SoC04 Tanzania tuitakayo: Mfumo wa kujulisha na utambuzi wa vitu vilivyopotea na kupatikana katika jamii zetu

SoC04 Tanzania tuitakayo: Mfumo wa kujulisha na utambuzi wa vitu vilivyopotea na kupatikana katika jamii zetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

John Sule

Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
85
Reaction score
97
Je, Ushawahi kupotelewa kwa Kitu cha “Thamani” au “Muhimu” …? Upatikanaji wake ulikuaje…Ulifanikiwa au Hukufanikiwa…TUANGAZIE MBINU NA NAMNA YA KULITATUA SWALA HILI.

UTANGULIZI:
Natumaini kundi kubwa la watu wengi wameshawahi kupotelewa na kitu fulani iwe kikubwa au kidigo kithamani, Muafaka au mwisho wake ulikuwa ni upi? Idadi kubwa ya watu ulimwenguni hupotelewa na mali, fedha na n.k huenda kwa kuibiwa, kusahau walipoweka au kudondosha kwa bahati mbaya bila ya wao wenyewe kukusudia. Kitu cha “Thamani” Mfano; Kompyuta mpakato(Laptop), Simu, Pesa Taslimu na N.k. Kitu cha “Muhimu” Mfano; (Vitambulisho) kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha kazi, kadi ya benki, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha chuo, Leseni ya udereva, Bima ya Afya na N.k

Kuwe na Mfumo ambayo watu watajiunga kwa kujisajili kwenye mfumo ili kuweka vitu vilivyookotwa na vitu vilivyopotea , mtu akiokota mali ya mtu ambayo siyo yake ataviainisha kwenye mfumo, huku pia watu waliopotelewa na mali zao watapaswa waingie kwenye mfumo ili kuzitafuta mali hizo. Aliyepoteza atatakiwa aweke taarifa sahihi za mali alizopoteza ili aliyeokota aweze kuridhishwa na maelezo yake ili aziwasilishe mali hizo kwa muhusika huyo moja kwa moja. Ikitokea muhusika huyo alikuwepo Dar es salaam na kitendo hicho cha upotevu wa mali zake ulitokea akiwa jijini hapo na yeye ni makazi wa arusha basi atalazimika kuzifata mali zake au kutumiwa huko huko aliko mkoani Arusha kwa garama zake mwenyewe.

CHANGAMOTO YA UPOTEVU WA MALI/KITU:
Watanzania Tunapaswa Kuwa na Umoja Na Upendo Baina Yetu. Serikali haiwezi kufanya kila kitu, sisi Wanachi ndiyo wahanga wakubwa wa kupotelewa na mali kwahiyo tunapaswa kuja na mikakati ya kuweza kujikomboa na changamoto ndogo ndogo kama hizi. Wanchi wa Taifa la Tanzania inabidi tuishi kwa upendo na kujaliana sisi wenyewe kwa wenyewe, karibia kila mmoja wetu hupotelewa na vitu. Uonaonaje kuleta tabasamu na furaha kwa muhanga wa kupolewa na kitu chake cha thamani au muhimu.

DHUMUNI LA TEKNOLOJIA HII:
•Ni kurahisisha upatikanaji na utambuzi za vitu/mali zilizopotea kwa wahusika wa mali hizo.
•Kuutarifu umma/jamii ya eneo husika kuwa unatafuta au umepotelewa na kitu Fulani.
•Kupashana Habari na taarifa maeneo mbali mbali upotevu na upatikanaji wa mali.
•Kukuza utamaduni kwa jamii yetu wa kurejesha/kujulisha na kotoa taarifa kwa upatikanaji na upotevu wa mali isiyo yako.

CHANGAMOTO ZA UTEKELEZWAJI WAKE:
Tuangazie kwenye usafiri wa umma, Mfano; Mwendokasi kwa jiji la Dar es salaam, Treni za umma, Mabasi ya mikoani na usafiri wa majini (Meli na Boti). Mara nyingi unaweza kuona Vitambulisho mbali mbali huwekwa mbele ya vyombo vya usafiri kama vile basi au daladala. Tuangazie Pia sehemu za umma Mfano; Masoko, Stendi ya Mabasi, Stendi ya Dalala, Stendi ya Mwendokasi(Vituo vya Mwendokasi), Shule za( msingi na sekondari, Vyuo vikuu na vyuo vya kati, Mahakama na n.k. Sehemu kama hizi zenye mkusanyiko wa watu upotevu wa vitu hutokea mara nyingi mnoo hapa haijalishi umeibiwa au umedondosha yote ya yote utakuwa umepoteza tu!

FAIDA ENDELEVU:
Umma wenye udhubutu: Hudumisha umoja na mshikamano baina yetu watanzania, kupitia Faraja na amani ya kupata kilichopotea. Hupunguza garama na kuokoa muda kwenye utafutaji wa mali zilizopotea, Kama unavyojua ufatiliaji wake na pesa zitumikavyo kufatilia yote hayo. Kukuza elimu ya kuripoti na urejeshaji wa mali ambazo siyo za kwetu, tunaijenga nchi ya watu muhimu kwa wote na bora zaidi kwa kila mmoja wetu.

UHAMASISHAJI NA ELIMU KWA UMMA:
Wangapi wamewahi kuokota au kuapata mali isiyo yake na kupeleka kituo cha polisi kwaajili ya utambuzi zaidi wa hizo mali? Mfano; simu, pesa taslimu, kitambulisho chochote kile na N.k

Kwasasa tuanzie na zoezi la kuzipeleka mali ulizookota kwenye mamlaka husika ambazo ni Kwenye kituo chochote cha polisi kilichopo karibu yako kwaajili ya utambuzi zaidi wa hizo mali kwa wahusika. Nafahamu watanzania wengi tunaogopa kupeleka vitu vilivyookotwa polisi kwaajili ya utambuzi wa wahusika wa mali hizo, sasa basi wala usiwe na shaka kuripoti mali uliyookota , Ukifika polisi utatoa maelezo kuhusu ujio wako pale na kutoa maelezo juu ya hivyo vitu ulivyowasilisha pale na wao watasaidia kumpata muhusika wa hizo mali.

Tunaweza kubadilika na tukafikia huko pakurudisha mali ulizookota kwa muhusika ambazo siyo mali zako, Wapo watanzania wenzetu wachache washafika huko , wakiokota mali za watu huwarudishia wahusika wa hizo mali haijalishi inathamani kwa ukubwa gani.

USHAURI:
Tuanzie kujizoesha na utamaduni huu mdogo mdogo kwa kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter(X), Pinterest na Threads kutuma mali za watu zilizopotea na kupatikana. Unaweza kupost kitu ulichookota bila kujali kinathamani gani, huenda kwako hakina thamani ila kwa aliyepoteza kikawa na thamani mnoo kwahyo tufanya kwa upendo na kujali mali za watu huko mitandani kitaonekana watu wataambizana mwishowe kitamfikia muhusika, pia unaweza kuwa tumia watu mashuhuri au wenye wafuasi wengi zaidi mitandaoni wakatangaza kwenye kurasa zao watu wengi zaidi wakaona na ujumbe ukamfikia muhusika pia.

MAPENDEKEZO:
Serikali kushirikiana na wadau wa sekta binafsi wanahitajika kuja na mifumo ya namna hii ili kupunguza upotevu na kuimarisha usalama wa mali za raia wake. Serikali kwa kushirikiana na wananchi na asasi za kiraia kuweka masanduku kwenye kila eneo la mkusanyiko au makundi kdhaa ya watu Mfano; Vyuoni, Mashuleni, Mahospitalini, Masokoni, Minadani, Vituo vya Mabasi na N,k.

HITIMISHO:
Kwenye ukuzwaji wa Matumizi ya teknolojia nchini mwetu “TANZANIA” kwenye kila sekta kutakuza maenedeleo binafsi na nchi kwa ujumla, mfano sekta ya kilimo, biashara, huduma za kifedha, Habari na mawasiliano, uchukuzi na usafirishaji ili kuboresha ufanisi na kuleta mabadiliko Chanya. Vitu hivi hueanda vikauzika au visiuzike baada ya kuokotwa hata pengine kuibiwa kutoka kwa wahusika wa vitu hivyo. Mfano wa hivyo vitu ni kama Vitambulisho vya (kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha kazini, kadi ya benki, Kitambulisho cha Taifa, Hati ya kusafiria, Leseni ya udereva) na mali au fedha taslimu. Unajiskiaje kupata vitu vyako baada ya kuvipoteza na kuvitafuta bila mafanikio kwa muda Fulani iwe muda mfupi au mrefu, Ni furaha kweli kupata kitu ulichokipoteza au kuibiwa.

IMG-20240422-WA0011.jpg
IMG-20240422-WA0016.jpg
IMG-20240422-WA0015.jpg
Screenshot_20240605-100159_Facebook.jpg
Screenshot_20240505-165600_WhatsAppBusiness.jpg
 
Upvote 4
Watanzania Tunapaswa Kuwa na Umoja Na Upendo Baina Yetu. Serikali haiwezi kufanya kila kitu, sisi Wanachi ndiyo wahanga wakubwa wa kupotelewa na mali kwahiyo tunapaswa kuja na mikakati ya kuweza kujikomboa na changamoto ndogo ndogo kama hizi. Wanchi wa Taifa la Tanzania inabidi tuishi kwa upendo na kujaliana sisi wenyewe kwa wenyewe, karibia kila mmoja wetu hupotelewa na vitu. Uonaonaje kuleta tabasamu na furaha kwa muhanga wa kupolewa na kitu chake cha thamani au muhimu
Ahsante kutukumbusha hili, na kuwa mfano mojawapo wa kuiishi imani katika ubinadamu. Wanaita 'Faith in humanity restored'. Utalipwa kwa afya ya mwili akili na uchumi, ubarikiwe🙏

. Unajiskiaje kupata vitu vyako baada ya kuvipoteza na kuvitafuta bila mafanikio kwa muda Fulani iwe muda mfupi au mrefu, Ni furaha kweli kupata kitu ulichokipoteza au kuibiwa.
Ina hisia nzuri sana. Tujaliane
 
Ahsante kutukumbusha hili, na kuwa mfano mojawapo wa kuiishi imani katika ubinadamu. Wanaita 'Faith in humanity restored'. Utalipwa kwa afya ya mwili akili na uchumi, ubarikiwe🙏

Ina hisia nzuri sana. Tujaliane
Hapa ndipo Ujamaa na upendo baina yetu unaweza rudi, watanzania hatupendani sisi kwa sisi...halafu tunahitaji kupendwa na mataifa mengine kama kenya, uganda n.k Upendo uanzie Nyumbani kwanza kwa namna yoyote ile...... kwa kufanya hivi Upendo baina yetu unaweza kukua🙃🙂
 
Hii ni nchi ya watu kwa asilimia 99.9% ni wenye hulka ya wizi
Haitowezekana, fikiria umepoteza funguo zako za gari na pia kuna
za nyumba yako
Mbulula akiziokota ndio zinakuwa za kuning'iniza kwenye lux za suruali aonokane mpambanaji wa maisha
 
Uko sahihi kuna wapo wanaoweza kurudisha na wapo amabao hawawezi......sasa inabidi tuwe taifa la Wasiyo-Wezi ili turudishiane vitu vyetu tulivyovipoteza sisi wenyewe kwa wenyewe........Usiseme haiwezekani! Tujaribu na tufanye huende ikawezekana....
 
Wazo ni zuri..

Ingawa miaka ya nyuma sina uhakika kama ule mfumo upo bado..

Kuna utaratibu wa kusajili kifaa chako katika database mapema kabisa kabla hakijapotea au kuibiwa.

Then, ikija kutokea imepotea/kuibiwa basi unarudi katika ule mfumo kubadiri status na kuiblack list hicho kifaa..

Means kama kitauzwa basi mnunuaji atapata shida..

Mnunuaji/Wanunuaji walikuwa encouraged kuingia katika huo mfumo kabla ya kunuanua device yoyote ile kujihakikishia ile mali si ya wizi au iliyopotea ambayo inatafutwa.. BLACK LISTED

Sina uhakika kama ule mfumo bado upo.. ni siku nyingi hasa..
 
Huu ni utakuwa kwaajili vya vitu vilivyopotea na kupatikana kwa maeneo yote Tanzania, pia utapunguza hulka ya wizi kwa sisi wenyewe kwa wenyewe, lakini siyo vitu vyote vinavyoibiwa huuzika vingene hutupwa......Muokotaji ndiyo atatakiwa kuviripo kwenye mfumo kwaamaana kwenda polisi ni kipengele haswaa kwa watu wengi na ukilinganisha na sheria zetu zilivyo watu huogopa kusaidia polisi...
 
Hapa ndipo Ujamaa na upendo baina yetu unaweza rudi, watanzania hatupendani sisi kwa sisi...halafu tunahitaji kupendwa na mataifa mengine kama kenya, uganda n.k Upendo uanzie Nyumbani kwanza kwa namna yoyote ile...... kwa kufanya hivi Upendo baina yetu unaweza kukua🙃🙂
Hakika, na inaanza na mtu binafsi
 
Hii ni nchi ya watu kwa asilimia 99.9% ni wenye hulka ya wizi
Haitowezekana, fikiria umepoteza funguo zako za gari na pia kuna
za nyumba yako
Mbulula akiziokota ndio zinakuwa za kuning'iniza kwenye lux za suruali aonokane mpambanaji wa maisha
Hizo takwimu umezitoa wapi.?

Kuwa makini na unavyosema kwa watu unaiona dunia/nchi uliyopo maana asilimia 99.9% huwa ni vile unavyojiona binafsi (Hizi takwimu na mi nimetoa wapi?🤔)

Labda ndio kusema 99.9% ya takwimu za kujiandikia huwa zinatungwa 'on the spot' 😁😁😁😅
 
Hizo ni kwa mtazamo wake binafsi! Hakuna takwimu rasmi zilizotoa tafiti kuwa Watanzania 99.9% wana hulka ya Wizi "HAPANA"
 
Hii ni nchi ya watu kwa asilimia 99.9% ni wenye hulka ya wizi
Haitowezekana, fikiria umepoteza funguo zako za gari na pia kuna
za nyumba yako
Mbulula akiziokota ndio zinakuwa za kuning'iniza kwenye lux za suruali aonokane mpambanaji wa maisha
😁 😁 😁 😁 Asee Mungu anakuona, kubeba funguo nyingi saivi fashen au sio
 
Wazo ni zuri..

Ingawa miaka ya nyuma sina uhakika kama ule mfumo upo bado..

Kuna utaratibu wa kusajili kifaa chako katika database mapema kabisa kabla hakijapotea au kuibiwa.

Then, ikija kutokea imepotea/kuibiwa basi unarudi katika ule mfumo kubadiri status na kuiblack list hicho kifaa..

Means kama kitauzwa basi mnunuaji atapata shida..

Mnunuaji/Wanunuaji walikuwa encouraged kuingia katika huo mfumo kabla ya kunuanua device yoyote ile kujihakikishia ile mali si ya wizi au iliyopotea ambayo inatafutwa.. BLACK LISTED

Sina uhakika kama ule mfumo bado upo.. ni siku nyingi hasa..
Huyu ni mwanafunzi wa chuo akilalamika kupoteza vitu vyake!
 
Attachments

  • Screenshot_20240505-165600_WhatsAppBusiness.jpg
    Screenshot_20240505-165600_WhatsAppBusiness.jpg
    133.2 KB · Views: 5

Back
Top Bottom