Bwana Yesu Asifiwe na Asalaama Aleykhum,
Jina IDARA YA USALAMA WA TAIFA tuliliiga kutoka Romania ambao shirika lao liliitwa DEPARTMENT OF STATE SECURITY (The Securitate). Tanzania, Romania, Cuba, Yugoslavia na Ujerumani Mashariki zilikuwa na ukaribu wa hali ya juu mno kisiasa na kiusalama.
Baadhi ya wakurugenzi wa ujasusi wa Tanzania walipata mafunzo yao Romania, Cuba, Yugoslavia, Eastern Germany na Czechslovakia . Hivyo hata mifumo ya kijasusi ya nchi hizi inafanana mno, pamoja na falsafa zake za kuendesha shughuli za kijasusi.
Mataifa yote haya yaliiga mfumo wa Ujasusi kutoka Urusi ya Kisovieti (USSR), ambapo idara za usalama zote zilikuwa ni sehemu za vyama tawala zinazohakikisha falsafa ya ukomunisti na ujamaa inadumu kwenye nchi hizo kwa gharama yoyote ikiwa kuwaondoa wote ambao mawazo yao yatakwenda kinyume na matakwa ya chama tawala.
Kiufupi, Dikteta wa Romania Nicolae Ceausescu alikuwa rafiki wa karibu mno na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Inasemekana hata miaka ya 1980's kabla hajauwawa kikatili na jeshi la Romania, Mwalimu Nyerere alimshauri bwana Nicolae Ceausescu kuachia madaraka, lakini akapuuza ushauri huo.
Kuna mengi yanaendelea Tanzania, ambayo nadhani watawala na vyombo vyao vya usalama inabidi wajifunze kutoka kwa nchi maswahiba (Sister States) kiusalama lama Cuba, Yugoslavia, Eastern Germany, Czechslovakia na hasahasa Romania.
Idara ya usalama wa taifa ya Romania (The Securitate), ilikuwa ina nguvu iliyopitiliza. Ilifika kipindi walikuwa na majasusi wasiopungua 11,000 na wapeleka taarifa (Collaborators and Informants) wasiopungua laki tano. Kiufupi, mtu alikuwa hawezi kufanya lolote lile bila chama tawala kufahamu.
Miaka ya 1980's baada ya ujamaa kuanza kudorora duniani, ilibidi serikali ya Romania iunde task-forces ambazo zilikuwa na lengo la kuhakikisha Raisi Nicolae Ceausescu anabaki madarakani kwa gharama yoyote ile. Walianza kuwatisha wasomi, kuwahonga watu fedha, kuwaharibia wasomi ajira na elimu bila wao kujua kwamba wanaharibiwa, kudhibiti vyombo vya habari na kuua mtu kwasasabu ndogo na zisizo za msingi.
Mwisho wa siku kama ilivyotokea Czechslovakia na Eastern Germany, Romania serikali yake ilianguka na kusababisha madhara makubwa kwa Raisi Nicolae Ceausescu na familia yake nzima. Jeshi alililitegemea kwamba lingemlinda ndilo lilimgeuka na kumkamata.
LAKINI: Jambo baya zaidi ni kwamba baada ya mapinduzi, taarifa za kijasusi kuhusu Idara yao ya usalama wa taifa (The Securitate) zikaanza kutoka nje kama ilivyokuwa kune Eastern Germany. Raia wakaanza kuwafahamu wabaya wao wengine wakishangaa kwamba waliowasaliti walikuwa ni ndugu zao wa karibu. Majina ya State Agents na Informants yakaanza kuwekwa nje-nje, na vikaanza visasi na kuumizana kusiko na sababu.
Eastern Germany, shirika lao la kijasusi The Stasi ndiyo lilikutwa limefanya mambo ya ajabu na kikatili kupitiliza, ambapo katika kila wajerumani 10 lazima kulikuwa na jasusi 1. Ila hizi nguvu zote, bado serikali ikaanguka na vikaanza visasi.
NAAMINI: TISS ni idara imara, lakini haizifikii hizi idara za kijasusi za Eastern Bloc ambazo ziliasisiwa na wanajeshi waliopambana vita za dunia. Mataifa kama Yugoslavia na Eastern Germany, walikuwa na fedha pamoja na teknolojia ya juu kabisa kwenye vyombo vyao vya usalama kuliko hata TISS lakini hawakuvuka mwaka 1990.
Ifika mahali sisi kama taifa masikini tunaotaka kuvuka hapa tulipo ni lazima tujifunze. TISS kuajiri watu wasiokuwa na weledi, wenye tamaa ya fedha na madaraka, na wasioweza kumwambia Raisi ukweli kwamba anakosea ni tatizo kubwa kwa nchi.
KINACHOENDELEA NCHINI: Kama TISS mnasingiziwa basi MUNGU atafunua ukweli, lakini kama mnahusika na kuwaua ndugu zenu mnaoishi nao mtaani kwenu, mnaenda nao kanisani, msikitini na mnafanya nao biashara kisa mishahara, posho na vyeo vya kisiasa, mtalifikisha hili taifa kubaya sana.
Haiwezekani mambo kama haya yafanyike nchini, halafu taifa lisigawanyike hata siku moja. Mimi kama mwanahistoria na msomi wa siasa, nimesoma historia za siasa za dunia hii hasahasa, historia za nchi za kijamaa na kikomunisti kwa miaka mingi sana na niseme tu kwamba, maanguko ya mataifa yote ya kikomunisti yanafanana sana. Kuanzia: USSR, Eastern Germany, Yugoslavia, Romania, Poland n.k
HUWA INAANZA HIVI:
Watalawa wanakuwa wote wanauwa watu sana.
Baadaye wanaanza kuhujumiana wenyewe kwa wenyewe kisa siasa na maslahi.
Halafu yanazaliwa makundi hasimu ndani ya chama na vyombo vya dola yakishindana.
Kundi moja linachukua madaraka na kuanza kuliumiza kundi jingine kwa kutumia dola.
Kundi linaloumizwa linaanza kulipiza dhidi ya kundi tawala, hata kutafuta marafiki wa nje ya nchi. (Crossing the Rubicon)
Makundi mawili ya watawala yanavyoanza kupambana kutumia hovyo rasilimali za nchi wananchi wanageuka Collateral Damage. (A Point of No Return)
Mwishowe makundi haya yanaumizana na wananchi wanajikuta wana nguvu kwasababu ili kundi moja lipate uhalali (Legitimacy) ni lazima lijifunganishe na wananchi. (Civil Disobedience)
Serikali inaanguka na hata kupelekea nchi kuingia kwenye machafuko. (Anarchy)
NB 1: Tanzania tumefikia hatua ya TANO (5) kwenye mlolongo huu, tukicheza vibaya zaidi tunaweza jikuta tuko hatua ya SITA (6). Huu mlolongo nimeuona kwenye mtifuano wa madaraka baina ya:
The Roman Triumvirate (Julius Ceaser, Marcus Lucinius Crasus), ambapo marafiki waliotawala dola la Rumi kwa pamoja wakageuka mahasimu wabaya mno na mwishowe kuingiza Rumi kwenye CIVIL WAR.
The Soviet Triumvirate (Vladmir Lenin, Joseph Stalin na Leon Trotsky), ambapo napo ilipelekea vifo vya maelfu ya watu ndani ya nchi kisa watawala wanavutana na kugombania madaraka.
NB 2: Rumi na Urusi ziliweza kujirudi kwasababu ni mataifa makongwe yalikuwa na historia za kujitawala kwa zaidi ya miaka zaidi ya 500. Japo mbali na hayo serikali za Rumi na Urusi zote zilianguka na vikazaliwa vitu vingine.
FOOD FOR THOUGHT: Ninyi watawala wa CCM + TISS + TPDF + PT, siyo bora kuliko wenzenu wa hapo jirani Kenya ambapo walidharirishwa mbele ya dunia kwa kuburuzwa kizimbani kwenye mahakama za kimataifa (ICC), jambo la aibu kabisa kwa nchi hata kama walishinda.
Kenya is more of a darling to the WEST than Tanzania is, hivyo wakachomoka kirahisi. Sisi tukipelekwa kule itakuwa ni POLITICAL BLACKMAIL na hatuwezi kuchomoka hata kidogo mpaka pale tutakapokubali kuuza rasilimali za nchi ambazo zinahitajika sana hawa wenzetu wa Magharibi.
Leo hii wakitoa INDICTMENT FOR CRIMES AGAINST HUMANITY, kuanzia Madam President, Director of DGIS, Party Secretary, IGP, CDF na baadhi ya wanasiasa ndiyo itakuwa mwisho kukanyaga nje ya Tanzania. Hata zile akaunti zetu za kufanyia Operesheni zilizopo Uswisi hamtaweza kuzifikia hata kidogo.
Hivyo, msiingie kwenye huu mtego ambao kina UHURU na RUTTO waliingia, itakuwa ni jambo la fedheha mno kwa nchi kama Tanzania inayojitanabaisha kama kisiwa cha amani. Mambo mengi tuwe na msuli wa kuyaacha yapite tu, sisi siyo MIUNGU wa kuweza kuendesha (MANIPULATE AND CONTROL EVERY POLITICAL EVENT).
Acheni, Jirekebisheni, Tutaumia......