kuendeleza Wataalamu, III) kuendesha Warsha na Masindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, IV) kueneza Mawasiliano Nchi mzima (Minara), V) kuboresha mitaala ya Elimu katika somo la Tehama kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu.
5. Kushawishi matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inapaswa kushawishi matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, serikali ili kuleta hamasa ya kuwepo kwake katika kulifanya hili serikali inapaswa kufanya I) matumizi ya mifumo ya Teknolojia kila sekta kwa kushirikiana na ega, II) Kila aina ya Malipo kwenda serikalini na katika sekta binafsi yapitie Mtandaoni, III) kuendeleza kitengo cha huduma Mtandao, IV) Kuruhusu matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi katika sekta za elimu katika kufanya mitihani na majalibio mengine, V) kufunga huduma ya Mtandao bure katika taassisi zote za umma na binafsi, VI) kuendeleza matumizi ya akili bandia, V) Miamala yote ya kuuza na kununua ifanyike mtandao, VI) Maombi yote ya kazi kwa serikali na sekta binafsi yafanyike mtandaoni.
6. Kupunguza Tozo na Kodi kwa Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na wawekezaji katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ili kuendelea kwa kasi katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano serikali haina budi kupunguza kodi na tozo katika vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na wawekezaji wa sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ili kufanikisha hili serikali inapaswa kufanya I) kupunguza tozo na kodi bandarini kwa wafanya biashara wa vifaa hivyo, II) kupunguza kodi kwa wawekezaji wa mitandao, III) kuweka ubora maalumu wa aina ya vifaa vitakavyoingia nchini vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kuepuka kuja kwa bidaa mbovu, IV) kupunguza kodi na tozo kwa wawekezaji wa viwanda vya uzalishaji wa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, V) kupunguza kodi kwa vyombo vya habari mtandaoni ikiwemo akaunti za youtube.
7. kusomesha Wataalamu nje za Nchi. Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wanapaswa kuwapeleka wataalamu wetu katika nchi zengine bobezi katika masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kuweza kuleta ufanisi mkubwa wa kiutendaji wanapokuja kwetu. Ili kufanikisha hili serikali inapaswa kufanya I) kupeleka nchi za nje wataalamu wetu kwa njia ya udhamini wa masomo ya muda mrefu na muda mfupi, II) kuwaleta wataalamu wa nchi za nje kuja kuwafundisha wataalamu wetu kwa njia ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji.
8. Kuandaa, Miongozo, kanuni, sera, na sheria madhubuti za kimtandao. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano lazima kuwepo na Makongamano na Warsha mbalimbali kwa ajili ya kuchukua maoni na mawazo ya wadau juu ya uundaji wa sheria za kimtandao. Ili kufanikisha ili serikali inapaswa kuhakikisha sheria zifuatazo zinaundwa I) sheria ya fedha ya kimtandao, II) sheria ya kimtandao ya unyanyasiji wa kijinsia, III) sheria ya usalama wa taarifa binafsi za mteja, IV) sheria za kimtandao za kimataifa, V) sheria ya mawasiliano ya kimtandao ya ujumla.
IMEANDALIWA NA: MALIKI ABDALLAH KILUME, 0685 344 373/0715 014 737

Upvote
0