Tanzania tumeingia nyakati ambazo watawala ndio majambazi na wauaji

Tanzania tumeingia nyakati ambazo watawala ndio majambazi na wauaji

Rungwe88

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
353
Reaction score
722
Zamani wananchi tulijua kwamba majambazi, wauaji, waporaji ni vikundi vya kihalifu vya watu binafsi hivyo wananchi hatukua na wasiwasi sababu ilikua rahisi kukabiliana navyo kwa kwa namna mbalimbali tukishirikiana na vyombo vya ulinzi, watanzania tulikosoa, tulilalamika, tulipaza sauti, tulipambana kujilinda na vikundi au uhalifu huo kwa namna nyingi.

Ila kwa mazingira ya Tanzania ya Leo watawala ndio wamegeuka majambazi, wauaji, watekaji, mafisadi n.k
Kitu Cha ajabu ni kwamba wanatumia mwamvuli wa uongozi kujificha na hayo mambo pia wanapofanya mambo hayo hawataki kukosolewa, hawataki kupingwa Wala hawataki wananchi walalamike kwa namna yeyote.

Kuna baadhi ya watu walionesha uthubutu wa kukemea hayo maovu yanayofanywa na hao watawala ila mfano Gwajima, Polepole, Katibu wa TEC, wananchi, asasi za kiraia, vyama vya siasa n.k ila wameishia kuuwawa, kutekwa, kufunguliwa kesi n.k

Vijana wakitanzania walionesha hisia na hasira zao kwa kuandamana ila waliishia kuuwawa kwa maelfu na wengineo kupotea kusikojulikana.

Wananchi hawana amani kwenye nchi yao Sasa, mtu akitoka asubuhi Hana uhakika asilimia mia kama atarudi nyumbani salama kutokana na vitendo vinavyofanywa na utawala wa sasa.

Swali
1. nyinyi watawala mnataka wananchi wakae kimya wanapoona ndugu zao wanatekwa na kuuwawa?
2. Watawala mnataka wananchi wakae kimya wakiona ufisadi wa kutisha wa rasilimali zao kama bandari, misitu, wanyama n.k?
3. Watawala mnataka wananchi wakae kimya wanapopokwa haki Yao kikatiba kuchagua viongozi wanaowahitaji n.k
 
Zamani wananchi tulijua kwamba majambazi, wauaji, waporaji ni vikundi vya kihalifu vya watu binafsi hivyo wananchi hatukua na wasiwasi sababu ilikua rahisi kukabiliana navyo kwa kwa namna mbalimbal
Inalazimu kwa namna fulani wananchi wakabiliane pia na huu ujambazi mpya. Jambazi ni jambazi tu; usipolikabiri litaendelea kukupa shida siku zote.

Ni lazima mbinu mpya zitumike katika kukabili ujambazi uliovamia mamlaka ya nchi. Ukweli ni kuwa tukiponda kilipo kichwa cha joka hili, kiwiliwili chake hakitupi matatizo sana.. Mbinu mpya zinatakiwa kufanikisha hilo.
 
Mbinu zimeshapatikana ndugu, kinachosubiriwa ni wakati sahihi wa kuzitumia.
Chuma hufua chuma, utakua ni mwendo wa roho mkononi kwa kila mtu sasa
 
hii picha itumike kuwa picha ya raisi akitumia kiuno na kupuliza mitungi ya gesi.
downloadfile.jpg
 
Ni kweli, serikali na viongozi ndio sasa yamekuwa majambazi yanaua na kuiba, yakiongozwa na lile shetani Samia, ni kupambana tuu la sivyo tumekwisha, na sasa naanza kuona tishio lingine ndugu zetu wasiojielewa wameanza kutumia udini , naamini wanatumiwa na Samia
 
Hakika, inabidi tupambane sana
 
Back
Top Bottom