Mwanahalisi20
Senior Member
- May 5, 2020
- 132
- 152
Dunia imezizima, Africa imezimama na Marekani imezizima. Kifo cha Mmarekani mweusi Mr. George Floyd(48) kimebadilisha kabisa mwelekeo wa siasa za Kibaguzi si Marekani tu baali dunia nzima ikiwemo Tanzania.
Siasa za Kibaguzi zipo tu kila sehemu duniani. Kuna watu wanafikiri ubaguzi ni wa rangi tu. Ubaguzi ni ubaguzi tu na uko wa Aina tafauti Upo Ubaguzi wa rangi, jinsia, siasa, kabila, Ukanda n.k.
Tanzania ni nchi iliyo jijengea heshima kubwa Africa na dunia nzima kwa kupambana na Ubaguzi wa rangi hasa wakti wa Uhai wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere(RIP).
Lakini kwa hivi Karibuni Tanzania chini ya Uongozi wa CCM Awamu ya 5, tatizo la Ubaguzi limerudi nchini kwa Kasi ya ajabu. Ubaguzi huu umejikita kwenye Siasa za Kibaguzi zinazotekelezwa na CCM.
Serikali ya CCM Tanzania chini ya Rais John Joseph Pombe Magufuli. Kuanzia 2016 baada tu ya kuingia Ikulu, Magufuli alipiga marufuku Vyama vingine vya siasa kufanya chochote; marufuku kufanya mikutano nje na ndani, marufuku maandamano, marufuku vikao vya kichama nje na ndani, marufuku kufanya kampeni wakti wa Chaguzi ndogo za Udiwani na Ubunge.
Serikali ya CCM ikaanza Sera za kuwabana Viongozi wa Kisiasa toka Upinzani kwa kuwakamata na kuwaweka Mahabusu,kuwafungulia kesi Mahakamani na KUWAFUNGA jela.
Kifo cha George Floyd kiwe fundisho kwa Viongozi wa CCM na waache hi tabia. Uchaguzi Mkuu wa 2020 bado miezi 3 tu, shime kwa CCM na Serikali yake kukomesha ubaguzi huu Vinginevo Tanzania itaenda kugeuka America ya Africa na kitakuwa na kina George Floyd wengi Sana watatengezwa na Serikali hii ya Rais Magufuli kama Serikali ya Rais Trump wa Marekani ilivyo sababisha kifo Cha George Floyd.