SoC04 TANZANIA TUITAKAYO: Matumizi ya Sayansi na Teknolojia Katika Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Tanganyika Mpya

Senior Member
Joined
May 3, 2024
Posts
170
Reaction score
375
Utangulizi:

Uchaguzi ni Haki ya msingi katika nchi yenye utawala bora ambao ni utawala unaofuata misingi ya sheria, haki, usawa, uwajibikaji, ushirikishwaji, demokrasia katika kuchochea uhuru binafsi katika ushiriki wa wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na kuwaona wanafaa katika kuwaletea maendeleo bila kujali vikwazo vya umbali, shughuli za kiuchumi wakati wa zoezi la upigaji kura

Hivyo Tanzania tuitakayo ni chaguzi zetu zote tatu ziendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuondokana na mfumo kongwe wa upigaji kura kuchagua viongozi wetu katika ngazi za kiuongozi (utawala). Hili linawezekana kama tutaruhusu kujifunza na kuboresha kutoka kwawalioanza matumizi ya teknolojia katika chaguzi zao mbalimbali, Mfano nchi kama Estonia, Ufaransa, Uswizi, Australia katika baadhi ya maeneo, India hasa Gujarat

Kutokana na ukubwa wa nchi yetu na jiografia ya maeneo ya kiutawala katika ngazi mbalimbali ya vitongoji, vijiji, kata, majimbo na taifa upelekea ugumu katika upatikanaji wa haki kwa wananchi katika kuchagua viongozi wanao wataka. Hii inatokana na vikwazo mbalimbali kama miundombinu barabara, kukosekana vituo vya kupigia kura, usalama wao binafsi, umbali ulipo kufikia sehemu zilizotengwa kupigia kura, shughuli zao binafsi (ajira, biashara, ibada) kuingiliana na zoezi la upigaji kura nk.

Pamoja na vikwazo vilivyopo ni muhimu fursa hii iweze kuwafikia popote walipo iwe ndani au nje ya nchi kwa kutengeneza mikakati sahihi na salama kwa wote

NINI KIFANYIKE?:

Kwanza kabisa ni kuendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kulidhia uanzishaji mchakato wa kadi moja yenye kubeba taarifa zote muhimu za mwananchi (TIN, NIDA, RITA, Uhamiaji, Nk) ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Hivyo tufanye yafuatayo kuelekea Tanzania tuitakayo kwa chaguzi zetu kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia:​
  • Kutengeneza mfumo ambao utabeba taarifa za wapiga kura wote na namba zao za utambuzi​
  • Namba za utambuzi (ID Number) zitawawezesha kupiga kura; utaingiza namba zako katika mfumo ili mfumo ukutambue na kukupa ruhusa ya kuendelea na mchakato wa upigaji kura.​
  • Kutengeneza mfumo utakao ruhusu mtumiaji kushiriki mara moja tu kupiga kura ili kuepuka upigaji wa kura zaidi ya mara moja​
  • Kutengeneza mfumo ambao utaruhusu kila mwenye sifa kutumia popote alipo na kumuwezesha kupiga kura bila kwenda kupanga foleni katika vituo vya kupigia kura. Hii ina weza fanyika kama watumiaji wa huduma za kibenki au kifedha kwa simu janja na simu za kawaida​

FAIDA YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA CHAGUZI ZETU MBALIMBALI NCHINI:

Zifuatazo ni faida za kuachana na mfumo kongwe wa upigaji kura na kuamia katika matumizi ya teknolojia ili kurahisisha matumizi ya mifumo na kuwafikia walengwa watumiaji

Kupunguza kwa kiasi kikubwa bajeti katika chaguzi zetu: Kila ikifika nyakati za uchaguzi huwa serikali ina tenga bajeti kwa ajili ya zoezi hilo, bajeti ambayo ina lenga matumizi bila kuwa na mapato kutoka katika taasisi husika. Hivyo matumizi ya tekinolojia yakitumika ipasavyo tuna tazamia bajeti kupungua kwa kiasi kikubwa na tuna weza kupata mapato baada ya uchaguzi kwa watu kulipia kupata taarifa au takwimu zilizopita ambazo zimehifadhiwa katika mfumo

Kuruhusu shughuli nyingine hasa za kiuchumi ziweze kuendelea: Mara kadhaa katika kipindi cha uchaguzi shughuli nyingi huwa zina simama kupisha zoezi hili liweze kufanyika, wafanyabiashara usitisha biashara kwa muda au siku nzima ili kupisha zoezi hili na wao binafsi waweze kushiriki. Hivyo kuruhusu matumizi ya teknolojia kuchukua nafasi ni kuruhusu shughuli zingine kuendelea bila kikwazo kwa kila mtu kushiriki kupiga kura pale alipo bila kulazimika kukusanyika vituoni

Kuepusha magonjwa ya milipuko: Mfumo kongwe unaotumika sasa una husisha au ruhusu mikusanyiko ambayo watu ukusanyika kupanga foleni kwa ajili ya kutimiza haki yao, na katika mikusanyiko kuna uwezekano mkubwa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama Uviko 19, TB; hivyo matumizi ya sayansi na teknolojia yanaenda kuondoa hii mikusanyiko ambayo inaweza kuwa kisababishi kwa magonjwa ya milipuko kutokea

Kuokoa muda wa kuhesabu kura: Matumizi ya mifumo hii itarahisisha kwa kiasi kikubwa kura kuhesabiwa kwa urahisi na kutoa matokeo kwa wakati ili kumtangaza mshindi wa uchaguzi, hivyo kwa teknolojia kutumika itaruhusu kila kura itakayopigwa kuonekana imeenda kwa mgombea fulani, wachama fulani hivyo kuokoa muda mwingi wa kuhesabu kura na kurudiarudia mara kwa mara. Hii itajenga imani na uwazi kama nguzo ya utawala bora

Kuondoa uwezekano wa kura zisizo halali kutokea: Kwa mfumo kuruhusu kila mwenye sifa kupiga kura mara moja pekee na kumtambua kila aliyepiga kura. Hii itaondoa uwezekano wa kura zisizo halali au batili na kuondoa malalamiko ya muda mrefu ya kuibiana kura baina ya wagombea na vyama shiriki katika chuguzi zetu

Kuongeza ushiriki wa makundi maalum: Matumizi ya teknolojia katika uchaguzi itasaidia kuongeza ushiriki wa makundi maalam kwa kiasi kikubwa kwa kutengeneza mfumo ambao utawazingatia ili kuweza kushiriki popote watakapo kuwa katika shughuli zao mbalimbali, kuliko mfumo na utaratibu wa sasa ambao watu wenye mahitaji maalum huwa wana jiondoa wenyewe kushiriki kwa kuona utaratibu uliopo na umbali wa kwenda katika vituo vya kupiga kura kama kikwazo kwao na kujihisi kubaguliwa na makundi mengine shiriki

Kuondokana na foleni katika vituo vya kupigia kura: Moja ya kero, kikwazo cha watu wengi kushiriki uchaguzi mkuu ni foleni zilizopo vituoni, hivyo matumizi ya sayansi na teknolojia yataenda kumaliza kero hii kwa kila mtu kuweza kushiriki popote alipo kwa uhuru bila kikwazo chochote cha kukaa foleni

Kuondokana na fujo ambazo utokea mara kwa mara nyakati za uchaguzi: Mara nyingi nyakati za uchaguzi zoezi hili uteka hisia za watu na mikusanyiko ya watu ubeba mawazo mbalimbali ambayo yanaweza shawishi uvunjifu wa sheria za nchi na ndio maana mara nyingi watu ushindwa kushiriki kupiga kura kuhofia fujo zinazoweza kutokea nyakati za uchaguzi. Hivyo kwa kila mtu kupiga kura alipo itasaidia uchaguzi kuendeleza amani na utulivu wa taifa letu

Utunzaji wa mazingira: Kuepuka, kupunguza uzalishaji na matumizi ya vifungashio na aina nyingine za vifaa kama plastiki, karatasi nk ambazo sio rafiki wa mazingira, vilevile mikusanyiko yenye kupelekea uharibifu wa mazingira kama kujisaidia hovyo, kutupa uchafu hovyo (chupa za maji, soda, juisi)​

Hitimisho:

Hivyo basi katika Tanzania tunayoitaka iruhusu matumizi ya sayansi na teknolojia, itasaidia kutoa haki kwa wote au wengi wenye sifa kushiriki kufanya maamuzi, na hii itakuwa faida kubwa kwa kizazi cha sasa na kijacho kuelekea Tanzania tuitakayo kwa kila mwananchi kuweza kutimiza haki aliyonayo kikatiba kwa njia ambayo ni rafiki na ya amani. Itasaidia pia kuimarisha ustawi wa taifa letu kama linavyo tambulika ulimwenguni kuwa kielelezo cha amani, demokrasia iliyokomaa na utawala bora​
 
Upvote 49
Ukiona hutajwi na Grea Thinkers kama hivi jua huna Thamani yoyote ile si tu hapa JamiiForums bali hata Dunaini kote.
 
Tanzania haijawahi Kuwa Na uchanguzi
 
Kura ya haki inapatika kwa kupiga kura ya wazi. Kwa nini ujifiche kumchagua kiongozi unayemtaka? Na kura ya wazi itapunguza gharama kubwa za uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…