Tanzania tunakwama wapi? Inakuaje tunazidiwa na Nchi zote za Afrika Mashariki kwenye Miundombinu bora ya Barabara?

Tanzania tunakwama wapi? Inakuaje tunazidiwa na Nchi zote za Afrika Mashariki kwenye Miundombinu bora ya Barabara?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Kazi iendelee!

Ni jambo la kushangaza kwamba Tanzania tunazidiwa na Nchi zote za Afrika Mashariki kwa mtandao na ubora Wa barabara isipokuwa Burundi.

Hivi kama Nchi hatuna dira,malengo na mkakati wa kutekeleza kwenye kila sekta Ili tupate ufanisi? Inakuaje kila kitu tuko nyuma? Tena tunazidiwa na Vinchi masikio kama Rwanda na Uganda?

Lazima kuna tatizo mahala maana haiwezekani kila kitu cha kutumia akili zetu sisi ni WA mwisho isipokuwa vitu vilivyowekwa na nature tuu.

Wakati tunajipiga kifua kwenye flyovers na madaraja ya suspension bridge kama la Kigongo-Busisi ,huko Jinja Uganda vipo siku nyingi Sana.

Screenshot_20220112-162107.png

Screenshot_20211214-210856.png

Screenshot_20211216-062345.png
 
Umeelezea vema,tunaishi nchi ya sifia sifia tu,wataalaam wetu wote wameokotwa jalalani,kituko cha RPC Dodoma eti ataanza to escort buses zinapoingia mkoani kwake!ni kichekesho kitupu,we need to be serious hapa hii T1 ni uchafu mtupu hasa Mbeya to Tunduma,Dar to Mikumi ,hii barabara inabidi tuijenge upya sio kuitia viraka!life span ya barabara hii imeshapitwa na wakati,hii barabara imejengwa Nyerere era,inabidi tuipanue hasa pale Mikumi National park ikiwa ni pamoja na kusafisha vichaka vyote 20m both sides (faida yake tutapunguza wanyama wadogo kuwa maeneo karibu na barabara),Kitonga Pass tuweke njia mbili pale,Chimala to Mbeya papanuliwe na njia hii ichepushwe isipite katikati ya Mbeya.Natamani waziri wangu wa mawasiliano afanye utalii wa kikazi kwa barabara,aanzie N1 from Beitbridge to cape town,then N7 from Cape town to Namibia border,pale achukue B1 to windhoek,then aruke kwa ndege to Gaborone pale akamate A1,A2 na A3 towards kazungula,definitely akirudi Dar ataona tofauti kubwa kati yao na sisi.
 
Kazi iendelee!

Ni jambo la kushangaza kwamba Tanzania tunazidiwa na Nchi zote za Afrika Mashariki kwa mtandao na ubora Wa barabara isipokuwa Burundi.

Hivi kama Nchi hatuna dira,malengo na mkakati wa kutekeleza kwenye kila sekta Ili tupate ufanisi? Inakuaje kila kitu tuko nyuma? Tena tunazidiwa na Vinchi masikio kama Rwanda na Uganda?

Lazima kuna tatizo mahala maana haiwezekani kila kitu cha kutumia akili zetu sisi ni WA mwisho isipokuwa vitu vilivyowekwa na nature tuu.

Wakati tunajipiga kifua kwenye flyovers na madaraja ya suspension bridge kama la Kigongo-Busisi ,huko Jinja Uganda vipo siku nyingi Sana.

View attachment 2086670

View attachment 2086671

View attachment 2086672
Sasa hata Burundi, japo mtandao wao wa barabara ni mdogo lakini barabara zilizopo ni nzuri kweli, hata nyumba zao...quality

Nchi hii iliharibiwa na "zidumu fikra za mwenyekiti"...katika mambo Mzee wetu Nyerere alifeli ni vile kutaka sifa kama Jiwe
 
Sasa hata Burundi, japo mtandao wao wa barabara ni mdogo lakini barabara zao zile zilizopo nzuri kweli, hata nyumba zao...quality

Nchi hii iliharibiwa na "zidumu fikra za mwenyekiti"...katika mambo Mzee wetu Nyerere alifeli ni vile kutaka sifa kama Jiwe
Hi nchi yetu ni kubwa sana ukilinganisha na hizo nchi. Utakuta huzi tulizojenga kwa uchache wake zitaenea eneo kubwa la hizo nchi. Bado tuendelee kuikumbusha Serikali watimize wajibu wao
 
hakuna lolote hapo, nchi za kiafrika hizi hizi et namibia 23 kidunia? labda kama kuna vigezo walivyo viweka na hivyo vigezo tungeviomba tuvione... ili tuangalie nchi kama USA, EU yote, Dubai, Qatar kwenye kombe la dunia, oman, kuwait, japan, china, S.korea, Malyasia, Singapore, Indonesia, Canada... ili tujue imefikaje 23? kwa kukopa? misaada? nk...

ili tujitafakali vizuri...
 
Sasa hata Burundi, japo mtandao wao wa barabara ni mdogo lakini barabara zao zile zilizopo nzuri kweli, hata nyumba zao...quality

Nchi hii iliharibiwa na "zidumu fikra za mwenyekiti"...katika mambo Mzee wetu Nyerere alifeli ni vile kutaka sifa kama Jiwe
Hii Nchi yetu ina watu tuna midomo Sana ila matumizi ya akili na vitendo ni hamna kabisa.

Hizo Nchi ukiacha udogo wao zimekuwa na matatizo ya kiusalama kiaka na miaka sisi tuna Amani lakini hakuna cha maana tumefanya.
 
Hadi senegal imetushinda? Huu ni uwongo!
Senegal unaisikia mitandaoni tuu ila hakuna kitu tumewazidi .

Kwenye Barabara wako mbali sana yaani hata Bukina faso hatuwagusi.

Hivi huoni aibu eti miaka hii ndio tunahangaika na fly over na barabara ya njia Sita wakati hapo Uganda zipo kitambo tuu? Huko Senegal ndio usiseme.

Barabara zenyewe bado tunajenga za grade ya chini Sana ,wenzetu walishahama huko.

Dakar roads 👇

Screenshot_20220118-200237.png

Screenshot_20220118-200156.png

Screenshot_20220118-200054.png
 
Senegal unaisikia mitandaoni tuu ila hakuna kitu tumewazidi .

Kwenye Barabara wako mbali sana yaani hata Bukina faso hatuwagusi.

Hivi huoni aibu eti miaka hii ndio tunahangaika na fly over na barabara ya njia Sita wakati hapo Uganda zipo kitambo tuu? Huko Senegal ndio usiseme.
Sisi hata Barabara za kawaida tu zinadumu kwa mwaka mmoja, na zinazinduliwa kwa mbwembwe na kulazimisha watu waache kazi zao na kukusanyika kushangilia
 
Sisi hata Barabara za kawaida tu zinadumu kwa mwaka mmoja, na zinazinduliwa kwa mbwembwe na kulazimisha watu waache kazi zao na kukusanyika kushangilia
Ni kweli mkuu afu hata hazivutii,zinalipuliwa yaani hazina viwango sijui hii Nchi ina shida gani kiukweli.
 
Back
Top Bottom