SoC04 Tanzania tuitakayo: Tuende kubadili Sheria ili Mashirika yetu ya Umma yawe na ufanisi kiasi cha baadhi yao kujiorodhesha kwenye soko la hisa la Dar

SoC04 Tanzania tuitakayo: Tuende kubadili Sheria ili Mashirika yetu ya Umma yawe na ufanisi kiasi cha baadhi yao kujiorodhesha kwenye soko la hisa la Dar

Tanzania Tuitakayo competition threads

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Tuanze kuwaza sasa kama nchi kubadilisha sheria zinazo simamia haya mashirika ya umma ili kuongeza ufanisi.

Mashirika mengi ya umma yanalalimikiwa kwamba hayana ufanisi, yanajiendesha kwa hara, wafanyakazi hawajitumi na kadhalika ila hatujawahi sana kukaa kama taifa kuona tunatoka vipi hapa tulipo na haya mashrika ya umma.

Ni ukweli kwamba mashirika mengi sana ya umma yamekuwa hayana ufanisi ukilinganisha na kampuni za biashara na sababu kubwa pia imekuwa ni kwamba yale ni mashirika ya umma hayana mwenyewe kamili, ni shamba la bibi, Wakurugeniz hawana ownership pale, Bodi pia vivyo hivyo.Yamegeuka kuwa vituo vya upigaji na baadhi hata yanaelekea kufa kabisa au yamekuwa ni mzigo kwa Serikali.

Ukitazama mashirika kama TTCL hata shirka la posta yalipaswa kwa sasa mfano, shirika kama TTCL liwe linashindana na makampuni ya simu kama Vodacom au Tigo au Airtel, lakini hakuna kitukama hicho na ukilinganisha hayo makampuni ya simu na TTCL ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu. TTCL ni kongwe kabla ya kampuni zote hizo ila leo hii TTCL in inapumulia mashine ya oxygen iko taabani. Ukiachana na mambo ya siasa na maswala mengine ila pia ukweli unabakia kwamba sheria zinazo simamia haya mashirika ni kikwazo kikubwa sana, hakuna ownership pale, Wafanya kazi na wakurugezi hawana ila commitement na shirika, mkurugenzi wakati wowote anaweza tenguliwa na akaletwa mwingine.

Mashirika yanakosa ufanisi kwa sababu sheria ni mbovu na yamegeuka kuwa vitege uchumi vya baadhi ya viongozi wan nchi. Sheria zinazo yasimamia ni kama zisha pitwa na wakati,

Shirika kama UDA linalo endesha mabasi ya mwendokasi linakosa kabisa ownership, mabosi wanawaza ni lini watabadilishwa na aletwe mwingine,Viongozi wakubwa wanaingilia shirika, Shirika linakosa ufanisi kabisa pamoja na kuwa na monopoly ya Barabara zake. Mifano ni mingi sana kwa Mashirika ya umma ambao yanapaswa kufanya biashara z ushindni ila hayafanyi hivyo.

Haya mashirika yanapaswa kuisaidia nchi kwenye kukuza uchumi badala ya ilivyo sasa ambapo yamegeuka kuwa mizigo mikubwa sana kwa walipa kodi, Shirika kama UDA unaweza shangaa kodi za wananchi tena ndio zinaenda kulipa miashara ya wafanya kazi kwa sababu shirika halijiendeshi kwa faida linaendeshwa kwa mujibu wa siasa.

Nini sasa kifanyike ili haya mashirika yaweze kuisadia nchi na yasiwe mizigo kwa walipa kodi wan chi hii kama anavyo sema mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.
  1. Mashirika yote ya umma wakurugenzi wawe wanatafutwa kwa njia za ushindani na nafasi zinakuwa wazi hata kwa watu wasio watanzania kuomba kazi ya kuwa mkurugenzi wa shirika, tuanchane na teuzi. Kuteua wakurugenzi ni tatizo kubwa sana kwa mashirika ya umma, teuzi nyingi ni za kisiasa na zinaweza kuwa ni za kujuana au kulipana fadhila, hii ni sababu moja wapo ya kudidimiza haya mashirika ya umma kwa sababu wanateuliwa watu wasio kuwa na uwezo wa kuendesha mashirika, au wanawekwa pale kwa kujuana tu na sio kwa uwezo walio nao wa kuendesha biashara.Hili limesababisha mashirika mengi sana kudolola na hapa kwa sababu ya teuzi muda wote mkurugenzi anawaza ni lini kazi itaisha.Moja ya siri ya nchi za kiarabu kufanya vyema ni kuwakabidhi wageni mashrika yao, yale mashirika ya ndege ya kiarabu yanaendeshwa na Wageni. Akipatikana mtalamu wa kigeni basi achukuliwe kwa sababu hataondoka na shirika bado shirika litaendelea kubakia ni mali ya umma, tuache huu utamaduni wa sasa wa kuteuana na baadae tunaanza kulalamika kwamba mashrika hayafanyi vyema, shirika haliwezi fanya vyema wakati teuzi ni za kujuana.
  2. Wafanya kazi wa shirika na bodi ya wakurugenzi waanze kuwa sehemu ya shirika na wawe wanapata gawio pale shirika linapo fanya vizuri au kutengeneza faida. Kuwapa gawio wafanya kazi wote inaweza kuwa ni moja ya njia inayo weza kuleta hamasa kubwa sana ya ufanyaji kazi na pia italeta ownership, wafanyakazi watafanya kazi wakijua kwamba na wao ni sehemu ya shirika au watapata faida pale shirik litakapo fanya vizuri.Hii inaweza waongezea nguvu sana wafanya kazi kufanya kazi za kuishindani dhidi ya makampuni binafisi kwenye biashara. Serikali inaweza anza kuwaza hii wazo la kubadili kama ni sheria ili kuwa sasa mashirika yote yanayo tengeneza faida sehemu ya faida iende kuwa gawio kwa wafanya kazi na bodi yote ya wakurugenzi.Kuna mashrika yanajitahidi sana kufanya biashara ila unaona kabisa kuanzia body hadi wafanya kazi wanakosa ownership.
  3. Serikali iachanane na tenguzi za wakurugenzi, Wakurugenzi waachwe wafanye kazi zao na ufanisi ndio uwaondoe kazini kwa wao wenyewe kuondoka kwa sababau ya kuto kufikisha malengo ya shirika. Leo hii tenguzi haziaingalii kama Mkurugenzi anafanya kazi au la ila sana ni siasa ndio zinao fanya kazi na kutengua na kutea. Hizi tenguzi ndizo zinafanya wakurugenzi wawaze ni lini watatenguliwa badala ya kuwaza na kuweka mkakati ya miaka 10 ijayo kwenye shirika. Mkurugenzi hawezi weka malengo hata ya miaka mitano ijayo kwa sababu hana uhakika na kazi yake. Hii inasababisha awaze kuchuma pesa haraka haraka kabla hajatenguliwa au kuhamishwa.
  4. Serikali ianze kuwaza kuorodhesha mashirika ya umma yanayo fanya viziri kwenye soko la hisa la Dar es salaamu, hili linawezekana kwa kubadili sheria, yale mashirika yanayo fanya vizuri yaingie kwenye soko la hisa na watu wanunue hisa, hii inaweza kuwa ni sehemu nzuri sana ya shirik kukuza mtaji wake kuliko ilivyo sasa ambapo mashirik yanategemea sana Serikali. Nini kinakwamisha shirika kama Shirika la nyumba kuto kuingia kwenye soko la hisa? Mashrika kama TANAPA ynafaa kuwepo oko la hisa kukusanya mitaji. Hata shirila la umeme.Kuyaingiza mashirika ya umma kwenye soko la hisa kutapunguza mzigo mkubwa sana kwa serikali wa kuyaendesha haya mashrika ya umma.
  5. Mashirika ya umma yawe ni huru kwa asilimia 100, yasiingiliwe na mtu yoyote Yule hata kama ni Raisi wan chi, kuingiliwa ndio pia kumeyafikisha hapa yalipo kwa sasa, yawe huru kujiendesha na kufanya biashara kwa faida na hata yakitaka kuwekeza nje ya nchi yaende yafanye hivyo. Wazungu mashrika yao ya umma unakuta yamewekeza hadi nchi za nje kwa sababu yako huru.
Serikali ifanyie kazi haya mapendekezo ili kuleta ufanisi kwenye mashirika ya umma na kuyafanya yashindane kuliko ilivyo sasa ambapo hayaweza shindana na kampuni binafisi kwa sababu mbalimbali. Hii itasaidia kuondole Serikali mizigo ya kuendesha haya mashirika.
 
Upvote 4
Serikali iachanane na tenguzi za wakurugenzi, Wakurugenzi waachwe wafanye kazi zao na ufanisi ndio uwaondoe kazini kwa wao wenyewe kuondoka kwa sababau ya kuto kufikisha malengo ya shirika. Leo hii tenguzi haziaingalii kama Mkurugenzi anafanya kazi au la ila sana ni siasa ndio zinao fanya kazi na kutengua na kutea. Hizi tenguzi ndizo zinafanya wakurugenzi wawaze ni lini watatenguliwa badala ya kuwaza na kuweka mkakati ya miaka 10 ijayo kwenye shirika. Mkurugenzi hawezi weka malengo hata ya miaka mitano ijayo kwa sababu hana uhakika na kazi yake. Hii inasababisha awaze kuchuma pesa haraka haraka kabla
Hakika kazi ndo iamue
 
Back
Top Bottom