Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 414
Baada ya Medali ya Kwanza ya Fedha kutoka Kwa Mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliyoipata kwenye Mbio Ndefu Marathon Tarehe 30/07/2022, Leo Jioni Tanzania imehitimisha ngwe ya ndondi kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa kupata medali mbili za shaba baada ya bondia wake wa pili Kassim Selemani Mbundwike kupoteza kwa pointi pambano lake la nusu fainali dhidi bondia wa Msumbiji jijini Birmingham, Uingereza.
Hivyo Tuna Medali ya Fedha Moja (Marathon) na Mbili za Shaba zote Ndondi (Boxing).
Wanariadha Wetu wa Mita 5000, Josephat Joshua Gisemo na Faraja Lazaro Damasi wamehitimisha Kwa kushika nafasi za 15 na 16 kati ya wanariadha 20, huku Mganda akichukua Medali ya Dhahabu na wakenya wakichukua medali za fedha na Shaba.
Nchi zinazoongoza Hadi Sasa
1. Australia -medali 155
2. Uingereza- Medali 148
3. Canada - Medali 84