SoC04 TANZANIA TUITAKAYO: Mfumo wa Elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kabydion Mamkwe

New Member
Joined
May 15, 2024
Posts
3
Reaction score
7
MWANZO

Mfumo wa elimu uliopo hauandai mtoto wa kitanzania kwa ajili yakua hazina kwa taifa la kesho kutokana na mtaala uliopo. Mtaala huu hauna dira bora kwa ajili ya taifa tulitakalo kwasababu mtaala huu hauandai watu wenye ubora unaohitajika.

MAPUNGUFU

Elimu iliyopo ni ya nadharia kuliko vitendo; elimu iliyopo haimuandai mtoto wa kitanzania kwa ajili ya kujipambania yeye na taifa kwa ujumla hii ni kutokana na muktadha mzima wa utoaji elimu wa nchi yetu, mtoto anajikita kujifunza katika kusikia kuliko kuona kitu kinachopelekea mtoto kuwa muongeaji sana tuliko mtendaji hivyo kukosa matokeo chanya kwasababu taifa halitofanikiwa kwa kua na watu wenye ubora katika kusema kuliko kutenda.

Muda; elimu iliyopo inatumia muda mwingi wa mtoto na haimuandai mtoto katika namna bora ya yeye kua mtu fulani hapo badae, kwa mafanikio binafsi na ya taifa. Mfano mtoto anatumia miaka 17 hadi 20 kuwa darasani ukijumlisha miaka yake mitano au sita ya makuzi kabla ya Kwenda darasani (shule) anafikisha miaka zaidi ya 22 kitu kinachopelekea taifa kuwa na vijana wengi tegemezi wasio na faida kwa jamii na taifa kwa sababu muda mwingi walitumia darasani kujiandaa kuajiriwa pasipo kujifunza uzalishaji.

Elimu isiyo na malengo; elimu iliyopo haijaweka malengo ya taifa wala haijali malengo ya mtoto wa kitanzania ndio maana elimu iliyopo haina mfumo wa kuonyesha kitu gani kinaitajika na kwa wakati gani na tathimini inafanyika kwa kuangalia ufaulu wa Watoto tu si matokeo ya mwisho baada ya ufaulu, yani utendaji wao umeleta manufaa gani kwao na kwa taifa.

MAREKEBISHO

Elimu ijikite kwenye nadharia na vitendo; hii ni kwasababu elimu ya nadharia itamsaidia mtu katika kujieleza na elimu ya vitendo itasaidia katika utendaji. Elimu yetu inapaswa izingatie vitu vyote hivi ili iweze kuandaa wataalamu wenye uwezo na ujasiri kwasababu wanajiamini kutokana na uwezo walio nao si hii elimu ya sasa inayomfunga mtu, unakuta mtu amesoma hadi chuo kikuu lakini hawezi kufanya kazi yake kikamilifu kwasababu alisikia tu hajui jinsi ya kutenda hali hii inaweza kushusha ujasiri wake kwa kua anaweza kuongea lakini ana hofu kwa sababu hajui kuamisha maelezo katika utendaji, hivyo ni vyema hivi vitu viende sambamba kwa mafanikio Zaidi.

Uwekaji wa malengo; taifa lazima liwe na malengo na si kuitaji tu wasomi, taifa lazima lijue linaitaji wasomi wa namna gani na kwanini linawaitaji hii itasaidia taifa kufikia malengo yake. Taifa letu linaitaji kuimarisha uchumi wake na wa watu wake kwa kutumia rasilimali zilizopo. Hivyo ni vyema kufanya tathmini bora ya rasilimali ili kujua wataanza na kitu gani na gani ili kuandaa mfumo bora wa elimu utakao waandaa wasimamizi na wafanyakazi bora watakaofanya kazi kwa maslai ya taifa. Mfumo wa elimu utapaswa uelekezwe sana kwenye malengo ya taifa mfano lengo la taifa ni kukuza uchumi wake kwa asilimia X mpaka kufikia mwaka Y, tutajikita sana kwenye tasnia A, B, C na D hivyo ni vyema kuongeza nguvu kuandaa wataalamu wa ndani katika tasnia zote ABCD tena wandaliwe wenye ubora katika utendaji ili uzalishaji ukue. Sio watu wanasoma vitu visivyo na uhitaji itakua kuongeza wategemezi badala ya wazalishaji.

Kuzingatia muda na umri; swala la umri na muda mtoto anaotumia kusoma ni muhumu kuzingatiwa, kwasababu ni vyema tathmini ya umri na muda ifanyike ili kupunguza watu wazima ambao ni tegemezi. Serikali izingatie umri mtoto anapoanza kujitambua na kuwa na uwezo wa kujifunza na kuiga huu ni muda sahihi kuanza shule na kupata wepesi wa kuelewa. Muda wa kuwa darasani upungue yani miaka iwe michache na wasome vitu vyenye tija tu kwa nadharia na vitendo kuanzia awali hadi elimu ya juu. Mfano kama mfumo wa sasa mwanafunzi anaweza soma miaka miwili sekondari na akafanya vizuri, ni vizuri mfumo huu utumike kusoma kidato cha kwanza hadi cha sita kwa miaka mitatu na marekebisho ya mtaala ubadilike ili miaka ya elimu msingi pia ipungue.

Tabia; elimu yetu inapaswa kujumuisha swala la malezi katika mtaala kwa sababu malezi huzaa tabia. Liandaliwe somo la malezi ambalo litakua likiongoza matendo ya mtu kuanzia akiwa mtoto. Mfumo ulioko haumfunzi mtoto uzalendo, haki na ujasiri ndio maana taifa letu lina Watoto na watu wazima waoga wasioweza kujisimamia wala kusimamia wengine, pia ongezeko lajamii, viongozi na watendaji wasiowajibika na wapenda rushwa. Somo hili linaweza kuandaa kizazi chenye watu jasiri, wazalendo, wanaojitambua na wanaowajibika hii itasaidia katika maendeleo ya taifa kwasababu watu watakua wanaojiamini, wanaojituma, wanaowajibika pale wanapokosea, hakutakua na vibaraka wa mataifa mengine wala ukoloni mamboleo kwa sababu kutakua na umoja.

Elimu na siasa; ni wakati sasa serikali kufanya maamuzi ya kutenganisha utendaji wa maswala ya siasa haswa maswala ya vyama na elimu, hii ni kwasababu elimu imekua sehemu ya kupigia upatu maswala ya vyama vya siasa mfano swala la vyama vya siasa katika ngazi ya elimu ya juu haziendeshwi katika njia sahihi hivyo ni vyema kama serikali imeona maswala ya siasa kuwepo kwenye ngazi ya fulani ya elimu ni bora, basi elimu hiyo ya siasa iwepo kuanzia ngazi ya chini sana, na elimu hiyo itenganishwe na vyama ili watu wawe na mwanga angavu kuhusu siasa ya nchi yao na wajue majukumu yao kama wananchi ni yapi, ili ikifika muda unaowaruhusu kufanya maamuzi kwa ajili ya taifa wafanye maamuzi sahihi kwa ajili yao na taifa zima bila kufanya maamuzi kwa maslahi binafsi au maslahi ya chama Fulani.

MWISHO

Ni muda sasa kwa taifa kusimama pamoja kufanya mabadiliko sahihi na kwa wakati sahihi, ni muda sasa wa watu kuwa watendaji sana kuliko waongeaji ili tukapate kuona mafanikio tunayoyatamani sana kwa muda mrefu. Viongozi wafanye maamuzi yenye tija kwa ajili ya taifa letu wajifunze kufanya tathmini ya mambo ili waweze kutuvusha kwa wakati unaostahili. Viongozi wakumbuke “tunatamani kufanikiwa na kufika mbali sana kama taifa lakini kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya kutufikisha TANZANIA TUITAKAYO wafanye tathmini ya jambo husika kwa upana sana, kwa kuzingatia muda na lengo (faida). Hivyo kuna muda kuliko kuwai kufanya jambo na kupoteza kikubwa ni heri kusubiri kufanya kwa ubora ili kupata kilicho bora Zaidi”.​
 
Upvote 8

Ni vyema sana
 
Elimu ijikite kwenye nadharia na vitendo; hii ni kwasababu elimu ya nadharia itamsaidia mtu katika kujieleza na elimu ya vitendo itasaidia katika utendaji
Saaafi sana, vyote viwili vinaenda pamoja. Haya ndiyo mawazo tunayotaka sasa👊.

mfano lengo la taifa ni kukuza uchumi wake kwa asilimia X mpaka kufikia mwaka Y, tutajikita sana kwenye tasnia A, B, C na D hivyo ni vyema kuongeza nguvu kuandaa wataalamu wa ndani katika tasnia zote ABCD tena wandaliwe wenye ubora katika utendaji ili uzalishaji ukue. Sio watu wanasoma vitu visivyo na uhitaji itakua kuongeza wategemezi badala ya
Tuongozwe na maono thabiti ya nini tunataka, na ndio tunafanya hicho.

Somo hili linaweza kuandaa kizazi chenye watu jasiri, wazalendo, wanaojitambua na wanaowajibika hii itasaidia katika maendeleo ya taifa kwasababu watu watakua wanaojiamini, wanaojituma, wanaowajibika pale wanapokosea, hakutakua na vibaraka wa mataifa mengine wala ukoloni mamboleo kwa sababu kutakua na umoja.
Somo linalotakiwa kuwa endelevu hadi kwenye media hili. Asee insha mirua sana hii.
 
MWANZO

Mfumo wa elimu uliopo hauandai mtoto wa kitanzania kwa ajili yakua hazina kwa taifa la kesho kutokana na mtaala uliopo. Mtaala huu hauna dira bora kwa ajili ya taifa tulitakalo kwasababu mtaala huu hauandai watu wenye ubora unaohitajika.

MAPUNGUFU

Elimu iliyopo ni ya nadharia kuliko vitendo; elimu iliyopo haimuandai mtoto wa kitanzania kwa ajili ya kujipambania yeye na taifa kwa ujumla hii ni kutokana na muktadha mzima wa utoaji elimu wa nchi yetu, mtoto anajikita kujifunza katika kusikia kuliko kuona kitu kinachopelekea mtoto kuwa muongeaji sana tuliko mtendaji hivyo kukosa matokeo chanya kwasababu taifa halitofanikiwa kwa kua na watu wenye ubora katika kusema kuliko kutenda.

Muda; elimu iliyopo inatumia muda mwingi wa mtoto na haimuandai mtoto katika namna bora ya yeye kua mtu fulani hapo badae, kwa mafanikio binafsi na ya taifa. Mfano mtoto anatumia miaka 17 hadi 20 kuwa darasani ukijumlisha miaka yake mitano au sita ya makuzi kabla ya Kwenda darasani (shule) anafikisha miaka zaidi ya 22 kitu kinachopelekea taifa kuwa na vijana wengi tegemezi wasio na faida kwa jamii na taifa kwa sababu muda mwingi walitumia darasani kujiandaa kuajiriwa pasipo kujifunza uzalishaji.

Elimu isiyo na malengo; elimu iliyopo haijaweka malengo ya taifa wala haijali malengo ya mtoto wa kitanzania ndio maana elimu iliyopo haina mfumo wa kuonyesha kitu gani kinaitajika na kwa wakati gani na tathimini inafanyika kwa kuangalia ufaulu wa Watoto tu si matokeo ya mwisho baada ya ufaulu, yani utendaji wao umeleta manufaa gani kwao na kwa taifa.

MAREKEBISHO

Elimu ijikite kwenye nadharia na vitendo; hii ni kwasababu elimu ya nadharia itamsaidia mtu katika kujieleza na elimu ya vitendo itasaidia katika utendaji. Elimu yetu inapaswa izingatie vitu vyote hivi ili iweze kuandaa wataalamu wenye uwezo na ujasiri kwasababu wanajiamini kutokana na uwezo walio nao si hii elimu ya sasa inayomfunga mtu, unakuta mtu amesoma hadi chuo kikuu lakini hawezi kufanya kazi yake kikamilifu kwasababu alisikia tu hajui jinsi ya kutenda hali hii inaweza kushusha ujasiri wake kwa kua anaweza kuongea lakini ana hofu kwa sababu hajui kuamisha maelezo katika utendaji, hivyo ni vyema hivi vitu viende sambamba kwa mafanikio Zaidi.

Uwekaji wa malengo; taifa lazima liwe na malengo na si kuitaji tu wasomi, taifa lazima lijue linaitaji wasomi wa namna gani na kwanini linawaitaji hii itasaidia taifa kufikia malengo yake. Taifa letu linaitaji kuimarisha uchumi wake na wa watu wake kwa kutumia rasilimali zilizopo. Hivyo ni vyema kufanya tathmini bora ya rasilimali ili kujua wataanza na kitu gani na gani ili kuandaa mfumo bora wa elimu utakao waandaa wasimamizi na wafanyakazi bora watakaofanya kazi kwa maslai ya taifa. Mfumo wa elimu utapaswa uelekezwe sana kwenye malengo ya taifa mfano lengo la taifa ni kukuza uchumi wake kwa asilimia X mpaka kufikia mwaka Y, tutajikita sana kwenye tasnia A, B, C na D hivyo ni vyema kuongeza nguvu kuandaa wataalamu wa ndani katika tasnia zote ABCD tena wandaliwe wenye ubora katika utendaji ili uzalishaji ukue. Sio watu wanasoma vitu visivyo na uhitaji itakua kuongeza wategemezi badala ya wazalishaji.

Kuzingatia muda na umri; swala la umri na muda mtoto anaotumia kusoma ni muhumu kuzingatiwa, kwasababu ni vyema tathmini ya umri na muda ifanyike ili kupunguza watu wazima ambao ni tegemezi. Serikali izingatie umri mtoto anapoanza kujitambua na kuwa na uwezo wa kujifunza na kuiga huu ni muda sahihi kuanza shule na kupata wepesi wa kuelewa. Muda wa kuwa darasani upungue yani miaka iwe michache na wasome vitu vyenye tija tu kwa nadharia na vitendo kuanzia awali hadi elimu ya juu. Mfano kama mfumo wa sasa mwanafunzi anaweza soma miaka miwili sekondari na akafanya vizuri, ni vizuri mfumo huu utumike kusoma kidato cha kwanza hadi cha sita kwa miaka mitatu na marekebisho ya mtaala ubadilike ili miaka ya elimu msingi pia ipungue.

Tabia; elimu yetu inapaswa kujumuisha swala la malezi katika mtaala kwa sababu malezi huzaa tabia. Liandaliwe somo la malezi ambalo litakua likiongoza matendo ya mtu kuanzia akiwa mtoto. Mfumo ulioko haumfunzi mtoto uzalendo, haki na ujasiri ndio maana taifa letu lina Watoto na watu wazima waoga wasioweza kujisimamia wala kusimamia wengine, pia ongezeko lajamii, viongozi na watendaji wasiowajibika na wapenda rushwa. Somo hili linaweza kuandaa kizazi chenye watu jasiri, wazalendo, wanaojitambua na wanaowajibika hii itasaidia katika maendeleo ya taifa kwasababu watu watakua wanaojiamini, wanaojituma, wanaowajibika pale wanapokosea, hakutakua na vibaraka wa mataifa mengine wala ukoloni mamboleo kwa sababu kutakua na umoja.

Elimu na siasa; ni wakati sasa serikali kufanya maamuzi ya kutenganisha utendaji wa maswala ya siasa haswa maswala ya vyama na elimu, hii ni kwasababu elimu imekua sehemu ya kupigia upatu maswala ya vyama vya siasa mfano swala la vyama vya siasa katika ngazi ya elimu ya juu haziendeshwi katika njia sahihi hivyo ni vyema kama serikali imeona maswala ya siasa kuwepo kwenye ngazi ya fulani ya elimu ni bora, basi elimu hiyo ya siasa iwepo kuanzia ngazi ya chini sana, na elimu hiyo itenganishwe na vyama ili watu wawe na mwanga angavu kuhusu siasa ya nchi yao na wajue majukumu yao kama wananchi ni yapi, ili ikifika muda unaowaruhusu kufanya maamuzi kwa ajili ya taifa wafanye maamuzi sahihi kwa ajili yao na taifa zima bila kufanya maamuzi kwa maslahi binafsi au maslahi ya chama Fulani.

MWISHO

Ni muda sasa kwa taifa kusimama pamoja kufanya mabadiliko sahihi na kwa wakati sahihi, ni muda sasa wa watu kuwa watendaji sana kuliko waongeaji ili tukapate kuona mafanikio tunayoyatamani sana kwa muda mrefu. Viongozi wafanye maamuzi yenye tija kwa ajili ya taifa letu wajifunze kufanya tathmini ya mambo ili waweze kutuvusha kwa wakati unaostahili. Viongozi wakumbuke “tunatamani kufanikiwa na kufika mbali sana kama taifa lakini kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya kutufikisha TANZANIA TUITAKAYO wafanye tathmini ya jambo husika kwa upana sana, kwa kuzingatia muda na lengo (faida). Hivyo kuna muda kuliko kuwai kufanya jambo na kupoteza kikubwa ni heri kusubiri kufanya kwa ubora ili kupata kilicho bora Zaidi”.​
Imekaa poa sana hii.
Tuijenge Tanzania pamoja
 
Back
Top Bottom