Tanzania tunahitaji Nini ili kufikia hizi Level?

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Habari wana-Jukwaa.

Nipo najiuliza maswali mengi sana kila nikiingia sehemu nikaona Mapungufu flani,nikitoka nawaza hivi lini na sisi tutakua kama Nchi Flani nikitoka sehemu hio nikipita sehemu Nyingine nikiona Tatizo najiuliza Lini tutakua kama Nchi Flani,Saivi ni miaka 60+ tokea tupate Uhuru lakini bado sielewi ni mda gani itachukua Nchi yangu Tanzania kuwa ...

1: Na uzalishaji Mkubwa wa Chakula Kama=CHINA
2: Kuwa Nchi salama kama ICELAND
3: Kuwa na Technology kubwa kama JAPAN
4: Kuwa na Elimu Bora kama U.S.A
5: Kuwa na Miundombinu Bora kama HON KONG
6: Huduma za Afya Bora kama S.KOREA
7: Kuwa Nchi yenye Ushwishi kama U.S.A
8: Kuwa Nchi yenye Uongozi Bora kama GERMANY
9: Kuwa Nchi yenye uzalishaji mkubwa katika viwanda kama CHINA

Kiukweli kuna Mengi sana Nawaza, hasa pale nikiona vile tupo Nyuma Na ukiangalia na Mda tulionao toka tupate Uhuru.. hadi najiuliza ni tunahitaji kitu gani kufikia hayo yote na mengine Mengi?

Labda mnipe Jibu tunahitaji Nini ili kufikia hizo Level?
 
Tutafika ila inapaswa kuanza upya katika kila kitu kuanzia katiba hadi uongozi uliopo.

Mana kwa sasa the whole system is corrupted.
 
Tunahitaji wananchi wengi wawe na Akili Nyingi na Utashi.

Ili kati yao iwe rahisi kupata Viongozi wazuri.
 
Sio rahisi, upigaji ni mkubwa mno, hela inayopigwa ni nyingi kuliko ya maendeleo
Kitu cha tshs 20m kinanunuliwa kwa tshs 150m (repoti ya CAG -MSD)
 
Kwa mifano yako, inaonekana kila nchi ina ubora kwenye angle flani kama ndio hivyo.

Basi tujiulize angle na sisi tujitahidi kuboresha tuwe best na tuwe mfano kama yako.
 
Kwa mifano yako, inaonekana kila nchi ina ubora kwenye angle flani kama ndio hivyo.

Basi tujiulize angle na sisi tujitahidi kuboresha tuwe best na tuwe mfano kama yako.
Exactly lakini ukiangalia hata hizo Zimepiga hatua kubwa kila angle ila kwenye hizo ndio zimeenda sana
 
Kila mtu awe na taarifa sahihi kwa vipomo vyenu, kila mtu atimize wajibu wake.
 
1.Mapinduzi ya fikra.
2. Uzalendo wa kweli.
3. Commitment.
4. Kufanya kazi zenye manufaa kama watumwa kwa moyo mnyoofu.
5. Mabadiliko ya kikemia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…