Tanzania tumepewa bahari, tuitumie kuongeza pato la taifa

Tanzania tumepewa bahari, tuitumie kuongeza pato la taifa

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
6,076
Reaction score
15,685
Tanzania tumepewa eneo kubwa sana la bahari ya Hindi ambapo tumejaliwa kuwa na bandari, fukwe, visiwa na hifadhi za asili.

Bahari tuliyonayo inatosha kuzalisha mapato kuzidi hata sekta ya madini ambayo sisi tunaitolea macho.

Zifuatazo ni shughuli ambazo zikifanyika kwa ustadi zitazalisha mapato makubwa ambayo hayajawahi kukusanywa tangu tupate uhuru:

1. Uvuvi wa kisasa
Wizara ya kilimo inabidi iwape vibali wazawa na wageni wenye uwezo wa kumiliki meli za kisasa katika uvuvi. Uvuvi huu wa majahazi na boti ndogo unatunyima mapato.
Inabidi meli za kuvuta Trawler au Longline ndio zitumike kuvua samaki eneo la bahari kuu, hii itasaidia pia ajira na upatikanaji wa chakula.

2. Kujengwa kwa bandari ya uvuvi na viwanda vya samaki
Kwa kipindi kirefu tumekosa bandari ya uvuvi na meli kubwa za uvuvi kushindwa kupata sehemu ya kupaki.

Uwepo wa viwanda vikubwa vya samaki vitsaidia ongezeko la mapato na ajira.

3.Nchi kusajili meli ambazo zitapeperusha bendera yetu
Nchi kama Panama, Liberia, Visiwa vya Cayman na Hong Kong vimeweza kupata kodi kwa kusajili meli. Hata sisi tuna uwezo wa kusajili meli nyingi zaidi, Raisi alisitisha usajili baada ya meli nyingi zenye bendera yetu kupatwa na skendo za madawa ya kulevya.

Tuna watalaamu wa Maritime Law na Flag and port state control tuna uwezo wa kusajili na kusimamia sheria vizuri ili kusajili meli nyingi zaidi.

4. Bandari zetu kuwa ndio lango kuu la mizigo kwa nchi jirani
Mapato tunaweza kuongeza zaidi endapo bandari yetu itaweka tozo rafiki, vifaa vya kisasa na kupunguza muda wa meli kushusha na kupakia na muda wa maroli kuingia kupakia na kushusha(Truck turn around time).

Nchi kama Singapore ni mfano mzuri wa kuigwa na kujifunza, wao wametumia bandari yao kuwa kitovu cha biashara na ndio moja ya bandari zilizo busy duniani na ni tegemeo kubwa la pato lao.

5. Fukwe zetu kutumika kwa utalii wa kisasa
Fukwe zetu kuanzia kaskazini mashariki mpaka kusini zimejaliwa kuwa na mandhari ya kuvutia na mchanga mzuri. Utalii wa fukwe utachangia kuongezeka kwa pato na ajira kwa vijana.
 
Back
Top Bottom