Tanzania tuna uhuru wa habari, ila media oga! Tungekuwa mbali sana kimaendeleo, rushwa, uhujumu, ufisadi, ubadhirifu vingeibuliwa kabla

utakuwaje mwoga kama una uhuru ?, samahani nimesoma heading na sio content, huenda nimepotoka.., kama ndivyo nisamehe.., ila heading yako ni imenipa maswali (kama kuna uhuru wanaogopa nini au wanamwogopa nani)
 

Where is Azory, Bwana Paskali? Tuanzie hapo!
 
Anachunguza anagundua kuna UFISADI,anamfuata mtuhumiwa atoe pesa au asubiri kuumbuka kwenye media (Blackmailer).
Kuna uchafu mwingi,sio kuangalia sehemu mmoja tu.
Habari imegeuka maslahi ya mtu au kundi la watu ni ipi iandikwe na ipi itupwe kapuni.
Tuna safari ndefu ya kuwa upande sahihi wa habari.
 
Hii habari umeileta vizuri sana lakini huko kwenye "vichwa maji"yaani ukisomama kwa umakini yakinifu na wewe umekandia fulani ni kweli "vichwa maji"
 
Where is Azory, Bwana Paskali? Tuanzie hapo!
Mkuu Everest Chahali, kwanini hili swali uniulize mimi?.

Azory yuko hapo alipo alipopelekwa na wale watu waliomchukua so does Ben Saanane wetu, no one knows majaaliwa yao hivyo it's not fair, kuniuliza mimi walipo.

Na sii hao tuu, hata Tundu Lissu, alishambuliwa na watu wasiojulikana.
P.
 
Mkuu mi
sidhani kama Karsan katumwa, bali Paskali katoa maelezo ya karsan kwa namna yake na tafsiri yake, kama una access nzuri ya internet we ingia tu youtube utafute hicho kipindi cha JICHO LETU KATIKA HABARI umsikie mwenyewe ndipo umjaji. Kumbuka Paskali kwasasa ni mpiga matarumbeta wa msukuma mwenzie, Hayupo real kivile kama alivyokuwa awali, japo yeye bado anajiona ana uwezo mkubwa wa kuwashawishi watu kwakuwa tu tulimwamini sana kwa machapisho yake yaliyokuwa yana utafiti mzuri hapo awali.
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Rais ni sehemu ya Bunge, ndiye boss. Ndio maana Job ana mhanya jamaa. Anasema yeye ndiye mlipaji.

Uliona wapi bunge linakusanya kodi..? Sasa wewe mchezee bwana Mapato uone kama utapewa mgao.

Utapata 4% ya bajeti. Ama unajifanya huoni wizara zinavyopigwa panga kwa bajeti iliyopitishwa na bunge na hakuna lolote lile.

Acha kuwaingiza chaka akina Job na timu yake,wasije limia meno.

Sent using iphone pro max
 
Umesema kweli, imekuwa Wasukuma wote wamekuwa CCM, tena wakereketwa.
Wako radhi hata kukushambulia uksema vibaya mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawatakia waandishi wenzangu wote wa habari, maandimisho mema ya siku hii ya kimataifa ya uhuru wa habari.
P.
 
Tanzania tuna uhuru mkubwa wa habari kama alivyosema Rais Mama Samia. Tatizo ni sisi media wenyewe
p
 
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari ambaye ni mwandishi wa habari huru na wa kujitegemea kwa kujitolea na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo huru cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari kwa media zetu za Tanzania yetu.

Nawatakia maadhimisho mema ya siku yetu hii ya leo na uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…