Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wakuu,
Katika kupata ufafanuzi na tafsiri sahihi juu ya mipaka na mamlaka ya bunge maalumu dhidi ya iliyokuwa tume ya katiba katika uandaaji wa rasimu ya katiba,bila shaka tunahitaji msaada ya wataalamu kutoka nje ambao watakuwa "neutral" na sio hawa wa ndani wenye maslahi binafsi katika jambo hili.
Nasema hivi kwasababu hivi sasa watanzania tunapotoshwa na hawa wanaojiita wataalamu wa sheria na mambo ya katiba.Wengi wao wanatoa maoni na ushauri wao si kwa misingi ya kuzingatia taaluma zao,bali kwa maslahi binafsi,kutumika na pengine hata kununuliwa kwa faida ya makundi fulani au taasisi wanazotoka au zilizowatuma.
Katika hili hata waandishi wa habari nao wanatumika kwa njia moja au nyingine ili tu malengo ya watu fulani katika jamii au taasisi fulani yatimie kwa kupata katiba wanayoitaka.
Ningekuwa na mamlaka ningesitisha zoezi hili na kualika wataalamu kutoka nje waje watupe ufafanuzi na maelezo ya msingi kabla hata ya bunge maalumu kutunga sheria na kanuni zitakazotumika katika bunge hilo na baadae waanze kuijadili rasimu hiyo.
Katika hatua tuliofikia na jinsi mambo yanavyokwenda,wataalamu wa ndani si wa kuaminika tena kwani wengi wao wamebeba agenda zao na za watu wao!