Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
Kwa huu ufisadi wa mawaziri na watendaji wengine unaoendelea nchini, ningekuwa Rais ningeukomesha ndani ya siku 100 za mwanzo katika uongozi wangu. Ningetunga sheria ya ufisadi na uhujumu uchumi ambayo ufisadi unaozidi mabilion adhabu yake ni kifo.
Kwamba kesi za namna hiyo sheria itaweka wazi kuwa zisikilizwe ndani ya siku 18 hii ni pamoja na rufaa. Baada ya hukumu ya mwisho mfungwa anapaswa kunyongwa ndani ya saa 48.
Kwamba vyombo vya habari vitaruhusiwa kurusha moja kwa moja mwenendo mzima wa kesi ili kuwapa nafasi wananchi kufuatili kesi ya mwizi wao na hukumu atakayopewa.
Kutakuwa na eneo maalumu pale Dodoma ambalo litatengwa kwa ajili ya kuzika mafisadi. Makaburi yao yataandikwa majina yao na kiasi cha ufisadi alioufanya. Hii ni kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi na wananchi watakaotembelea makaburi hayo kwa ajili ya kutalii.
Kwamba mkuu wa magereza Tanzania CGP atapewa mamlaka na sheria kunyonga wafungwa wa ufisadi na uhujumu uchumi ndani ya saa 48 tangu hukumu ya mwisho kutolewa kama mhusila alikata rufaa. Wala haitasubiri Rais kusaini.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
====
Pia soma:
- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
- Luhaga Mpina: Waziri Bashe na Mwigulu walitengeneza uhaba wa sukari nchini, zilikuwa njama za kuiba mapato ya nchi