Tanzania tunahitaji noti za sh 100,000/=

Firigisi

Member
Joined
Feb 13, 2009
Posts
91
Reaction score
33
Wadau kutokana na huu mfumuko wa bei na kushuka ''purchasing power'' nafikiri
tunahitaji noti za sh 100,000 zichapishwe kuondoa mzigo wa minoti.Sijui itakuwa na
implication gani kwenye uchumi ,waliobobea kwenye hayo maswala naomba mtudadavulie!

Nawasilisha na pia nawatakia mwaka ujao wenye mafanikio tele.
 

itashusha mno thamani ya shillingi yetu. Ni jambo la hatari sana kwa uchumi,,sababu faida hakuna,,halafu hasara ni nyingi mno. Mkuu unajua kiwango cha chini cha mshahara wa mtanzania?
 
itashusha mno thamani ya shillingi yetu. Ni jambo la hatari sana kwa uchumi,,sababu faida hakuna,,halafu hasara ni nyingi mno. Mkuu unajua kiwango cha chini cha mshahara wa mtanzania?

Mkuu tiririka vizuri kitaalamu basi ,kwani inauhusiano gani na kima cha chini cha mshahara, na inakuwaje kuchapisha noti mpya kushushe thamani ya shilingi? Naomba kuelimishwa!
 
Labda tutumie dola ya marekani kama ambavyo zimbabwe wanatumia rand ya africa kusini
 
Mkuu tiririka vizuri kitaalamu basi ,kwani inauhusiano gani na kima cha chini cha mshahara, na inakuwaje kuchapisha noti mpya kushushe thamani ya shilingi? Naomba kuelimishwa!

Ntarudi kukuelimisha zaidi mida mkuu,,sababu nahitaji nikufafanulie kwa kina..Anza na kufikiria kwa nini uchumi wa Zimbabwe uko mahututi ingali wanachapa mpaka noti ya milioni moja. Halafu jiulize pia kwa nini enzi za mwalimu Shillingi ilikuwa na thamani mno,,na kima cha chini cha mshahara kilikuwaje?
 

Mkuu kama ndio fani yako udadavue vizuri tupate mwanga wa kisomi zaidi!!!!!!
 
Mkuu tiririka vizuri kitaalamu basi ,kwani inauhusiano gani na kima cha chini cha mshahara, na inakuwaje kuchapisha noti mpya kushushe thamani ya shilingi? Naomba kuelimishwa!

- Kima cha chini cha mshahara ndiyo kiwango cha chini kabisa ambacho serikali inakisia kinamtosha mfanyakazi au raia mwingine yeyote wake aishi ndani ya mwezi au muda ulioaniashwa. Sina uhakika sana na kiwango halisi cha sasa, lakini kwa uelewa wangu ni 175,000 tshs. Sasa kwa mfumo wa wa kuwa na noti ya laki moja,,hawa mabwana watapewa noti mbili,,na chenji watatakiwa kurudisha,,hii itawasababishia wenye pato la ina hiyo kushindwa kununua vitu au huduma nyingi zaidi, sababu bei ya vitu nayo ni lazima ipande,,pale tu utakapoitoa hiyo noti ya laki moja. LAZIMA

Sasa kima cha chini ndivyo kinavyohusika,,kwenye makadirio ya mtu kuweza kukidhi mahitaji muhimu wa binadamu.

Lakini kima cha chini sio tatizo la msingi kwenye kuchapisha noti ya laki moja. Tatizo ni kupanda kwa bei ya vitu na huduma. Upandaji huu wa bei ya vitu kwa nchi ambayo haitengenezi hata kiberiti chake yenyewe,,kutasababisha tuongeze idadi ya vitu tunavyoagiza kutoka nje ya nchi( imports).
Sasa kwa nchi yetu ambayo kwa sasa tu thamani ya bidhaa iingizwayo nchini ( mostly used products) ni kubwa kuliko bidhaa zitokazo nchini( natural unused rare products) halafu unataka uongeze hilo gap liwe kubwa zaidi,,,
,maskini watashindwa hata kununua chumvi itakuwa hatari.

Kikubwa ni upandaji bei wa vitu,,utakaoshusha zaidi thamani ya fedha yetu,,na kusababisha tuhitaji dollar zaidi ili tuweze kununua hizo imports zaidi,,,hizo dollar tunatoa wapi?? tunauza natural resources zetu zaidi na zaidi..

Sasa ukiangalia faida ya kuwa na noti ya laki moja labda kwa ajili ya wallet,,sababu kweli siku hizi kukunja wallet haiwezekani kama una kilaki tano tu mfukoni.

cha muhimu ni kwenda na wakati,,kuboresha IT na matumizi ya card na m-pesa au huduma za staili hiyo zaidi,,ili pesa isibebebebwe nyingi sana kwa wakati mmoja na vile vile watu na serikali iweze kutrace matumizi na kodi yake inayopata vizuri zaidi.

Kuna mathara mengi ya kuwa na hiyo noti ya laki moja,,nadhani wengine watakunyunyizia zaidi.
 
Badala ya kukunja pochi, mtabebea kwenye makapu na badala ya kubebea laptop hayo mabegi yatageuka wallet za kubebea fedha

Tutajimaliza katika maisha. usiombe yatukute ya zimbabwe.

Ni hatari na balaa isiyopimika.
 
sahihi wahusika wafanyi kazi coz juzi nilipat ten milions nilipata shida sana kusafiri nazo ikanibidi nikauze ili nipate uuu shhuuu diiiii yaani usd
 
Thanks wakuu kwa michanganuo , kuna baadhi ya nchi kama Ghana wameshawahi kuondoa sifuri moja kwenye thamani ya pesa zao , ila purchasing power inabaki ile ile >>>mfano kwenye 10,000/
wanaondoa 0 inabaki 1000/ ili uwezo wa manunuzi unabaki ule ule wa sh 10,000/.........hili haliwezi kufanyika kama tunaona kuongeza noti za 100,000/ kutashusha thamani ya fedha?
 

Firigisi,,kitaalamu hiyo process inaitwa currency devaluation: Ni staili ya kuongeza thamani ya pesa zako: Wachina wamempiga sana US kwa staili hiyo:

Binafsi,,naona kabisa inawezekana kuishi bila noti ya 10,000. Yaani kiwango chetu cha juu cha pesa kiwe ni shs 5,000. Halafu wachape noti ya shs 3000 na shs 4000 tu. Tatizo njia hii,,SIO LAZIMA bei ya bidhaa ishuke, sababu ni ile ile,,uzalishaji wetu ni mdogo mno,,tunategemea bidhaa nyingi kutoka nje.
 
nimeelewa kwa mbali sana hasa hapo kwenye currency devaluation, plz one more lecture!
 
Ile kampuni iliyokuwa inachapisha ya kule Uingereza ya Tomas de la Rue itakuwa na datas za kutosha, na ndio kampuni pekee duniani yenye wataalamu wa kutengeneza noti bandia.

Mkuu tiririka vizuri kitaalamu basi ,kwani inauhusiano gani na kima cha chini cha mshahara, na inakuwaje kuchapisha noti mpya kushushe thamani ya shilingi? Naomba kuelimishwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…