SoC04 Tanzania tuitakayo yenye huduma bora za mikopo ya Elimu ya juu, na kuweka utaratibu mzuri wa marejesho Kwa wote hata kwa ambao hawapo sekta rasmi

SoC04 Tanzania tuitakayo yenye huduma bora za mikopo ya Elimu ya juu, na kuweka utaratibu mzuri wa marejesho Kwa wote hata kwa ambao hawapo sekta rasmi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
346
Reaction score
522
UTANGULIZI.

👉Lengo kuu la HESLB ni kutoa msaada wa kifedha kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kuhakikisha kuwa wanaweza kukamilisha masomo yao bila kikwazo cha kifedha. Dhamira yake ni kuongeza upatikanaji wa elimu ya juu na kusaidia kuboresha ubora wa elimu nchini Tanzania.

👉Baada ya kumaliza masomo, wanufaika wa mkopo wanatakiwa kuanza kurejesha mikopo yao kwa mujibu wa makubaliano.
HESLB inafuatilia urejeshaji wa mikopo kwa kutumia mifumo ya kisasa ili kuhakikisha kuwa mikopo inarejeshwa kwa wakati na hivyo kuwezesha wanafunzi wengine kufaidika ambayo nyakati nyingine haiwasomi wanufaika na kuwabaini ili warejeshe fedha zao.

CHANGAMOTO ZINAZOKABILI BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU NA MBINU MBADALA ZA KUITATUA.
01. Changamoto!
👉
Baadhi ya changamoto ni pamoja na wanufaika kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, upatikanaji wa fedha za kutosha kugharamia idadi kubwa ya waombaji, na ufuatiliaji wa wanufaika walioko nje ya nchi. Wanufaika wengi hawarejeshi mikopo kwa wakati au hawarejeshi kabisa, hali inayosababisha upungufu wa fedha kwa ajili ya wanafunzi wapya.

👉Wanafunzi wengi hulalamikia ucheleweshaji wa kupokea fedha zao za mikopo, jambo linaloathiri masomo yao na hali ya maisha. Je tujiulize kama mnamcheleweshea pesa Yake inawezekana vipi yeye akawalipa Kwa wakati????. Serikali iongeze BAJETI YA FUNGU HILI

👉Fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya mikopo hazitoshi kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote wanaoomba mikopo, wengineo hukosa mikopo na hivyo kuathiri masomo Yao.
👉Kuna changamoto katika usimamizi wa mifumo ya utoaji mikopo na ufuatiliaji wa wanufaika walioko nje ya nchi au wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

02. Namna ya kutatua changamoto zinazokabili HESLB.
👉
Kutumia mifumo ya kidijitali na benki ili kuhakikisha fedha zinafika kwa wanafunzi kwa wakati na kupunguza ucheleweshaji. Mfumo wa malipo wa moja kwa moja kutoka benki kwenda kwa mwanafunzi unaweza kusaidia kuondoa ucheleweshaji.

👉Kuimarisha sheria na kanuni za urejeshaji wa mikopo, ikiwa ni pamoja na kutoza riba na adhabu kwa wale wanaoshindwa kulipa kwa wakati. Pia Kufanya kazi kwa karibu na waajiri ili kuhakikisha mikopo inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mishahara ya wanufaika, hata Kwa wale walioko kwenye sekta isiyo rasmi.
👉Kutumia teknolojia ya kuunganisha na kufungamanisha mifumo yote ndani ya nchi mfano ,NIDA Namba,LITA-usajili wa vizazi na vifo, LATRA- usafiri na usafirishaji,Huduma za kipesa bank na mitandao ya simu,Brela , TRA - TIN Namba,Huduma za vidole finger prints kulink generation husika BIMA ,leseni za udereva na mikataba mbalimbali,yote ni kwa ajili ya kufuatilia mikopo na kuhakikisha usalama wa taarifa za wanafunzi na urejeshaji wa mikopo. Kuanzisha mfumo wa usimamizi wa data wa kisasa utakaowezesha ufuatiliaji wa wanufaika popote walipo duniani.
👉Kutoa mafunzo na programu za kujiajiri na kuajirika kwa wanufaika wa mikopo ili waweze kujiajiri na kuajiliwa hivyo kuwa na uwezo wa kurejesha mikopo yao kwa wakati.
👉Kuweka utaratibu wa ufuatiliaji wa wanufaika walioko nje ya nchi kwa kushirikiana na balozi za Tanzania nje ya nchi na kuanzisha ofisi maalumu za HESLB kwenye maeneo yenye watanzania wengi.
👉Kuendeleza uchumi wa nchi ili kutoa elimu bure Kwa ngazi zote,inahitaji mipango thabiti na utekelezaji wa mikakati mbalimbali,hivyo tutaachana na hiki kinachoitwa bodi ya mikopo.
MWISHO.

👉Kwa ujumla, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza elimu na maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania. Kupitia mikopo, vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu hupata wanafunzi wengi zaidi, na hivyo kupata fedha zaidi za uendeshaji na kuboresha huduma zao.
👉Mikopo inavyowezesha upatikanaji wa elimu ya juu, inaongeza ushindani na hivyo kuchochea taasisi za elimu ya juu kuboresha ubora wa elimu wanayotoa.
 
Upvote 6
Back
Top Bottom