SoC04 Tanzania Tuitakayo: Watoto wetu hazina yetu

SoC04 Tanzania Tuitakayo: Watoto wetu hazina yetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Wanasema watoto wetu ni maisha yetu ya baadaye. Hili ndo kundi ndio watakaopeleka vizazi vyetu mbele zaidi na kuvumbua mbinu mpya za kufanya maisha ya mwanadamu kuwa endelevu na yenye starehe zaidi. Lakini kama wazazi na walezi, lazma tuzungumzie kuhusu siku zijazo; tuwe na umakini mkubwa katika suala la usalama wa watoto wetu haswa katika ulimwengu wa leo.

Je, tunaweza kusema kwa ujasiri kwamba watoto wetu wako salama kwa asilimia mia moja leo? Je kuna mzazi ambaye anaweza kusema kwa hakika kuwa mtoto wake yupo salama shuleni kwa asilimia mia moja? Je, mtu yeyote anaweza kusema watu wanaowazunguka watoto wetu ni watu wenye nia njema linapokuja suala la usalama wa watoto wetu? Majibu ya wazazi na walezi wengi ni Hapana, hakuna mzazi ambaye ana uhakika wa mtoto wake tena katika zama hizi.​
1716886557079.png

Picha kwa hisani ya Variety.
Binafsi ukiniuliza swali hili jibu langu ni hapana, kwa sababu, Takriban kila siku, tunapata magazeti, tovuti na vituo vya televisheni vikipiga yowe na visa vipya vya unyanyasaji pamoja na ukatili dhidi ya watoto. Mauaji, unyanyasaji wa kimwili, unyanyasaji wa kifikra, na mengine mengi. Mtoto fulani amelawitiwa na ndugu yake akiwa nyumbani, mwingine anatekwa nyara na kushikiliwa kwa ajili ya fidia kubwa kutoka kwa wazazi na walezi wake. Dunia si mahali salama tena kwa watoto wetu wadogo, amini usiamini.

Jambo lingine la kuangaliwa hapa ni kuongezeka kwa hii mtandao na athari inayopatikana kwa akili za vijana, wengi tunaelewa kuwa ujio wa mitandao haswa hii ya kijamii. Sote tumesikia kuhusu matukio kadhaa ya watoto wetu wa sekondari kuwa na akaunti katika mitandao ya Facebook na mingine na kujamiana na watu ambao kiuhalisia sio watu wema. Hivyo basi, huu ndio wakati wetu kama jamii kuingilia kati na kutafuta njia za kuwaweka vijana salama. Ni lazima tuhakikishe kwamba watoto wetu wako salama kutoka kwa macho ya wawindaji na waharibifu.​
1716886701853.png

Picha kwa hisani ya Getty Images.

Imeripotiwa kuwa takriban watoto milioni 40 duniani kote wanafanyiwa ukatili wa aina mbalimbali kila mwaka, ambapo kati yao 25-50% ya watoto hunyanyaswa kimwili, huku 10% hunyanyaswa kifikra. Ripoti hiyo inaongeza kuwa takriban wasichana milioni 3 wanakutana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kila mwaka, wavulana zaidi ya milioni 2 nao hukutana na uaktili haswa wa kingono zaidi, ingawa mashirika mengi yamekuwa wakiwatazama zaidi wasichana kuliko wavulana.

Tukichanganua data zaidi, tutagundua kwamba kizazi cha vijana kinakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia kwa kiasi kikubwa kwani angalau msichana mmoja kati ya watatu ananyanyaswa kingono kabla ya umri wa miaka 17 huku kwa wavulana idadi hiyo ikifikia mmoja kati ya wanne. Ukweli mwingine wa kutisha unaopaswa kuzingatiwa hapa ni kwamba katika asilimia 90 ya visa vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto mkosaji ni mtu anayejulikana kwa mtoto au familia; yaani ni mtu wa Karibu haswa ndugu au majirani.​
1716886949578.png

Picha kwa hisani ya CNN.

Hivyo, nini cha kufanya? Jinsi ya kuhakikisha kuwa watoto wetu wako salama? Kuongezeka kwa idadi ya uhalifu sasa kumesababisha wazazi wengi kuwaficha watoto wao kila siku, na kuwa na hofu juu ya ustawi wao kila mahali. Lakini je, hili ndilo suluhisho kweli? Tukubali, kuwa kwa mantiki ya kawaida haiwezekani kuwa na mtoto wako masaa ishirini na nne siku saba za wiki. Tunachohitaji kufanya ni kuchanganua hali hiyo kwa uangalifu na kubuni njia tunazoweza kuwaacha watoto wetu wawe salama, huku tukidumisha hali isiyo na mkazo kwao na sisi wenyewe pia.
Hapa kuna njia chache tunazoweza kujaribu na kuweka njia kuelekea mazingira salama kwa watoto wetu:​
  • Wajulishe kuhusu mguso mzuri na mguso mbaya, na waeleze tofauti kati ya mema na mabaya. Tena kwa uwazi pasipo kuwaficha chochote, mficha magonjwa kifo…….. Hapa ndo kazi kubwa ya mzazi na mlezi inaonekana. Watoto wapate elimu ya kutosha kuhusu usalama wao haswa wakiwa peke yao. Baba na Mama wakiwa hawapo nyumbani je ni vitu gani hatakiwi kuvifanya kabsa. Kuna ripoti kadhaa za mabinti waliobakwa na kurudi nyumbani kujificha bila kufahamu kuwa anaweza kwenda kituo cha afya moja kwa moja au kwenda kituo cha polisi kupata msaada. Tuwafundishe watoto wetu kujidhahari na makundi ya watu haswa wale ambao mtoto wako hutumia muda mwingi pamoja nao, mfano, shuleni, viwanja vya michezo pamoja na sehemu ambazo kwa kawaida mtoto anaweza kujikuta yupo peke yake. Hapo hata taaluma ya sel defence inahitajika kwa upana wake.​
  • Iwapo mtoto analalamika kuhusu mtu fulani au jambo fulai na kuliona kama ni tatizo kwake, daima baki wazi na ruhusu miango ya kumsikiliza kwa makini na jaribu kuelewa wasiwasi wake badala ya kumkasirisha mtoto. Tumia muda mwingi katika kumsikiliza zaidi na kumsoma mwili wake. Zungumza na watoto wako mara kwa mara kuhusu shughuli zao za mchana, siku zao zimeendaje, je wamekutana na changamoto zipi na wameonaje Maisha yao siku nzima. Achana na ubusy linapokuja suala la kuzungumza na kujamiana na watoto wako.​
  • Dumisha uhusiano wa wazi na watoto wako ili waweze kujisikia huru katika kukueleza matatizo yao na wasiwe na wasiwasi wa kudhihakiwa. Kuna baadhi ya wataalamu wa maelzi wameeleza kuwa usiwe rafiki kwa mtoto wako ila kuna nyakati tengeneza mazingira bora ya mtoto wako kukuelezea mambo yake kwa uwazi. Wafanye watoto wako wakuamini. Wafanye waamini kuwa uko kwa ajili yao kila wakati, na kwamba wanaweza kukutegemea, haijalishi ni nini, au kitatokea nini, wafanye wajisikie huru wakiwa na wewe.​
1716887072546.png

Picha kwa hisani ya CNN.
Kama wazazi na walezi tuna jukumu kubwa sana la kuwatazama watoto wetu, tuangalie hatua za jumla za usalama zinazochukuliwa shuleni. Shule ni mahali ambapo wazazi huwapeleka watoto wao wakiwa na mawazo akilini kwamba mtoto wao atakuwa akijifunza kwa uwezo wake wote kwa saa chache zijazo na atakuwa salama ndani ya mipaka ya shule. Wanaweka imani yao kwa walimu na mamlaka ya shule ili kuhakikisha usalama wa mtoto wao. Rai kwa serikali, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu tengenezeni mikakati mizuri kwa ajili ya watoto walipo ndani ya Tanzania, tusifumbe macho kwa kigezo cha kwamba sio watoto wetu. Tanzania ni moja na sisi ni wamoja.​

Tanzania Tuitakayo: Watoto wetu Hazina Yetu.
 
Upvote 0
Iwapo mtoto analalamika kuhusu mtu fulani au jambo fulai na kuliona kama ni tatizo kwake, daima baki wazi na ruhusu miango ya kumsikiliza kwa makini na jaribu kuelewa wasiwasi wake badala ya kumkasirisha mtoto.
Mawasiliano, muhimu sure.
 
Back
Top Bottom