Tanzania tumedhalilishwa sana nchini Kenya. Isijirudie la sivyo tutalipiza kwa Uhuru Kenyatta desemba 9/2021

Tanzania tumedhalilishwa sana nchini Kenya. Isijirudie la sivyo tutalipiza kwa Uhuru Kenyatta desemba 9/2021

mleta mada inaonekana unapenda sana kudeka, wewe ni mtoto wa mwisho kuzaliwa??
tuanzie hapo kwanza...
 
Inaelekea una taarifa za kila jambo mkuu.
Inamaana haukuona alivyokuwa na mwenyeji wake ikulu Mama akipigiwa gobore 21 na kukagua manamba kwa heshima zote?

Huwezijua mwenyeji wake alikua na masahibu gani au ratiba zilikuaje.

Punguza kidogo roho mbaya inayochagiza kisasi...umeenda mbali sana kupanga adhabu bila kujipa muda ujue ukweli wa mambo.

Inamaana kweli serikali wanaweza kuusikiliza huu ushauri wako???
Anataka kuleta mambo ya jiwe huyu,eti ukimwaga mboga namwaga ugali,jiwe alikua chanzo cha mipaka yetu na Kenya kifungwa mara kwa mara.
 
Tusitake kukuza mambo yasiyo na msingi jamani!
Kweli kabisa, nafikiri Watz tujaribu kupunguza Low-key discussions na kuwa too subjective kwa kila kitu na badala yake labda, tujikite kwenye issues za kwa jinsi gani twaweza tatua, mambo na changamoto zetu nyingi na za msingi zinazotukabili....kaazi iendelee.
 
Jambo ambalo hulijui ni kwamba linapokuja suala la usalama hasa nchini Kenya kwenye ugaidi. Jua kwamba unapopokelewa na Rais mwenzio unakuwa salama zaidi kiulinzi. Sisi hatukupokelewa na PSU ya Kenya. Tulijitegemea. Vipi lingetokea la kutokea si tiyari CDF Mabeyo angeshafunga mipaka? Naongea kama mtu wa diplomasia. Ulijua kwa nini mama alivaa rangi maruni? Au unadhani ni urembo kwake? Unataka shule?!
Haya mambo ya kuvaa rangi fulani yanalisaidia nini taifa?Kwani tuko harusini?
Tulichokitaka ni mama kurudisha uhusiano na wakenya uliovunjwa na jiwe,
Tulitaka mipaka iwe huru baina ya nchi zetu watu wafanye biashara kwa uhuru,
Haya mambo ya kuvaa rangi gani subiri siku ya harusi.
 
subiri akienda marekani akapokelewe na afisa mtendaji wa new york uje ulielie tena hapa
 
Haya mambo ya kuvaa rangi fulani yanalisaidia nini taifa?Kwani tuko harusini?
Tulichokitaka ni mama kurudisha uhusiano na wakenya uliovunjwa na jiwe,
Tulitaka mipaka iwe huru baina ya nchi zetu watu wafanye biashara kwa uhuru,
Haya mambo ya kuvaa rangi gani subiri siku ya harusi.
Nenda chuo Cha diplomasia Kurasini pengine ukajua ninaongea nini.
 
Tanzania ni nchi kubwa Afrika Mashariki. Kihistoria Tanzania ina heshima kubwa duniani.

Tumesikitika sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan na ugeni wake akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya badala ya Rais kama mwenyeji wake.

Tukumbuke Rais (mwenyeji) anapokupokea unakuwa na Ulinzi wote wa uhakika. Badala yake SSH alilindwa na walinzi wa Tanzania bila wenyeji.

Kwa nini mama yetu hakupokelewa na Uhuru Airport na badala yake baada ya sisi kulalamika ndipo Kenyatta anajibaraguza kumsindikiza Airport kurudi Dar? Hii ni dharau sana. Je, ni kwa sababu ya jinsia yake? Hatujapenda hii. Tumenyong'onyea sana kwenye ndege.

Naye mwaliko wake mama Mulamula atampokea sherehe za Uhuru iwe 50/50. Ova
#FreedomIsBack
Kama watu mnaoambatana na Mama Samia, ni watu kama ninyi, basi tayari ni hasara kubwa kwa Taifa!
 
Kwanza ni dharau mwanaume mzima nikampokee Mwanamke Airport,naweza kumsindikiza sio kumpokea.
Nipo na Uhuru Kenyatta katika hill.
 
Jambo ambalo hulijui ni kwamba linapokuja suala la usalama hasa nchini Kenya kwenye ugaidi. Jua kwamba unapopokelewa na Rais mwenzio unakuwa salama zaidi kiulinzi. Sisi hatukupokelewa na PSU ya Kenya. Tulijitegemea. Vipi lingetokea la kutokea si tiyari CDF Mabeyo angeshafunga mipaka? Naongea kama mtu wa diplomasia. Ulijua kwa nini mama alivaa rangi maruni? Au unadhani ni urembo kwake? Unataka shule?!
Hata kwenye usalama inaonekana hujui kitu. Magaidi wanawatafuta Wakenya. Kuwepo kwa marais wawili ni target ya kuvutia zaidi kwa magaidi kuliko uwepo wa Rais wa Tanzania bila ya Rais wa Kenya.

Kiintelijensia, wakenya wamefanya vizuri. Wakati ilipotarajiwa Uhuru angeenda uwanja wa ndege, hakwenda. Walipodhani kuwa hawezi kwenda kumuaga airport SDH maana wakati wa kuja, hakwenda, ndiyo ameenda.
 
Huo ni utaratibu wa nchi nyingi sana,raus hapokewi na rais
Wewe Acha uongo utaratibu wa wapi kuwa Rais hapokelewi na Rais,sema Marais nao Wana dharauriana kama ambavyo ilivyo katika Jamii.

Kupokelewa na Rais mwenzako kama ni safari yako ya kwanza katika Nchi hiyo itategemeana na CV yako duniani au CV ya Nchi yako.

Unachosema aje sa HV Joe Biden Tanzania apokelewe na Mulamula.
 
Nenda chuo Cha diplomasia Kurasini pengine ukajua ninaongea nini.
Kama hicho chuo ndiyo ulichosoma, na haya ndiyo uliyosomea, basi hicho chuo kitakuwa ni jalala. SSH siyo Rais wa kwanza Duniani kupokelewa na Waziri wa masuala ya nje.

Mataifa mengi, Rais mwenyeji hukaa Ikulu, kumsubiria mgeni wake ili ampokee, na siyo kumsubiria pale airport.

Lakini suala la Rais kwenda airport kumsubiria Rais mgeni, hutegemea pia ushauri wa wanausalama.
 
Back
Top Bottom