SoC04 Tanzania tuitakayo katika miaka ijayo vyombo vya habari viache kuajiri watu wasio kuwa na ujuzi wa habari& utangazaji na uandishi

SoC04 Tanzania tuitakayo katika miaka ijayo vyombo vya habari viache kuajiri watu wasio kuwa na ujuzi wa habari& utangazaji na uandishi

Tanzania Tuitakayo competition threads

HARUNI IDDI

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
8
Reaction score
3
Tanzania tuitakayo katika miaka mitano ijayo na kuendelea Vyombo vya habari kama vile vituo vya redio, magazeti, na vituo vya runinga, vinapaswa kutoa fursa kwa vijana ambao wana ubunifu& maarifa na ujuzi na badale yake huajiri watu wasio kuwa na taaluma ya uandishi na utangazaji na kuajiri watu maarufu wasio kuwa na ujuzi katika maswala ya habari na utangazaji.

Pia vyombo vya habari hapa nchini vimekuwa vikijikita katika kugombania wandishi wenye majina makubwa badala ya kukuza vijana wenye vipaji ambao wana maliza katika vyuo vikuu kama chuo kikuu Cha Dar es salaam kwenye shule ya utangazaji na uandishi wa habari na taasisi nyingine zinazotambuliwa na serekali ilikuvindoa vyombo vya habari kwenye matatizo ya kukiuka sheria, kanuni, na miongozo inayo ongoza sekta ya habari kutokana kuwepo wa watu wasio kuwa na ujuzi kwenye maswala ya habari.

Serekali kupitia mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Baraza la habari la taifa (MCT) wizara ya bahari Teknologia ya habari na mawasiliano na taasisi nyingine ambazo Zina husika na maswala ya habari na kuandaa miongozo inayotaka mwandishi angalu kuwa na elimu ya cheti, (certificate ).au astashahada (Diploma). Ilikuwapa fursa vijana wanamaliza kusoma katika fani za uandishi wa habari na utangazaji kuweza kupata ajira na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wanaohitimu vyuoni.

Vyombo vya habari vina dhima ya kutoa elimu, kufichua maovu, na kushirikiana na serekali katika kutangaza fursa za kimaendeleo zilizopo kwenye jamii.
 
Upvote 1
Mwenye elimu husika, aifanye kazi husika.

Tena wasiishie hapo tu kwenye habari, watu wote ambao wanatamka na kusikika na makundi makubwa ya watu wawe na elimu ya mambo hayo;
Wanahabari
Waandishi wa vitabu
Wahubiri wachungaji na mashekhe
Viongozi
Wazazi

Elimu muhimu sana
 
Nigusie kwenye media.

Asilimia kubwa ya vyombo vya habari vimeajili waandishi walio na elimu ya uhandishi wa habari na baada ya mfumo kubadilishwa pale serikali ilipotaka waandishi waajiliwe kuanzia na diploma.

Pamoja na hilo kumekuwepo na Media ambazo zinaajili influencers media presenter ili kuvutia msikilizaji na hata baada ya kuwapa ajira au nafasi, baadhi ya media house vinawapa nafasi kusoma.

Sikuungi mkono kwa unalotaka, maana wewe utakuwa bado upo stone age kwamba cheti kikupe kazi how?.


Waanzilishi wa hivi vyombo asilimia kubwa siyo waandishi wa habari ila kwa sababu ya kuamua kuwekeza, wao wanajua kuna faida, hivyo basi elimu ni muhimu ila si lazima wakuchukue wewe mwenye elimu ya uhandishi alafu huna impact au profit.

Ipo hivi Media house zinaendeswa kwa pesa nyingi pamoja na mambo mengine bado sikuungi mkono, yeyote anatakiwa kuingia kwenye tasnia ili mradi awe na uwezo ndipo cheti kifuatie.
 
Back
Top Bottom