Umuhimu wa malls ni kuwa “one-stop shopping centre”. Maduka ya bidhaa za kila fani na aina zinapatikana pahala pamoja na hivyo kumuondolea mteja adha ya kuzunguka mjini kutafuta bidhaa tofauti tofauti.
Malls ni muhimu sana mijini kadiri “urbanisation” inavyoongezeka. Gharama ya kuzunguka mjini ni tatizo linalohitaji ufumbuzi. Yawezekana baadaye online shopping ikalimaliza lakini face to face interaction bado ni muhimu kwa binadamu. Aidha, malls vile vile ni sehemu za outing, burudani, rendezvous, “viwanja”, nk.
Kwa vijiji na vitongoji vyetu sidhani; magenge, fremu, na mini-shopping centres zinatosha. Unatembelea ndugu sehemu sehemu wanachemsha maji kisha wanamtuma mtoto dukani anunue vijiko vinne vya sukari na viwili vya majani ya chai!