Kuna Dira ipo toka wakati wa mkapa, na kuna Dira ya juzi awamu hii. So sio kweli kwamba Nchi Haina Dira, ila ni wananchi tu wapo tuu busy kwenye petty issues na kutofuatilia mambo ya maana.
Dira ya wakati wa mkapa iliitwa Dira 2025 na ilianza 1999 hadi mwaka 2025.
Dira ya sasa ni 2050 inaanza mwaka huu hadi 2050.
Dira ya kwanza unaweza kusoma hapa
View: https://www.scribd.com/document/470890495/Dira-Ya-Taifa-Ya-Maendeleo-2025
Na huu muhtasari wa Dira ya 2050
Unategemea nini kama vision yake ilikuwa awe muhudumu wa ndegeNchi inaenda kwa kufuata kiongozi mkuu anataka nini, ila haifati kuwa kwasasa kama nchi tunahitaji nini..!
Si mbaya kiongozi kuwa na vipendeleo vyake lakini ni vyema mapendekezo ya nchi kwa wakati huo yanatakiwa yapewe kipaumbele!.
Leo anakuja rais anaependa nakuamini ktk uanzishwaji wa taasisi, lakini nchi kwa wakati huo haihitaji hilo!.
unakuta matatizo yanayowakuta wananchi ni tofauti na malengo ya kiongozi!, huku ni kucheleweshana ktk kufikia ile inaitwa nchi ya asali na maziwa!.
Pia kumekuwa nashida hii yakuheshimu kiongozi kwa nidhamu ya uoga!, kila atakachofanya ni kupiga makofi. wenyewe wanaita UCHAWA!, tusipokuwa makini hili linaenda kuipoteza nchi. watu wamekalia kujaza matumbo yao hafikirii kesho ya wajukuu zake itakuwaje!.
Ni dhahiri kabisa swala la kurekebisha katiba hatutakiwi kuliacha lakini kila kiongozi analipita nakuliona kama sio swala linalomuhusu!.. imefika muda sasa lazima tuelewe hivi sasa si kama miaka ya nyuma vitu vinatakiwa kubadirika, hivyo swala la kurekebisha katiba ni halikwepeki!.
Nina mashaka na uwezo wa uongozi wa viongozi wa taifa hili!, Haiwezekani kundi la watu miatatu ni kupiga makofi nakushangilia kila kitu!, nina mashaka na kile kinachoitwa usomi!.
Ya kwamba aliempinzani ndie anatakiwa kupinga ila wewe wa chama tawala ni kupiga makofi tu hata kwa kitu kisichostahili!.
Rai yangu kwa viongozi waache ukiritimba waangalie nakutatua vitu ambavyo ni tija kwanza, Vilevile wananchi tunatakiwa kujitambua kwenye kusema hapana tuseme na tusimame kwa pamoja kwenye yale malengo makuu ya nchi ambayo moja kwa moja yanamnufaisha kila mtanzania!.
Ile dhana ya kula kwa urefu wa kamba yako, iwe ya haki na wala si janjajanja!.
Maswala yakusheherekea doti za kanga chumvi na sukari ni sawasawa na kujididimiza kwenye haki yako ya msingi wewe mwenyewe!.
Mwenye ufahamu na afahamu, jitafakari.
Umesoma Dira ina kilimo kwanza? Usichanganye maneno ya wanasiasa na Dira ya Taifa ambayo imeandaliwa na proffesionals.Kama dira ipo inakuwaje baadhi ya sera tunaziona katika awamu moja na awamu nyingine huoni mwendelezo wake,mfano kilimo kwanza