Waafrika wenyewe tuna mchango mkubwa sana kwenye kudidimiza maendeleo yetu ya kiuchumi, stability za mataifa yetu na evolution za kimawazo katika jamii, vizazi vya leo haviwatendei haki vizazi vyao vya baadae. Aiwezekani baada ya miaka 60 ya most african independencies the social thinking is almost the same, the causes of the problems are the same and the solutions are the same (external interference from our colonial masters).
Kwenye dunia za wenzetu on the same time scale the thoughts have evolved with time, mawazo ya babu wa kizungu si sawa na vijana wa leo in terms of morals, tolerance and political rightness. Sisi kila siku tunaona kwenye dunia matatizo ya mawazo tofauti ndani ya jamii yanavyoweza kuwa chanzo cha chaos lakini bado politicians are always using those circumstances to further their personal ambitions.
Kizazi cha leo kinajukumu la kurithisha mawazo mapya kizazi cha kesho, kama JKN aliweza kupigana kupunguza fikra za kidini na kuwabana watu wa dini nje ya siasa na kutumia nguvu nyingi sana kwenye propaganda za utaifa, maraisi waliofuata walitakiwa kuelekea kutoa kabisa mawazo ya ukabila ndaani ya fikra za watu (eventually we will have to get there, that is very important hili jamii kushirikiana kikamilifu, na wazungu walichomana moto hili kuwekana sawa).
Sisi leo tupo kwenye karne ambayo kuna elimu na mambo yamesonga mbele ni kujifunza tu jinsi waliopo mbele yetu waliwezaje, hatuhitaji trial and error approach iliyowafikisha hapo, maana wao kama walichomana zamani, leo wameshajua kumwekea mtu mawazo tumia mass media kueneza propaganda na sheria maana ni raisi kuzi monitor.
Sasa leo kiongozi anapewa jukumu la kuandika katiba, kitu ambacho kinaenda kukaa miaka na kwa faida ya kizazi cha baadae, anaenda kuweka agenda zake wakati yeye mwenye ni mpita njia tu hapa na anajua matatizo ya leo, badala kulenga kufuta hayo mawazo anakuja na mapendekezo yenye kuchochea hayo mawazo ya mgawanyiko. Wanasiasa tena imekuwa wanatafutiana njama za kutafuta uhalali wa namna zao ndio sawa.
Kwenye kujiuliza kwetu cha muhimu si kuangalia nani yuko sawa leo, cha muhimu ni mawazo ya nani yanamfikiria "Rajabu" na "John" watakaozaliwa in 2040, hawa watu Tanzania bado waikute yenye ukabila, udini, upendeleo, umaskini mkubwa. Sisi kizazi cha leo tunalenga nini kwa sasa kwa ajili ya hawa watu wa kesho kwa matendo yetu.
Utakuja kugundua swala kubwa na tatizo kubwa kwa sasa ni nguvu za raisi (kwenye katiba ya sasa, hili leo aliitajiki tena na muda wake umepita), hili tuanze kujenga misingi imara ya kukosoana na kushitakiana, kuanza kuweka watu kutokana na sifa zao hili taifa lisonge mbele na mawazo yenye kutupeleka mbele. Leo tunaangaika na katiba na maswala ambayo si matatizo halisi zaidi ya mitazamo tofauti ya watu wachache. Lakini hakuna mtu anaefikiria raisi ajae hawe na sifa gani mfano kwa hali tuliyonayo hili tusogee mbele kwenye sifa za kiongozi tujali uzoefu wa mtu, au kazi zake alizofanya, mtu mwenye mawazo ya kesho na jinsi ya atakavyotusogeza etc.
Tunarudi palepale kwenye mawazo ya mleta mada, maana tumefikia hatua hatumianiani kwenye kulijenga taifa letu tunataka watu watoke nje kujakutusaidia, watu hao hao wenye malengo ya kuja kuchukua mikataba isiyo na haki leo kwenye dunia ya biashara.
Kwa mtaji waafrika tuna safari ndefu sana, kama watu wa leo hatuwezi kuwaachia chochote watu wa kesho kukiendeleza zaidi ya mawazo ya chukichuki tu, kibaya zaidi tunataka bomoa hata hatua chache tulizopiga na kuwarudisha nyuma zaidi.