Tanzania tutumie njia hii tufanikiwe kwa Soka la kimataifa

Tanzania tutumie njia hii tufanikiwe kwa Soka la kimataifa

CodeX

Member
Joined
Sep 2, 2018
Posts
27
Reaction score
200
Kwanza naanza kusema Tanzania tuna vipaji vingi sana wa michezo mbalimbali vinavyokosa rutuba ya kuendelezwa ama kwa sera mbovu za mchezo au ukosefu wa kimkakati!

Sasa kama wote tunapenda na kuumia na matokeo ya soka letu basi kwanini tusiwekeze?! Majuzi tumetumia zaidi ya bilioni moja kuandaa mashindano ya AFCON U17. Ni pesa nyingi sana ila tulikubali kwa sababu wote tunapenda michezo na soka ni mchezo pendwa wa watanzania wengi.

.
Nini tufanye sasa? ??!!

Tukubali kupeleka vijana wetu katika Academies bora za Ulaya na tukifanya hivi tutaweza kukaribia furaha kama za wenzetu. Hata kama hatutaki wenzetu wa Afrika magharibi wanafanya hivi sana.
.

Mfano pale Southampton tukapeleka wawili, Leicester wawili, Napoli labda watatu, Beskitas labda wanne nk. Tukiwa na vijana kama 30 katika academies mbalimbali hawatuwezi kutuangusha huko mbeleni.
.

Yes, mpira ni fani kama fani zingine zinazopelekwa kisasa sana katika karne hii ya 21, sasa kama tunapeleka kusomesha watu kusomea uchimbaji wa mafuta ghafi na bado hatujaanza kuchimba kwanini tusipeleke vijana wetu wakajifunze mpira wa kisasa ili baadae watutoe kimasomaso.


.

Mwisho. Serikali ndio iwe mdau mkubwa kwa hili.
 

Attachments

  • IMG-20190628-WA0011.jpeg
    IMG-20190628-WA0011.jpeg
    17.7 KB · Views: 11
Back
Top Bottom