Tanzania tunge-host Formula 1 kwa mara ya kwanza

Tanzania tunge-host Formula 1 kwa mara ya kwanza

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Tanzania bara na (au) visiwani tulikua katika moja ya nchi za Africa zilizopendekezwa au zilizofikiriwa kuhost Grand Prix.

Ikumbukwe kwa Africa ni South Africa tu waliwahi host F1 GP, first time ilikua 1934 na last time ilikua 1993.

Lewis Hamilton, amewahi sikika akisema ktk moja ya interview yake anatamani sana angeendesha F1 katika bara la Africa.

Zanzibar:

By 2027 tunategemea first F1 ikafanyika hapo visiwani. Tayari pesa ishatengwa na MoU ishasainiwa uko Italy baina ya serikali ya Zanzibar (kupitia ZIPA - Zanzibar Investment Promotion Agencies na F1 organizer & stakeholders (hawakutaja exactly majina)).
images (33).jpeg

(Hii ilitengenezwa na fans katika moja ya forums za F1, sio official)

Race track itakua ni closed sio street circuit, na imetengewa eneo la square kilometa 2.5 uko Zanzibar. Ujenzi utaanza 2025 na by 2027 utaisha. Kama itakua tayari imemeet vigezo vya FIA Grade 1 standard, kuna uwezekano tukaenda kusikiliza 1.6 V6 Hybrid engine hapo visiwani. What a wonderful time to be alive.

Tanzania

Bara hatuna chance kubwa sana. Na kama ipo tunategemea itakua street circuit sio closed. Sema serikali yetu kwenye michezo ya racing tupo nyuma sana.

Proposed circuit hii hapa iitwe Oysterbay Grand Prix

images (34).jpeg

Itakua na urefu wa 4.45 kilometa, laps zikipigwa 57 inakua race distance 255 km.

images (35).jpeg


Hii google map yake inavyoonesha.

Faida:

Itaongeza utalii, mapato, pesa, heshima, na watanzaia tuta enjoy.

Bei ya chini kabisa kuingia kwenye mashindano ya F1 ni $200 kwa siku tatu (Fri, Sat & Sun) lakini sisi masikini tutakaa nje kwa mbali tusikie mlio wa V6 hybrid engine.

Dah
 
Kama Safari Rally kuandaa miaka hii ambapo michezo inapewa kipaumbele ni ngumu.

Wenzetu wa Kenya kuandaa Safari Rally kumewafanyq wapate nafasi ya kuandaa World Rally Champion (WRC) miaka karibia 3 na mpaka wakapenyeza wakenya kwenye kamati za mashindano
 
Mwezi uliopita niliona Kenya kunafanyika mashindano ya rally yakirushwa LIVE kupitia DStv hawa wenzetu wakenya wajitambua sana maana yale mashindano yalifanyika kwenye mbuga za wanyama
hiyo rally nilikuwa naicheki live kupitia dstv huko naivasha kwenye mbuga ya hell's gate . Kenya wapo njema sana kwenye hu host haya mashindano. Una enjoy zile drift skills za madereva hadi raha
 
Kiingilio $200 najiuliza tu wabongo tutalipia kweli...... halafu tunalipiaje wakati ni mtaani tu. Ukipanda ghorofa unaona laivu😆😆.

Hata hivyo kwa mashindano ya mbio kutazama kwenye TV unapata picha kubwa zaidi ya kukaa sehemu moja tu unasikilizia vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuumFyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu kameshapita heeeh!!🤯
 
Kiingilio $200 najiuliza tu wabongo tutalipia kweli...... halafu tunalipiaje wakati ni mtaani tu. Ukipanda ghorofa unaona laivu😆😆.

Hata hivyo kwa mashindano ya mbio kutazama kwenye TV unapata picha kubwa zaidi ya kukaa sehemu moja tu unasikilizia vuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuumFyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu kameshapita heeeh!!🤯
Hahahaha ilo nalo neno. Kweli mtu atoe laki 5 kisa race ya saa 1. Hafu vigari vinapita kama upepo.
 
Back
Top Bottom