Tanzania tuna tatizo la msingi sana la ujinga na upumbavu


Mnhhhhhh

Nimekuambia kingereza kikifundishwa kuanzia vidudu, hakutakua na tatizo kwenye kuelewa...

Umetaja kukariri ndio tatizo,

Kwa muktadha huo tatizo liko kwenye mitaala...

Haijitoshelezi au haipo inayowa encourage wanafunzi kuwa Independent thinkers...
 
Haya Sisi sote wajinga na wapumbavu, tuambie wewe mwerevu cha kufanya tuondokane na hayo maujinga na maupumbavu! Usikosoe tuu ! Toa suluhisho kama mwana JF GREAT THINKER !
 
Kwa hiyo wewe bado unang'ang'ania kiingereza?


Unadhani hayo mataifa yanayotumia lugha zao za asili kufundishia hazikuiona lugha ya kiingereza?
Unadhani wao ni wajinga kutumia lugha zao kufundishia?
Je nchi kama ya Kenya ambayo inatumia lugha ya kiingereza toka elimu ya chini mpaka chuo kikuu unaiona imefanikiwa?
 
Haya Sisi sote wajinga na wapumbavu, tuambie wewe mwerevu cha kufanya tuondokane na hayo maujinga na maupumbavu! Usikosoe tuu ! Toa suluhisho kama mwana JF GREAT THINKER !
maendeleo yanaletwa na mawazo kinzani ambayo yanazaa mawazo chanya,ananchomanisha mtoa mada!
 
Unajua kwamba na wewe ni mpumbavu?
 
Watafiti wameona hilo lakini utafiti unaweza kupingwa na utafiti pia. Mimi naona tatizo ni kutojitambua na uvivu.
Tukiondokana na ujinga na uvivu lugha yeyote haiwezi kuwa tatizo.
Wako watoto wa pre school wanajieleza vizuri kwa kiingereza lakini mtu wa form six anashindwa kwa ninii. Elimu ya darasani haikuletwa na waafrika haya masomo tumeiga kwa wazungu. Ni muhimu sana tujue vizuri lugha zao kama ilivo kujua lugha yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Genge la CCM hawawezi kuwaza kuleta maendeleo, LENGO lao ni KUTAFUNA NCHI na KUWARITHISHA watoto wao KEKI YA TAIFA.

Watu masikini wako easily radicalised and controlled. In short watu wengi hawajielewi.

Mtu yuko tayari kuvumilia TABU NZITO iliyotokana na maamuzi ya mtawala fulani kwa kuwa tu mtawala huyo anatoka KABILA LAKE, DINI au CHAMA CHAKE.

Tena hata hawatumii nguvu kubwa, ukishamnunua DIAMOND ushanunua MISUKULE wake wote, vivyo hivyo kwa MBOWE, GWAJIMA, MWAMPOSA, LIPUMBA

Mbaazi na Korosho zilionesha DALILI za kumkomboa MKULIMA, Wamezivuruga wamekulima wamerudi ZERO.

PESA za kulipa wakulima wa korosho, Bima, Ajira mpya au kujenga barabara hakuna, ila PESA za kuhonga wabunge wa upinzani wahame na kufanya chaguzi za marudio zipo siku zote.

Binadamu wenye FIKRA HUQU Duniani ni WACHACHE SANA.
 
Nakuomba unitajie nchi yoyote duniani iliyoendelea, ambayo haitumii lugha yake ya asili kama lugha ya kufundishia.
 
mkuu umeshamaliza, haiwezekani miaka 58 ya uhuru serikali inakwepa suala muhimu la ujenzi wa shule inawaachia wananchi jukumu la kujenga miundombinu ya shule halafu wao jukumu lao linakuwa ni kununua v8, prado, vx etc.
hii ni kweli kabisa mwananchi wa Tanzania tunabebeshwa mzigo mkubwa sana! hii initwa nguvu ya jamii unachangia michango ya shule ,zahanati,Hospitali n.k bado watu wanatoa direct tax na indirect tax.
 
huwezi fanya ugunduzi wa kitu chochote kwa kutumia lugha ya mtu mwingine!
 
Mleta mada ninakuheshimu sana hivyo usikwazike swali langu. Umegundua tatizo hili wewe mwenyewe ukiwa ndani au nje ya hao wajinga na wapumbavu?
 
Nikajua mwisho utaweka suluhisho. Mawazo yako wewe kama wewe umechukua hatua gani. Au na wewe umekubali kuwa mmoja wa wapumbavu.
Hana haja ya kuweka suluhisho. Viongozi wa nchi hii wameshauriwa mazuri mengi ya kufanya kwa mustakabali wa Taifa. Lakini wanasiasa tulionao wanafikiri uchaguzi na kubaki madarakani tu. Mimi naamini mafanikio ya mtu moja moja ili tuseme tuna Watanzia wengi wenye uchumi wa kati na maendeleo ya Taifa kiujumla unategeme utawala bora wa wanasiasa.
 
mkuu umeshamaliza, haiwezekani miaka 58 ya uhuru serikali inakwepa suala muhimu la ujenzi wa shule inawaachia wananchi jukumu la kujenga miundombinu ya shule halafu wao jukumu lao linakuwa ni kununua v8, prado, vx etc.
Walio wengi wanatetea nafsi zao hivo mtu akipata cheo anaangalia maslahi yake na sio ya jamii. Ndio maana ukipata cheo hata jamii itasema umeula.
Kuna watu duniani walifanya makubwa kwa mateso na sasa tunafaidi. Chukua wagunduzi wa kisayansi. Leo hii sisi tunaangalia tu maslahi binafsi na misifa ya hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mnhhhhhhhh

kuna vyuo kibao vinafunsisha kwa kingereza kwenye nchi hizo ulizozitaja...

Kwa nini tuwa limit wasomi wetu..

Wakitaka kufanya kazi nje ya nchi...???????

Halafu kuja na data,specific kuonyesha tatizo la lugha ya Swahili kwenye nchi yetu limechangia/kutochangia maendeleo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…