Tanzania Tujifunze: Russia inafadhili vikundi vya mazingira, vinavyopiga kelele Ulaya na Marekani kuzuia uzalishaji nishati

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Kuna vikundi vitatu vikubwa nchi za Ulaya na Marekani, ambavyo vimekuwa vikibweka sana kuzuia miradi mikubwa ya uzalishaji nishati mbadala kwa Ulaya na Marekani ambavyo vimesababisha uzalishaji wa nishati kwa nchi hizo upungue sana, hadi kuifanya Ulaya sasa kutegemea Nishati ya Russia kwa asilimia arobaini.

Imefahamika kwamba vikundi hivyo vikubwa vinavyohusisha League of Conservation Voters, the Natural Resources Defense Council, na Sierra Club vimekuwa vikifadhiliwa na Russia ili kuhakikisha nchi za Ulaya na Marekani zinaachana na uzalishaji wa nishati na kuwafanya wawe tegemezi wa nishati kwa Russia.

Tanzania tunapaswa kujifunza hili, hususani kwenye sekta ya Utalii. Kila mradi tunaotaka kuanzisha, tunapigiwa kelele na vikundi vya mazingira fulani vilivyomo ndani na nchi jirani ya kaskazini vikijifanya vinathamini zaidi na mazingira. Ukiangalia kwa undani vikundi hivyo vina connection na watu au nchi wasiopenda tutoke kwenye utalii.

Tusisahau ule mpango wetu wa kutaka kujenga barabara ya lami kupitia hifadhi ya Serengeti ambapo ulipigiwa kelele na vikundi kama hivi na pia kuzuiwa na Mahakama ya Afrika Mashariki.

Tanzania tuamke usingizini.

Pascal Mayalla Yericko Nyerere

 
Umejikoroga sana.

Hivi kwa maneno machache unajaribu kuzungumzia nini?
 
Ni Pale unapomuwekea sumu mtoto wa kambo ale afe, chakula icho icho akaja kukila mwanao[emoji2]
 
Naona vile vikwazo vya kiuchumi vimewakwaza Hadi wao wenyewe walioviweka[emoji2]
 
Nishati MBADALA ni kama zipi?
 
Tanzania imekazana na kuimarisha dola tu na siyo pande nyingine...wenzetu Kenya tu wanajitahidi Wana vijitu vyao vimepachikwa kwenye taasisi mbalimbali lengo ni kupigia chapuo Mambo yanayowaletea faida kiuchumi tu, kazi yao kutetea faida zao tu,sisi tumekazana na maslahi ya kidola...
 
Sisi ni wajinga.
 
Sisi tunafikiri kuwa mataifa makubwa ni wapuuzi kuweka watu wao kwenye taasisi za kimataifa au mashirika binafsi,utakuta wamejaa humo wamarekani,waingereza nk lengo ni kutetea nchi kwa mfumo wa kutoa agenda kwenye mikutano na kujadiliwa,sisi tunakubali na kupitisha tu kumbe kuja kushtuka tayari majamaa wamependelea upande wao zaidi tukidhani eti wameotuokoa...
 
Tusiweke nguvu nyingi sana duniani, tunapita tu hapa, wote hao, Putin na Biden watakufa tu siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…