SoC04 Tanzania tuitakayo na safari ya kuifikia nchi ya ahadi

SoC04 Tanzania tuitakayo na safari ya kuifikia nchi ya ahadi

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 23, 2020
Posts
12
Reaction score
23
Tanzania ni nchi inayopatikana ndani ya bara la Africa na ipo kwenye ukanda wa Afrika ya mashariki pia kusini mwa jangwa la sahara,ni nchi inayoundwa na nchi mbili ambazo ziliamua kuungana mnamo tarehe 26/04/1964. Muungano huu ulifanyika kwa Jamhuri ya watu wa Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar walipoamua kuungana kutokana na sababu za kijiografia, kihistoria na hata kiusalama na kuunda nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9, 1961 kutoka katika makucha ya mkoloni ambaye alikuwa mwingereza aliyepewa dhamana ya kututawala na kutuandaa kupata uhuru na Umoja wa mataifa, Zanzibar nayo ilipata kujikomboa kwenye makucha ya utawala wa kisultani ulioachwa na mwingereza Januari 12,1964 mara baada ya kufanya mapinduzi matukufu.

Tanzania ipo katika nyuzi 0 na 12 kusini mwa ikweta na nyuzi 12 hadi 40 mashariki mwa Greenwich. Tanzania inapakana na Kenya na Uganda (Kaskazini); Rwanda, Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (Magharibi); Zambia, Malawi na msumbiji (Kusini) na Bahari ya Hindi ( Mashariki). Tanzania ina eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 945,203 likijumuisha maeneno ya maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa pamoja na mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko milima yote Afrika. Nchi ya Tanzania imesheheni vivutio kedekede na vikubwa vya kitalii ikiwemo mbuga za wanyama, hifadhi za taifa, fukwe za bahari, milima na mabonde. Tanzania ina Rasilimali nyingi zikiwemo ardhi, madini, gesi asilia, misitu, mazao ya kilimo, mifugo, samaki na ambazo ndizo nguzo kuu za uchumi wa Taifa.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi mwaka 2022, Tanzania ina idadi ya watu wapatao milioni 61.7,Zanzibar ina jumla ya watu watu 1,889,773 na Tanzania bara ina watu 59,851,357. Taifa hili lina watu wenye makabila 125 na jamii zenye tamaduni mbalimbali za asili kama Wasandawe, Wamasai, Wahadzabe, Wabarbaig na Watumbatu. Pamoja na wingi wa makabila haya Kiswahili imekuwa ni lugha kuu inayounganisha watanzania wote na kuwaleta pamoja. Kiutawala Tanzania imegawanyika katika mikoa 31(Tanzania bara ina mikoa 26 na Zanzibar ina mikoa mitano) na ambayo imegawanyika katika wilaya,kata au shehia na vijiji au mitaa. Mhimili mkuu mikuu ya dola ni Bunge au Baraza la wawakilishi, Mahakama za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mahakama za Zanzibar na Tanzania Bara, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Pamoja na dola, asasi za kiraia na sekta binafsi hushiriki kikamilifukatika maendeleo ya nchi kwenye Nyanja za kiuchumi, kijamii,kisiasa na kiutamaduni. Kuelekea Tanzania tuitakayo miaka 50 ijayo tunaitaka Tanzania yenye;

Uhuru wa vyombo vya habari na kulindwa kwa Waandishi dhidi ya dola na jamii kandamizi, Katika nchi ya kidemokrasia uhuru wa watu kujieleza, kutoa taarifa na kupata taarifa ni moja ya jambo la muhimu na kubwa zaidi. Waandishi makini na wenye weledi na hatari kwa utawala wenye mashaka na dhalimu lakini ni hazina kwa jamii yenye wanyonge, kufikia mwaka 2074 tunaitaka Tanzania itakayoheshimu uhuru wa vyombo vya habari na kuheshimu waandishi wa habari ili wafanye kazi zao katika mazingira salama. Ili kufikia Tanzania huru kwenye vyombo vya habari ni lazima kufanya mabadiliko katika sheria inayompa mamlaka waziri wa Habari juu ya Vyombo hivi, lazima kufanywa mabadiliko katika katiba yetu au katiba mpya itakayopatikana lazima izungumzie uhuru wa vyombo vya habari kwa kina na upana wake. Mfano katiba ya Ghana ya mwaka 1996 imezungumza kwa kina zaidi na ndani ya katiba hiyo kuna sura moja ambayo inazungumza uhuru wa vyombo vya habari.
Screenshot_20240615-080822~2.png


Chanzo; Katiba ya Ghana ya 1996

Waandishi wa habari watakapo kuwa huru na kulindwa wanaweza kuandika kwa weledi habari za kiuchunguzi haswa katika Nyanja ya siasa, utawala pamoja na uchumi na kupitia taarifa hizi nyeti zitasaidia wananchi kutathimini utendaji wa watu ambao wamewachagua na kuwaweka madarakani lakini wale ambao wana wawakilisha. Vyombo vya habari vitakapo kuwa huru na kulikwepa rungu la dola vitaweza kusawazisha mizania ya usawa katika ukusanyaji na utowaji wa taarifa haswa zile zinazohusu uchaguzi na kampeni za uchaguzi mkuu. Hivi sasa tunaona kuwa mizani ya utoaji wa taarifa haswa nyakati za uchaguzi mizani imeegemea zaidi upande mmoja ambao ni wa chama tawala lakini pia taarifa nyingi zinazooneshwa haswa kwenye vyombo vya habari vya Taifa nyingi zinahusu serikali tu na hata vyama vingine ambavyo havijaunda dola pia vinapata wakati mgumu kutumia vyombo hivi vya habari. Katika video hii kuna takwimu zinazoonyesha kutokuwepo kwa usawa wa kimizania na uwiano sambamba wakati wa kuripoti taarifa mbalimbali za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

1718708226368.png


Chanzo; GLOBAL TV ONLINE.​

Kufikia mwaka 2074 tunataka vyombo vya habari vya Taifa kurudi mikononi mwa wananchi na visiendeshwe na serikali ili vipate uhuru kamili na kuweza kuripoti na kutoa taarifa zisizo na kuegemea upande mmoja. Kama tutafikiria namna ya kuweka ada katika visimbuzi wakati wa mtu anapokwenda kununua pia wakati wa ulipiaji wa malipo ya vifurushi vya mwezi ili vyombo hivi vya umma viweze kujiendesha venyewe pasipo kutegemea kuendesha na serikali au kupewa fungu na serikali na jambo hilo kusababisha kupangiwa namna gani wao watakavyoendesha vyombo hivyo, kuripoti habari lakini kuangalia nani haruhusiwa kutumia na nani anaruhusiwa ilhali ni vyombo vya umma na vipo kwa ajili ya malsahi ya umma.

Kwa kuhitimisha, Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu sana kwa taifa la kidemokrasia na linalohitaji kupiga hatua kwakuwa waandishi wenye weledi wanaiweza kuchambua siasa, uchumi na kuhabarisha umma ili kuchochea fikra chanya na zenye mabadiiko kwa kuzingatia miiko na maadili ya tasnia hiyo na wataweza kuonyesha wazi dosari za mfumo wetu wa kisiasa,kiuchumi na kijamii. Kuvipa uhuru zaidi vyombo vya habari kutavifanya kuviondoa mikononi mwa watawala wanaovifanya kama vipaza sauti vyao vya kusema ana kutoa ajenda zao
 
Upvote 1
Back
Top Bottom