SoC04 Tanzania Tuitakayo yamejikita katika nyanja za Elimu, Afya, Teknolojia, Uchumi, Mazingira na Miundombinu

SoC04 Tanzania Tuitakayo yamejikita katika nyanja za Elimu, Afya, Teknolojia, Uchumi, Mazingira na Miundombinu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Meekboy

New Member
Joined
Jun 14, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Maono yangu kuhusu TANZANIA TUITAKAYO yamejikita katika nyanja 6 ambazo ni elimu, afya, Teknolojia, uchumi, mazingira na miundombinu.

1. ELIMU.
-serikali kuendeleza mchakato wa elimu ya watu wazima (MEMKWA) hasa vijijini.
-serikali kutoa vifaa shuleni vya TEHAMA vya kufundishia na kujifunzia mfano kompyuta za mezani, vishikwambi na laptop.
-serikali kuongeza ajira kwa kada ya ualimu wenye uwezo wa kufundisha kuendana na maendeleo ya TEHAMA.
-Mikopo inayotolewa kwenye elimu ya juu iweze kutolewa kwa wote watakao omba na kwa asilimia zinazofanana , ili kila mtanzania aweze kuendelea kusoma kwa wakati.
-Serikali kujenga nyumba za walimu,ili waweze kufundisha Hadi mida wa ziada ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
-serikali kuboresha vyanzo vya maji vinavyotumiwa na wanafunzi kwa kuwatengenezea mifumo mizuri ya maji, mfano visima na Bomba.
-kuwapa motisha walimu wanaofanya vizuri katika ufundishaji na ujifunzaji.
-serikali iweze kuongeza mishahara ya walimu kwasababu inaonekana Ni kada yenye mishahara midogo kuliko zote.

2. AFYA
-kuajili wahudumu wa afya ambao no Bora na wapo tayari kulitumikia taifa kwa uadilifu
-kutoa vifaa Bora vya afya katika kila zahanati na hospital,ili watu pia wa vijijini waweze kupata huduma za afya zilizobora siyo mpaka waende mjini endapo iyo huduma itakosekana kwenye hiyo zahanati.

3. TEKNOLOJIA
-serikali itengeneze mkakati mzuri wa kudhibiti wizi wa mtandaoni.
-kuwapa watu elimu kuhusu matumizi Sahihi ya mitandao ,ili watu nao waweze kunufaika na mitandao na siyo kupoyeza muda wakiwa mitandaoni.
-kudhibiti watu wanaotukana matusi mitandaoni.

4. UCHUMI
-kuhimiza wananchi kutoa Kodi Hadi vijijini.
-kuhimiza wananchi kufungua akaunti Benji.
-serikali iweze kuzuia uvuvi haramu hasa katika mito na kwenye maziwa.
-serikali kujenga viwanda sehemu ambazo ni karibu na malighafi zinapozalishwa au kulimwa , mfano kyela-mbeya Kuna mazao mengi lakini Hakuna kiwanda ata kimoja.

5. MAZINGIRA
-serikali kuhimiza matumizi ya nishati salama kwa watanzania wote, mfano matumizi ya Sola na majiko ya gesi, umeme.
-upandaji wa miti katika mazingira.
-uwepo wa sehemu za kuhifadhia taka hasa vijijini Hakuna huduma hiyo.
-kuendelea kuwazuia wananchi kujenga na kulima kando na vyanzo vya maji.
-kuzuia utiririshaji wa kemikali kutoka viwandani kwenda kwenye vyanzo vya maji.

6. MIUNDOMBINU.
-kuongeza viwanja vya ndege viwepo kila mkoa ili kila mwanamchi aweze kunufaika na usafiri huo.
-kuboresha barabara za vijijini ambapo zinawatesa Sana wananchi kupitika kipindi Cha masika.
-kutengeneza barabara za wapita kwa mguu wanaokatisha barabara zinazopita juu sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa Vyombo vya usafiri ili kupunguza ajari.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom