Mkuu tiririka vizuri kitaalamu basi ,kwani inauhusiano gani na kima cha chini cha mshahara, na inakuwaje kuchapisha noti mpya kushushe thamani ya shilingi? Naomba kuelimishwa!
- Kima cha chini cha mshahara ndiyo kiwango cha chini kabisa ambacho serikali inakisia kinamtosha mfanyakazi au raia mwingine yeyote wake aishi ndani ya mwezi au muda ulioaniashwa. Sina uhakika sana na kiwango halisi cha sasa, lakini kwa uelewa wangu ni 175,000 tshs. Sasa kwa mfumo wa wa kuwa na noti ya laki moja,,hawa mabwana watapewa noti mbili,,na chenji watatakiwa kurudisha,,hii itawasababishia wenye pato la ina hiyo kushindwa kununua vitu au huduma nyingi zaidi, sababu bei ya vitu nayo ni lazima ipande,,pale tu utakapoitoa hiyo noti ya laki moja. LAZIMA
Sasa kima cha chini ndivyo kinavyohusika,,kwenye makadirio ya mtu kuweza kukidhi mahitaji muhimu wa binadamu.
Lakini kima cha chini sio tatizo la msingi kwenye kuchapisha noti ya laki moja. Tatizo ni kupanda kwa bei ya vitu na huduma. Upandaji huu wa bei ya vitu kwa nchi ambayo haitengenezi hata kiberiti chake yenyewe,,kutasababisha tuongeze idadi ya vitu tunavyoagiza kutoka nje ya nchi( imports).
Sasa kwa nchi yetu ambayo kwa sasa tu thamani ya bidhaa iingizwayo nchini ( mostly used products) ni kubwa kuliko bidhaa zitokazo nchini( natural unused rare products) halafu unataka uongeze hilo gap liwe kubwa zaidi,,,
,maskini watashindwa hata kununua chumvi itakuwa hatari.
Kikubwa ni upandaji bei wa vitu,,utakaoshusha zaidi thamani ya fedha yetu,,na kusababisha tuhitaji dollar zaidi ili tuweze kununua hizo imports zaidi,,,hizo dollar tunatoa wapi?? tunauza natural resources zetu zaidi na zaidi..
Sasa ukiangalia faida ya kuwa na noti ya laki moja labda kwa ajili ya wallet,,sababu kweli siku hizi kukunja wallet haiwezekani kama una kilaki tano tu mfukoni.
cha muhimu ni kwenda na wakati,,kuboresha IT na matumizi ya card na m-pesa au huduma za staili hiyo zaidi,,ili pesa isibebebebwe nyingi sana kwa wakati mmoja na vile vile watu na serikali iweze kutrace matumizi na kodi yake inayopata vizuri zaidi.
Kuna mathara mengi ya kuwa na hiyo noti ya laki moja,,nadhani wengine watakunyunyizia zaidi.