Tanzania Tujiandae na Utawala wa Joe Biden (Democrat)

Status
Not open for further replies.
Hii inferiority complex tutakuwa nayo mpaka lini? Inaonekana hatujataka kujitawala! Au ndiyo maana Lissu anawachumbia wakoloni warudi?
Kujitawala kupi kaka wakati hata zoezi dogo tu la kuchaguana wenyewe kwa wenyewe kupata viongozi wetu kwa kutumia katiba na sheria za nchi hatuwezi..aibu kubwa sana hii kwa Taifa.
 
Wewe mnywa balimi wa tandale ndio ujue dunia inaelekea wapi. Wewe endelelea kukariri tu conspiracies zisizo na mbele wala nyuma
Dunia iko kiganjani Yoda,sio lazima uwe Marekani kujua yanayoendelea huko,amka.
 
Kujitawala kupi kaka wakati hata zoezi dogo tu la kuchaguana wenyewe kwa wenyewe kupata viongozi wetu kwa kutumia katiba na sheria za nchi hatuwezi..aibu kubwa sana hii kwa Taifa.

Kwa sababu ya kushindwa uchaguzi, hata Trump na supporters wake wanaamini Marekani haiwezi kufanya uchaguzi kwa kufuata katiba na sheria zake. Kwa ujumla, popote walipo duniani, narcissists hawana utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi yanayoonesha kuwa wameshindwa. Hata kama malaika wa Mungu watashuka kuratibu na kuendesha huo uchaguzi, narcissists watapinga matokeo yoyote yanayoonesha wameshindwa. They strongly believe they’re too good to lose an election to anyone!
 
You mean kuletewa Balozi shoga, au kuandamwa makanikia yetu?
 
Wewe ndiye unayeota kwa ktoa tuhuma zisizo na uthibitisho wa kisheria. Endelea kuota kwamba siku moja wewe pamoja na genge lenu kuongoza nchi ya Tanzania labda uhamie upande wa pili.
 

Ukweli kuhusu Trump wa Republic party na Joe Biden wa Democratic nchini Marekani tunapolinganisha na Tanzania, yaani CCM ya Jiwe na CHADEMA ya Mbowe ni hivi:
  • Donald Trump-Republican ni sawa na Magufuli- CCM.
  • Joe Biden- Democratic ni sawa na Aikael Mbowe- CHADEMA.
Kama Tundu Lissu wa CHADEMA angelishinda uchaguzi Mkuu wa Oktoba,2020 basi Magufuli angelica ya vituko kama vya Trump.....believe it or not.
Kuna mfanano wa karibu sana kitabia, kihaiba na kimatamshi baina ta hawa watu 2 yaani Trump na Jiwe....!!!
Majitu kama haya aghalabu hayatakiwa kabisa kushika madaraka hasa ngazi za Urais.....!!!!!
 

You must be kidding. Biden huwezi kumfananisha na watu ambao kamwe hawajawahi kukubali matokeo yoyote ya uchaguzi yanayoonesha kuwa wameshindwa! Kama alivyo Trump, wao hung’ang’ana na unsubstantiated claims kuwa wamedhulumiwa ushindi wao. Biden has never refused to concede an election loss in his political life!

Watu wanaofanana zaidi na Donald Trump ni Tundu Lissu na Maalim Seif. Bila kudhibitiwa hawa narcissists wangekuwa wameshaingiza blind followers wao kibabe katika Ikulu zetu.
 
Hii inferiority complex tutakuwa nayo mpaka lini? Inaonekana hatujataka kujitawala! Au ndiyo maana Lissu anawachumbia wakoloni warudi?
Yaani acha tu. Africa safari yetu ngumu sana. Hata watumwa waliuzwa na machief wetu kabisaaa
 
Haya mambo ya kulilia nchi nyingine ije kukusaidia ndo udhaifu wa akili. Hakuna mfano wowote ktk dunia hii ambapo US imesaidia maendeleo na wakaendelea. Watu kama wewe, nikiuliza unamtaka Biden kwa lengo gani, nadhani unataka aje akusaidie kumtia adhabu Magufuli, which is filing for bankruptsy!
 
Hii inferiority complex tutakuwa nayo mpaka lini? Inaonekana hatujataka kujitawala! Au ndiyo maana Lissu anawachumbia wakoloni warudi?
Ni mapungufu ya mtu ambaye ana nafasi ya kugusa keyboard. Kabla ya mitandao watu kama huyu walikuwa hawasikiki, tatizo ni hali ya sasa ambayo hata bwenge anaweza itisha mkutano/press conference.
 
Wewe ndiye unayeota kwa ktoa tuhuma zisizo na uthibitisho wa kisheria. Endelea kuota kwamba siku moja wewe pamoja na genge lenu kuongoza nchi ya Tanzania labda uhamie upande wa pili.
Kilichotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kinafahamika.

Kilichotokea uchaguzi mkuu 2020 pia kinafahamika. Aidha, yaliyotokea katika chaguzi za marudio pia yanafahamika.

Waliyofanya akina Mnyeti na kudukuliwa wakipanga njama za kupora madiwani na wabunge wa CHADEMA, yanafahamika.

Kwa kifupi, mbinu za kuengua wagombea wa upinzani, kuwateka, kuwakamata ovyo, kuwatisha, ziko documented.

Rais Magufuli alipiga marufuku shughuli halali za upinzani, kinyume na katiba, kinyume na sheria ya vyama vingi.

Hata katibu mkuu Bashiru Ali alitamka wazi kwamba ccm ipo tayari kutumia dola ili kubaki madarakani, badala ya kutumia njia halali za uchaguzi huru.

Kama hayo yote huyaoni, basi huna hoja
 
Uliambiwa uingie barabarani ukagwaya sasa acha kutupotezea muda wetu sisi tuko busy na kazi uchaguzi umeshaisha mpaka 2025 tena.
Kama Magufuli aliyaogopa hayo maandamano kiasi cha kuwakamata viongozi wa CHADEMA usiku na kuwaficha, kama maaskari kibao walisambazwa mitaani kukamata na kuwatesa yeyote atakayejitokeza, ni wazi kwamba Serikali ya Magufuli ilikiuka sheria ya vyama vingi inayoruhusu maandanmano kupinga serikali. Hatua ya kwenda barabarani ilikuwa hatua ya kidemokrasia, kuonesha kutokubaliana na mambo kadhaa katika uchaguzi.

Magufuli alihofia kwamba kama angeacha watu waandamane, zile nyomi za Lissu zingeibuka na kuhamia mtaani, nchi isingetawalika.

Lakini mapambano yanaendelea, hilo ndio la msingi.
 
Hii dhana ya kupenda kujiona unatawaliwa muda wooote imekukaa Kichwani sana. Huko Marekani mbona Waandamanaji wameuwawa nje ya Jengo la BUNGE mnaojifanya Wanaharakati mmekaaa kimiaaaaaa pimbi nyie.
Kumbe walikuwa ni waandamanaji siyo wahasi?
 
Hii inferiority complex tutakuwa nayo mpaka lini? Inaonekana hatujataka kujitawala! Au ndiyo maana Lissu anawachumbia wakoloni warudi?
Unajitawala kwa uchumi upi ulionao
wewe,ombaomba Ana uwezo gani wa kujitawala? Sisi ni makoloni hadi mwisho wa dunia.
Uchumi wetu tunauza Ni nini nje? Akiba yetu ya dola kufanya manunuzi inatosha miezi 5 tu, tuna jeuri gani sisi.Mafuta ya petrol jeuri yetu tuna uwezo wa kuagiza mafuta ya siku 21 tu
Acha siasa kujifarijie wakat ww si lolote si chochote.Tukifungiwa MISAADA miezi mitano hapa tutakufa km nzige waliopigwa sumu.
Bajeti yetu zaidi ya 50% tunategemea MISAADA na Mikopo ili tuweze kuishi.
Sisi ni maskini tunaosubiri kifo cha asili.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…