Tanzania tunahitaji shopping malls?

Tanzania tunahitaji shopping malls?

Kuna mtu alisema dunia ilipofikia/inapoelekea sasa hivi siyo tena muda wa kujivunia kuwa na malls nyingi maana siku hizi habari ya mjini ni online shopping.
Lakini kwa nchi kama yetu online shopping/business inawahitaji wenye hizo biashara wawe waaminifu. Kwa bongo online business inafeli hapo tu...
 
Umuhimu wa malls ni kuwa “one-stop shopping centre”. Maduka ya bidhaa za kila fani na aina zinapatikana pahala pamoja na hivyo kumuondolea mteja adha ya kuzunguka mjini kutafuta bidhaa tofauti tofauti.

Malls ni muhimu sana mijini kadiri “urbanisation” inavyoongezeka. Gharama ya kuzunguka mjini ni tatizo linalohitaji ufumbuzi. Yawezekana baadaye online shopping ikalimaliza lakini face to face interaction bado ni muhimu kwa binadamu. Aidha, malls vile vile ni sehemu za outing, burudani, rendezvous, “viwanja”, nk.

Kwa vijiji na vitongoji vyetu sidhani; magenge, fremu, na mini-shopping centres zinatosha. Unatembelea ndugu sehemu sehemu wanachemsha maji kisha wanamtuma mtoto dukani anunue vijiko vinne vya sukari na viwili vya majani ya chai!
 
Hii nayo ni point nzuri sana. Online shopping inakuja kwa kasi. Haya ma Mall yatakuwa hayana maana tena.
Yeah siku hizi kuna Amazon, Aliexpress, Kikuu, Jumia, eBay et al ushindwe wewe tu. Dunia inaenda kasi sana.
 
Lakini kwa nchi kama yetu online shopping/business inawahitaji wenye hizo biashara wawe waaminifu. Kwa bongo online business inafeli hapo tu...
Yeah uaminifu ndiyo shida. Lakini laiti tungelikuwa waaminifu online shopping is bae.
 
Hii nayo ni point nzuri sana. Online shopping inakuja kwa kasi. Haya ma Mall yatakuwa hayana maana tena.
mnachekesha sana mnaosema online shopping ni bora kuliko malls

kwa uelewa wangu mdogo tu naamini ya kwamba online shopping inahitaji uelewa mpana, inahitaji smart phone, inahitaji uwe na bando pia inahitaji ujue zile site ambazo unaweza ukafanya manunuzi

wakati shopping mall ukijua tu kuwa lile ni jengo la shopping mall unaenda tu kupata mahitaji yako

sasa hapo ni kipi bora? Tuwe na Malls au watu wanunue mahitaji mtandaoni?

watanzania wangapi wenye smartphone? watanzania wangapi wanajua site za kufanya manunuzi? Watanzania wangapi wana uwezo wa kuweka bando? watanzania wangapi wanajua matumizi ya mitandao zaid ya kutumia fb & instagram?

kwaiyo online shopping haiwezi kuvunja soko la Malls
 
Hata huko kwenye mall wanaweza kuweka kitengo cha online shopping kwa kuweka bidhaa kwenye mtandao mtu akipenda anapelekewa.
online shopping hata kwa bwana mangi unafanya tu

kwani tafsiri halis ya lipa kwa Mpesa au lipa kwa tigo pesa ni kitu gani?

inshort online shopping ni kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao ,

sasa unapoambiwa lipa kwa tigo pesa nayo si ni online shopping jaman?
 
Dah sipendi kwenda shopping malls sababu Kila mtu kapaki gari lake Sasa kweli ninunue halafu yenyewe huwa yapo mbali na daladala nianze kubeba viroba hapana ngoja niende tu sokoni na kiroba changu hakuna atanishangaa....dah kukosa gari unaishi kinyonge jameni hata bar nzuri unaona aibu kwenda...unaishia za mtaani tu.
 
Back
Top Bottom