Tanzania tunahitaji Rais ambae ni Mwanasiasa Bora au Mzalendo?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF ,Kiuhalisia unapozungumzia sifa NZURI za kiongozi hasa kwa Ngazi ya Urais huwa Hatuna kiongozi Bora ila tuna Mwanasiasa Bora au Kiongozi Mzalendo.

Kiongozi bora maana yake ni Mwanasiasa Bora na ni Mzalendo pia kupata mtu mwenye sifa hizi Mbili ni Ngumu sana kwa hiyo ni either utapata Mwanasisa bora au Kiongozi Mzalendo kwa upande wa sifa Nzuri za kiongozi wa Nchi.

Mwanasiasa Bora ni kama Kina Rais mstaafu Jakaya na Mwenyekiti wa CHADEMA mbowe hawa wenyewe hashughulika za katika kuweka mazingira ya Kuonekana kuna Usawa na Uhuru hata kama Hakuna ,mwananchi au kiongozi akilalamika inatafutwa tu namna ya Kutuliza hilo Jambo Maisha yanaendelea .Kwa kifupi ni watu wanaocheza na Akili za watu tu.

Kiongozi Mzalendo hawa wenyewe huangalia Maslahi ya Nchi tu kwa kutatua kero za Wananchi bila kujali nani anaumia kikubwa Nchi kwanza ,wako Tayari kufunga midomo watu kwa ajili ya maslahi ya Taifa .Mifano Yao ni kama Hayati Nyerere ,Hayati JPM na Putin.

Ukimsikiliza hapa JPM anakiri kabisa yeye sio Mwanasiasa Mzuri.

Kwa Maelezo hayo je Tunahitaji Mwanasiasa Bora au Kiongozi Mzalendo ?
 
..Tunahita KATIBA MPYA NA BORA.

..Katiba itakayopunguza madaraka ya Raisi.

..Katiba itakayolipa BUNGE mamlaka ya kuisimamia serikali kikamilifu.

..Katiba itakayosimika uhuru wa MAHAKAMA ktk kutafsiri sheria na kutoa haki.

..Katiba itakayotuwezesha Watanzania kuwawajibisha viongozi wetu kupitia sanduku la KURA.
 
Bado tuendelee kuamini CCM kutuletea katiba mpya ?
 
..huwezi kuwakabidhi Ccm, Cdm,Act, etc halafu uka-relax kusubiri katiba mpya.

..lazima kuwe na MSUKUMO wa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa mchakato wa wazi, na kuzingatiwa kwa mawazo ya wananchi.
 
Hakika
 
Ukijuakutofautisha siasa na maendeleo basi utajua ni Rais gan wananchi wanamtaka. Niaonavyo mimi wanasiasa hawapendi kabisa Rais anashugulika na kero za wananchi wanahisi watakosa agenda kipindi cha kampeni. Kwa wananchi wao ni case tofauti.
 
Ungetupa kwanza maana ya uzalendo ni nini mana ni ngumu kuwatambua kuna viongozi wanaigiza uzalendo
 
Mimi naamini hivyo. Tukiwa na Katiba bora, ambapo mihimili yote mikuu iko huru kiutendaji lakini inategemeana, mfano rahisi tu tusingekuwa na wale wabunge 19.
Mbona hata katiba tuliyo nayo haifuatwi hiyo mpya itafuatwa ?
 
Ukijuakutofautisha siasa na maendeleo basi utajua ni Rais gan wananchi wanamtaka. Niaonavyo mimi wanasiasa hawapendi kabisa Rais anashugulika na kero za wananchi wanahisi watakosa agenda kipindi cha kampeni. Kwa wananchi wao ni case tofauti.
Uko sawa
 
..huwezi kuwakabidhi Ccm, Cdm,Act, etc halafu uka-relax kusubiri katiba mpya.

..lazima kuwe na MSUKUMO wa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa mchakato wa wazi, na kuzingatiwa kwa mawazo ya wananchi.
Msukumo kama Upi ?
 
Mbona hata katiba tuliyo nayo haifuatwi hiyo mpya itafuatwa ?

..Katiba iliyopo haifuatwi kwasababu imetoa MIANYA ya kutofuatwa.

..Katiba mpya itakuja kuziba mianya hiyo, na kutengeneza utaratibu mzuri wa kushughulikia wavunja katiba.

..Katiba ikitokana na WANANCHI kutakuwa na hamasa ya kuilinda na kuhakikisha viongozi wanaiheshimu.
 
  • Thanks
Reactions: RNA
Mpaka hapa tulipofikia, nadhani kama Taifa tunahitaji mfumo imara, na utakaojengwa kupitia katiba bora (Katiba ya Wananchi).

Kwa sasa hatuhitaji tena Rais Mwanasiasa au Rais Mzalendo! Maana hao wote hutekwa kirahisi na makundi mabaya na yenye maslahi binafsi kupitia mfumo dhaifu uliopo sasa.
 
..Katiba iliyopo haifuatwi kwasababu imetoa MIANYA ya kutofuatwa.

..Katiba mpya itakuja kuziba mianya hiyo, na kutengeneza utaratibu mzuri wa kushughulikia wavunja katiba.

..Katiba ikitokana na WANANCHI kutakuwa na hamasa ya kuilinda na kuhakikisha viongozi wanaiheshimu.
Sawa
 
Back
Top Bottom