Huu ni mradi bunifu wa kuitangaza Tanzania kwa njia ya vitabu, kwamba vitabu vinavyohusu hadithi na matukio ya kitalii, vivutio, wanyama pekee, picha za maeneo ya kitalii vitakuwa katika simulizi nzuri na kusambazwa kwenye shule za msingi, upili na vyuo katika bara la Ulaya, Amerika na Asia.
JE MRADI WA VITABU ni nini? ni vitabu vya simulizi za wanyama, matukio, historia na maeneo ya utalii ambavyo vitakuwa vikiandikwa na kusambazwa barani Ulaya, Amerika na Asia kwa lengo la kuandaa watoto kuanzia miaka 7-18 kuwa watalii wa Tanzania katika siku zijazo lakini pia kuitangaza nchi yetu kwa namna mpya.
JE NI YAPI MALENGO LA MRADI HUU?
MOSI, KUWAANDAA WATOTO NA VIJANA TOKA BARA LA ULAYA, ASIA NA AMERIKA KUWA WATALII WETU SIKU ZIJAZO.
Kwamba kupitia simulizi za wanyama, jamii zinazoishi karibu na maeneo ya utalii na matukio ya utalii kunaweza kuwa ni sababu ya kuandaa watoto katika nchi husika katika siku za usoni kuja kutalii nchini kwetu kwa sababu wanakuwa wameona na kusoma kuhusu wanyama wa kipekee tulionao, maeneo ya utalii, matukio ya kitalii, huduma za kitalii na bidhaa za kitalii.
Hii maana yake nini? Leo vijana wengine hasa mimi tumekuwa tunatamani kwenda nchi za Ulaya na Amerika kwa sababu toka utotoni kwetu tumekuwa tunahadithiwa na kusoma juu ya tamaduni za nchi hizo na maendeleo yake.
Mfano wa 1: wa simulizi: simulizi ya FARU JOHN, FARU FAUSTA,matukio ya kitalii ya historia za Zanzibar na utumwa, TUKIO LA KUHAMA KWA WANYAMA KATIKA MBUGA YA SERENGETI, simulizi ya Mlima Kilimanaro na watu wake, simulizi za SOKWE KWENYE MBUGA YA GOMBE NA MAHALE, simulizi ya kusisimua ya MV LIEMBA n.k.
Pili, KUWAPA WATU SABABU YA KUJA TANZANIA KUTALII
Imani yangu kuwa baada ya miaka 10-25 watalii watakuja kwa wingi Tanzania kwa sababu wanataka aidha kuthibitisha kile walichokisoma kwenye simulizi za vitabu vyetu, kushuhudia kwa macho yao matukio ya kitalii baada ya kusoma, kuja kufanya utafiti juu ya matukio ya kitalii waliyoyasoma, au kuja kwa sababu ya kuona jamii ya Tanzania waliyoisoma.
JE NI NAMNA GANI VITABU HIVI VITAKAVYOSAMBAZWA: -
Mosi, KUPITIA MAKTABA ZA SERIKALI, SHULE NA VYUO.
Kwamba; vitabu vitatolewa bure kwenye maktaba za serikali, shuleni na vyuoni kwa nchi husika zitakazolengwa kwenye mradi huu.
Mfano wa 2: Tunataka kuinua Utalii nchini Argentina, basi vitabu vinavyohusu simulizi za utalii toka Tanzania vitawekwa kwenye maktaba za serikali za nchi ya Argentina ili watu wanaofika kwenye maktaba kujisomea wapate pia kuviona vitabu hivi na kuvisoma.
Mfano wa 3: Tunataka kutangaza utalii nchini Canada kwa kuwalenga wanafunzi wa shule za msingi basi tutaweka vitabu kwenye shule za msingi kama: SAINT HELANA ELEMENTARY SCHOOL, +17079672772
Mfano wa 4: kama tunalenga kutangaza utalii nchini Japan, vitabu vitatolewa bure kwenye vyuo kama UNIVERSITY OF TOKYO, TOHOKU UNIVERSITY, KYOTO UNIVERSITY, NAGOYA UNIVERSITY, OSAKA UNIVERSITY n.k.
Pili, kupitia mabalozi za Tanzania, kwamba balozi zote za Tanzania zitakuwa na utaratibu wa kugawa vitabu hivi kwa wateja wao kama zawadi ya kuichagua Tanzania.
JE VITABU HIVI VITAKUWA NA TAARIFA GANI NYINGINE UKIACHA SIMULIZI?
Kwamba, vitabu vitakuwa vina siumulizi fupi sana ambazo hazizidi maneno 500 (kursa 20-30) na pia Vitabu vitakuwa na taarifa za Tanzania juu ya idadi ya watu, mipaka ya nchi, namba za dharura, huduma za kitalii, aina ya utalii na sera ya nchi kuhusu utalii kwenye kurasa tatu za mwisho baada ya simulizi kuisha.
JE WATALII PEKEE NDIO WANALENGWA NA MRADI HUU?
Hapana, bali ni Imani yangu kuwa simulizi nzuri za matukio ya kitalii zitaweza pia kuwahamasisha au kuzishawishi kampuni kubwa za filamu, matukio na picha kuja Tanzania kufanya kazi na kuwekeza kwenye tasnia ya filamu nchini kupitia sekta ya utalii.
MFANO5: simulizi bora na yakuvutia kuhusu FARU JOHN; ni faru wa ajabu kuwahi kutokea duniani, Faru huyu mwenye sifa za kibidamu za wivu, kujali, Kujidai, kupenda kupilitiliza na kujipenda anapambana kuwaangamiza wenzake ili kujenga milki ya kizazi chake na kuifanya dunia (Mbuga) kuwa salama katika kizazi chake. Fikiria hii tu ikiwa kama ni filamu ya watoto.
JE KUNA FAIDA YA MRADI HUU KATIKA MIAKA 10-25 IJAYO?
Ndio! Ukiacha Kwamba; watalii watakuwa na sababu ya kuja Tanzania kutalii na kujifunza juu ya matukio yaliyopo kwenye simulizi za vitabu jambo ambalo awali halikuwepo. Lakini pia mradi huu utasisimua watoto na kuwahamasisha wazazi wao kuwaleta Tanzania, utawafanya vijana wengi kutaka kuijua Tanzania zaidi kupitia mitandao ya kijamii kama mtando “Google.com” lakini utaifanya Tanzania kuwa nchi maarufu mashuleni na vyuoni katika siku zijazo.
JE MRADI HUU UTAONGEZA AJIRA ZAIDI KWENYE SEKTA YA UTALII?
Ndio! Kuongezeka kwa watalii nchini kutaongeza mzunguko wa fedha za kigeni, kuwapa soko wauzaji wa bidhaa za kitalii, kuwapa fursa watoa huduma za kitalii na waongozaji wa watalii nchini.
JE MRADI HUU UTAIFANYA TANZANIA KUWA NCHI PEKEE DUNIANI INAYOTUMIA UBUNIFU KUTANGAZA UTALII?
Mpaka naandika andiko hili na kuliweka Jamii Forum kama sehemu ya mchango wangu kwa Taifa langu bila shaka Hakuna nchi inayotumia njia hii kwa sasa kutangaza utalii na hivyo kwa ubunifu huu utaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kujitangaza kiutalii na kuwaandaa vijana wadogo wa Bara la Ulaya, Bara la Amerika na Bara la Asia kuwa watalii wa kesho wa Tanzania.
JE YAPI MAJUKUMU YA WIZARA YA UTALII NA MALIASILI KATIKA MRADI HUU?
Mosi, Kwamba wizara itaunda kamati maalum ya mradi huu na pia Wizara itagharamikia uandishi na uchapishaji wa vitabu kisha kuvisambaza kwenye nchi husika kama sehemu ya kutangaza utalii kwa muda mrefu zaidi na kwa gharama nafuu. Na Pili, Wizara itagharamia gharama za kutafsiri vitabu husika.
Kwamba, Wizara itaingia gharama katika kutafsiri simulizi kwenye lugha za kimataifa kwa lengo la kuleta ubora wa kazi na kufanya kazi ifike kwa watu wengi Zaidi na lugha pendekezwa: kama KINGEREZA, KICHINA, KIFARANSA, KIHISPANIA
Neno langu la mwisho kuhusu mawazo bunifu yangu, natumai nimetumia jukwaa hili kutoa maono na mawazo bunifu kwa faida ya nchi yangu na sio kwa faida yangu au marafiki zangu au familia yangu na kuwa nipo tayari kuwajibika kama mawazo bunifu yatakuwa madhara hasi kwa nchi yangu. ASANTE!

Upvote
1