Well said, tukiimarisha hata vyanzo vilivyopo tu...tunaweza kupata umeme wa uhakika? je tumeshatumia vizuri tulichonacho? nafikiri ili uanze kufikiri nuclear inatakiwa kwanza uwe na mahitaji makubwa kutokana na development progress uliyo nayo..sisi tuna viwanda tumefikia hapao?
Tumeimarisha umeme kutumiavyanzo vya maji, majibu yake ni Mgao bara na Zanzibar. Tumetumia Dizeli, shukurani yake ni mgao. Sasa wengine wanazungumzia Makataupepo, sijui tutafika wapi. Na wakati huo huo tunazungumzia Gesi, sinamatumaini. Kuna tetesi za umeme wa jua na ule wa kutumia mawimbi ya bahari.
Hebu tuanze na makataupepo: Ndugu zanguni sipendi kuwakatisha tamaa, lakini kwanza hakuna nchi hata moja duniani, hususan hizo zilizoendelea ambazo zinatumia angalau 15% ya umeme wake toka hayo makataupepo. Hii hutumika kama kijazilizo tu na si kama muhimili tegemezi wa umeme.
Umeme wa Gesi: Rusia ndio inaongoza kwa utoaji wa Gesi duniani lakini umeme wa Gesi inayotumia haizidi hata 5% ya umeme wa nchi. Ninawasiwasi kama wanaotuambia hivyo wanania ya kutusaidia au ndio ile mbinu ya "Buy time".
Umeme wa jua: Huu ni umeme dhaifu sana, sana sana unafaa kwa matumizi binafsi, kama taa, TV, Jokofu n.k. Isitoshe bado unategemea kudra za Mwenyeezi Mungu na ni ghali. Kifupi wazo hili si practicle.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba njia hizo zote nilizozitaja hapo juu pamoja na nyingine uzijuazo ama ni ghali ukilinganisha na ule wa Nuclaer au sio practicle kutokana na uwezo wake mdogo kwa matumizi ya viwanda. Na ndio maana hata wale wagunduzi wake hawautumii kutokana na gaharama zake kuwa kubwa.
Mnakumbuka tulipojenga kidatu, mayowe ya wanasiasa yalikuwa makubwa sana. Huku wakidai kuwa umeme tuliokuwa tunautumia ni 30% tu, na leo hii tunaambiwa tatizo jingine kabisa. Lazima tuelewe kuwa maendeleo ya uchumi hayaletwi kwa execuses.
Viwanda vya kutumia umeme huo tunavyo, kama kuna mwenye hofu na maedeleo ya viwanda vyetu. Tena tukiwa na umeme wa kueleweka, utaona jinsi wawekezaji watavyomiminika. Na ni kwa sababu hizo ndio maana wawekezaji wamewekeza zaidi katika nchi kama China, Rusia, India n.k.
Ukiprocess mafuta ya Nuclear mpaka 5%, unapata umeme na si hatari sana kama ukiprocess mafuta hayo kwa kiwango cha kupata Bomu. Kwa hiyo katika level tuliyonayo tunaweza kabisa kujikita katika usalama wake.