Tanzania tuwe na bunge la senate

MNYISANZU

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
7,046
Reaction score
1,102
Ni kama kutakuwa na serikali tatu. Tuwe na bunge la senate badala ya bunge la muungano. Kila mkoa kwa Tanganyika na wilaya kwa upande wa Zanzibar achaguliwe senata mmoja .

Bunge la senate liwe na mamlaka ya;

1. Debate and approve bills and trieties,

2. Consider and determine the resolution impeachement of the president and his/her vice president,

3. To represent the regional/district interests at the national level ,

4.To consider and determine the national revenue distribution at the regional levels and, 5. To review and provide advice on presidential appointments and nominations.

Je wewe una maoni gani?
 
Also to probe and check the administration of laws in Tanzania.
 
Na Kila Senata awe ni mwenye asili na mkoa husika tushawachoka kina rage waeleweke kabisa ni masenata wa Somalia na India... ila ni wakazi... tupunguze wachaga bungeni.... hili ni Tatizo maana kuwa na Utawala kama huu jamii fulani ni Wezi na hawapendi maendeleo ya nchi wao ni kuweka mikakati mizuri na ukifka wakati wa utekelezaji pesa haionekani wameichukua yote... hii kitu inahitajika sana ili mikoa yote iendelee tushachoka kuambiwa Dar ndio inakusanya kodi 80% na mikoa mingine kwa pamoja ikiwemo unguja na pemba 20% yaani ni malumbano tu
 
Una element hatari sana za ubaguzi. Ni vizuri kama utajadili powers, composition and other related issues about senatorial parliament.
 
Una element hatari sana za ubaguzi. Ni vizuri kama utajadili powers, composition and other related issues about senatorial parliament.
Basi tuendee hivi hivi no need to change maana vya wenzako unaona havifai... wa Mtwara wanataka maendeleo na wa Rukwa vile vile.... mnawaza madaraka na si maendeleo...
 
Basi tuendee hivi hivi no need to change maana vya wenzako unaona havifai... wa Mtwara wanataka maendeleo na wa Rukwa vile vile.... mnawaza madaraka na si maendeleo...
Hoja iliyopo hapa mezani inahusu bunge la senate. Hayo mengine yafungulie thread yake.
 

WaTz watu wa ajabu! Mkiitwa janja ya NYANI mnanuna! Kifungu cha kwanza cha Rasimu ya Katiba Mpya kinasema kuwa: "Tanzania ni Jamhuri ya Shirikisho la Tanganyika na Zanzibar" Kituko kinaanzia hapa. Senate iko Marekani kwenye Shirikisho mnalolitaka.Lakini shirikisho lenu mnaliita Jamhuri halina serikali za majimbo, ni nchi moja yenye utawala mmoja tu.


Au labda Zanzibar ndiyo inasababisha tuite shirikisho.Hamwoni mfumo halisi wa Shrikisho na Mfumo halisi wa Jamhuri haiwezi kuendesheka pamoja isipokuwa kwa watu wababaishaji? Kama huoni mbali basi nchi yako ni Jamhuri na Bunge la pili linalotakiwa ni la maMwinyi kama Uingereza. Swali ni je tunao watu wanaostahili kuingia katika Bunge la maMwinyi? Tukimpeleka huko Mzee wetu Rukhsa tutaishia kumaliza mali asili ya nchi kwa kuruhusu kila mtu kuchukua kila kitu kama Kunguru hata akiitwa JANGILI au FISADI. Ni Nyerere tu ndiye angekuwa Candidate wa Bunge la maMwinyi, lakini, Duh! WaTz ukiwambia anakuja Rais anayetaka kuzuia dhahabu, gesi na mafuta visiibiwe wanaingia vichakani kumlisha sumu mpaka eti afe.Huwezi amini mpaka uwakute wakipanga uongo huo.Nyerere angekuwa na akili ya ujinga mlionao sasa dhahabu yote na gesi mngeikuta?


Na hapo ndipo unapokuja na Zanzibar iwe na maSenator kutoka kila Wilaya, Bara watoke Mikoani ili kuenzi Jamhuri yao. Kisa hutaki Zanzibar ikawa na majimbo kumi na Tanganyika Majimbo 250 kwa sababu Zanzibar itamezwa. Amua Shirikisho kama la Marekani au Jamhuri ya Kifalme kama Uingereza, vyote kwa pamoja ni utatanishi wa kuleta kero kwa wananchi wa Tanzania.Vinginevyo WaZenj wawe na Bunge lao linalolipwa na WaZenj, na Bara wawe na Bunge lao linalolipwa na Bara. Tusibebeshane mizigo kiujanja ujanja. Bunge la Jamhuri liwe Mkutano wa Mabunge Mawili haya kuamua mambo ya "Mutual Interest" basi. Vikao vya Bunge la Jamhuri vikae wakati wa kujadili "Mutual Interests" tu na kama kukitokea kutofautiana katika pande 2 za Muungano. Hatuwezi kuhukumu watu milioni 40 wa Bara kwa kura za watu milioni 1 wa Zenj eti tujulikane ni washiriki wa nguvu sawa katika shirikisho. Na Bunge la Jamhuri linapokutana WaZenj walipe gharama za vikao husika kwa kila kichwa cha Mbunge waZanzibar ndani ya Bunge hilo kutetea maslahi ya nchi yao.


Si vizuri kuwapunja lakini pia si hekima kuwalipia gharama, huo uhusiano hautakiwa katika nchi 2 zinazofanya shirkisho. Wapeni uhuru wazenj kuleta idadi wanayodhani itatosha kupima nguvu zao Bara lakini wajue kugharamia uwakilishi wao.
 
Mkishashindwa kuaminiana basi kunakuwa hakuna haja ya kuwa na taasisi zenye kuongeza gharama katika maisha ya wananchi bila tija yoyote. Kuwepo kwa serikali tatu itakuwa ni dalili fika sana ya kusindwa kuaminiana na ni afadhali kabisa kuvunja muungano huo ili kila sehemu ijue jinsi ya kujiendesha. Baada ya miaka zaidi ya arobaini ya Muungano nilitegemea mawazo ya kuunda serikali moja na kuanzishwa kwa tasisi zinazotunchanganya zaidi badala ya kusistiza taasisi zinazotutengenisha zaidi.
 
Mnyisanzu, mimi nina swali moja tu. Je Hao wajumbe wa Baraza la Seneti wanachaguliwa na nani? Na kwa kutumia vigezo gani? Pili, kama watakuwa wanachaguliwa na wananchi, ni nini itakuwa hatima ya siasa za Tanzania? Hebu fikiria: Una Executive Branch (Raisi wa nchi ambaye anachaguliwa na wananchi), utakuwa na two legislative Bodies (Ambazo zote zinachaguliwa na wananchi) Hello U.S Politics!!!! Je, unadhani kwamba hii nchi kweli itatawalika? Bear in mind kwamba, hadi leo hii, 52 years after Independence hakuna hata institution moja (Executive Branch, Legislative na Judiciary) ipo accountable kwa wananchi. Je ukiongeza the 3rd and elected institution siitakuwa majanga? :A S 39:
 

Wee Kichuguu vipi?!

Huwajui WaZenj wewe. Hapa swala la kuaminiana hakuna. Julius alikubali wawe na Serikali yao ili wajifunze kuwa nia ya Bara ilikuwa ni safi. Baadaye wakapewa na Urais wa Jamhuri, badala ya kuona kuaminiana ndani yake akaja Bwana Mkubwa kutawala Bara, na akasema hivyo. Na alipokuwa madarakani Bwana Mwinyi kulikuwa na mpaka maneno kama "Kunhguru wa Zanzibar na Panya wa Zanzibar" lakini yakihusu tabia ya Wazanzibar katika uchumi wa Bara. Hata Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar iligharimu mara sitini zaidi ya sherehe za siku zote. Zanziba wakaanza hata kujiita nchi ya kiBiashara, wakaacha kulima Karafuu. Baadaye akatafuta zao la mwani kuficha aibu.

Lakini bado Zenj ao hao ndiyo wana kero zote za Muungano! Wewe utaendelea kumwamini mshirika wa namna hiyo?
 

Nadhani hata wewe unaelewa kwa nini watoto wadogo huambiwa historia kwa hadithi. Wewe nadhani ni mtoto ambaye huyajui na unajaribu kuyaweka jinsi yanavyotakiwa kukaa lakini unashangaa kwa nini yamewashinda hata Wazee. Akilini kwako unadhani hii mizee haina akili, imekomaa na haina uelewa wa mambo, wewe ni "fresh from School" na unataka kuielimisha mikubwa hii. Sikulaumu kwa sababu maisha huwa hivyo. Lakini…………………………………….

Imani ya Mwalimu Nyerere kuwaamini Wazenj haikuwa ndogo. Alikubali Muungano wa Serikali moja kwake na Serikali mbili kwa Wazenj, wasije wakajisikia wamemezwa na Muungano. Wao wakasherehekea ujinga wa Bara. Mwalimu akafikia kuwaalika katika Muungano na kumpa Mwinyi Urais wa Muungano. Hapo ndipo "Ngamia kajihisi ameingia ndani ya hema la Bwana Mkubwa". Mwinyi kwa kauli yake mwenyewe aliwahi kuwaambia BBC kuwa alikuwa amepewa kutawala Bara. Bunge la Bara (la Muungano) likiwa limejazwa Wazanzibari kwa wingi sawa na Bara, likalipuka na hadi lugha ya "Kunguru wa Zanzibar" na "Panya wa Zanziba". Hii yote kuficha lugha halisi kuwa baada ya kupewa Urais Bara waZenj walikuwa sasa wakiiba maliasili ya Bara. Wewe! Ilifikia mpaka akina Njelu Kasaka na G8 wakadai uhuru wa Bara na Wazenj ndiyo waliopinga kufikia kuchaniana mashati Bungeni. Imagine, Bara kudai Uhuru kutoka kwa Wazenj kwa sababu tu Mzenj ndiyo Rais, na WaZenj ndiyo wakapinga Bara kupewa Uhuru! Eti Mwinyi akaenda kuwashitaki akina Kasaka kwa Nyerere ili awakataze badala ya yeye kuelewa kuwa uovu uliokuwa ukipingwa ulikuwa wa Wazenj, aonyeshe uaminifu katika Muungano, lakini wapi!. Kuaminiana kutatoka wapi tena hapo?

Pia wakati wa Mwinyi Zanzibar hao hao walitangaza kuachana na Kilimo cha Karafuu. Zanzibar ikajitangaza imepaa kibiashara na mwaka huo sherehe ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaligharimu mara sitini (60) ya miaka mingine. Kenya hawakubahatika kuwa na mgodi hata mmoja wa dhahabu lakini wakati wa Utawala wa Mwinyi Bunge la Kenya na Kaserikali kao vilitikiswa na magendo ya dhahabu ya Ulyanhulu ambayo ilikuwa inanunuliwa na Wazenj waliokuwa wamesambazwa nchi nzima. Mtu wa Bara kwenda Zanzibar ilikuwa unaonyesha pasi, lakini Mzanzibari kuja Bara alikuwa Mtanzania anayekwenda kwake kwa hiyo hakuna pasi.

Kama Zenj kuna mafuta na Bara yapo, si chini ya bahari? Kisima Bara kikivuta mafuta chini ya bahari Mzanzibar amezuiwa na nani naye kuchimba huko kwake akachota hapo hapo? Kuna sababu ya kulifanya hili kuwa la kupigiwa makelele au ni kutafuta hoja za kubabaisha watu?

Bado unataka kuaminiana na watu wenye tabia hiyo? Mimi sitaki! Kwanza sipendi kuja baadaye kudai Uhuru kwa Zanzibar. Waje kwenye Muungano, wachague wabunge wao wengi iwezekanavyo lakini wawalipe mishahara huko huko na posho za vikao. Sitaki sitaki sitaki hatma ya Watanzania million arobaini kuamuliwa na Wazanzibar million moja kwa lugha ya ujanja ujanja kuwa Wazenj wanamezwa! Hivi milioni arobaini ni muhali kumeza milioni moja? Mbona lugha inabadilishwa kwa uongo kabisa hapa, nani afurahi? Sijakiona ambacho Bara wanakipata kutoka Zanzibar. Badala yake Bara imegeuka kuwa mgawa-fadhila za bure Zenj kuwapa umeme bure na kutuibia dhahabu.
 

Hivyo vyote si vinafanywa na bunge? Kama wabunge wanalala na wa kwenye senator watalala pia. Wewe ungesema nchi iombe itawaliwe tena kwa masharti.
 
Hivyo vyote si vinafanywa na bunge? Kama wabunge wanalala na wa kwenye senator watalala pia. Wewe ungesema nchi iombe itawaliwe tena kwa masharti.

Demokrasia ikishakuwa tu pekee ndiyo kauli ya kuongoza maisha yenu msahau kabisa kuona kila kizuri mnachokitaka. Pateni viongozi mnaowataka muendeshe idara mnazozitaka lakini mkose pia mnavyovitaka kwa sababu idara mlizozitaka hazina namna ya kuwapa vizuri mnavyovitaka. Idara hizo zikiwapa vizuri mnavyovitaka zitakufa na mnaowataka watakosa walivyovipata. Hii ndiyo huitwa mizunguko ya umasikini inayosema: "You are poor because you are poor.".Usiniulize maswali Jogoolashamba kwa sababu nimemaliza fumbo langu na wewe unalielewa linasema nini!
 
Nyie watoto mnahitaji sana kupewa hadithi kwenye choto jioni. Au pia mpewe vitisho vya nyau na zimwi ili mjue kwenda bila kuraise issues zisizowahusu.

Mfumo mzima wa utawala una dosari kubwa. Fikiria mgombea uRais anatimka kwa muda wa wiki tatu kuzunguka nchi nzima kuomba kula kwa watu hata wasiomjua akitoa ahadi lukuki. Mikiki mikiki ni ya kasi kubwa mpaka wengine kuzirai huko huko majimboni.

Haya, mwenzetu akishapata urais anaanza kuwakumbuka waliompeleka Ikulu kwa mapesa yetu sote. ana mamlaka ya kuchota kodi kuwapa wakulima wa pamba kama si wa korosho. Akiwapa machinga wanapiga mayowe. Na baada ya kumchagua huyo huyo hafukuziki Ikulu hata umkamate anaiba heleni za shangazi yako. Wanaoweza kumfukuza ni wenzake alio nao huko mlikowapeleka nyie.

Akishanyamaza huyo kote chini kunaharibika. Polisi wanaua na kupora halafu wanakwenda kungoja aliyeporwa akafungua RB kwao. Ofisi zinaibiwa halafu zinateua Tume ya kuchunguza wizi kutoka miongoni mwa wezi wenyewe.

Halafu Ikulu ni patamu, huyo huyo uliyemchagua kwa kumwona kwa siku moja akipita kuomba kula ndiyo nakutengenezea Katiba.

Kalaga baho ukiomba upewe mabunge KUMI yakusaidie kusimamia SERIKALI wakati Serikali ni ya huyo ALIYEPEWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…