Habari JF ,Kiuhalisia unapozungumzia sifa NZURI za kiongozi hasa kwa Ngazi ya Urais huwa Hatuna kiongozi Bora ila tuna Mwanasiasa Bora au Kiongozi Mzalendo.
Kiongozi bora maana yake ni Mwanasiasa Bora na ni Mzalendo pia kupata mtu mwenye sifa hizi Mbili ni Ngumu sana kwa hiyo ni either utapata Mwanasisa bora au Kiongozi Mzalendo kwa upande wa sifa Nzuri za kiongozi wa Nchi.
Mwanasiasa Bora ni kama Kina Rais mstaafu Jakaya na Mwenyekiti wa CHADEMA mbowe hawa wenyewe hashughulika za katika kuweka mazingira ya Kuonekana kuna Usawa na Uhuru hata kama Hakuna ,mwananchi au kiongozi akilalamika inatafutwa tu namna ya Kutuliza hilo Jambo Maisha yanaendelea .Kwa kifupi ni watu wanaocheza na Akili za watu tu.
Kiongozi Mzalendo hawa wenyewe huangalia Maslahi ya Nchi tu kwa kutatua kero za Wananchi bila kujali nani anaumia kikubwa Nchi kwanza ,wako Tayari kufunga midomo watu kwa ajili ya maslahi ya Taifa .Mifano Yao ni kama Hayati Nyerere ,Hayati JPM na Putin.
Ukimsikiliza hapa JPM anakiri kabisa yeye sio Mwanasiasa Mzuri.
Your browser is not able to display this video.
Kwa Maelezo hayo je Tunahitaji Mwanasiasa Bora au Kiongozi Mzalendo ?
Mimi naamini hivyo. Tukiwa na Katiba bora, ambapo mihimili yote mikuu iko huru kiutendaji lakini inategemeana, mfano rahisi tu tusingekuwa na wale wabunge 19.
Ukijuakutofautisha siasa na maendeleo basi utajua ni Rais gan wananchi wanamtaka. Niaonavyo mimi wanasiasa hawapendi kabisa Rais anashugulika na kero za wananchi wanahisi watakosa agenda kipindi cha kampeni. Kwa wananchi wao ni case tofauti.

Mpaka hapa tulipofikia, nadhani kama Taifa tunahitaji mfumo imara, na utakaojengwa kupitia katiba bora (Katiba ya Wananchi).
Kwa sasa hatuhitaji tena Rais Mwanasiasa au Rais Mzalendo! Maana hao wote hutekwa kirahisi na makundi mabaya na yenye maslahi binafsi kupitia mfumo dhaifu uliopo sasa.