Mkishashindwa kuaminiana basi kunakuwa hakuna haja ya kuwa na taasisi zenye kuongeza gharama katika maisha ya wananchi bila tija yoyote. Kuwepo kwa serikali tatu itakuwa ni dalili fika sana ya kusindwa kuaminiana na ni afadhali kabisa kuvunja muungano huo ili kila sehemu ijue jinsi ya kujiendesha. Baada ya miaka zaidi ya arobaini ya Muungano nilitegemea mawazo ya kuunda serikali moja na kuanzishwa kwa tasisi zinazotunchanganya zaidi badala ya kusistiza taasisi zinazotutengenisha zaidi.
Nadhani hata wewe unaelewa kwa nini watoto wadogo huambiwa historia kwa hadithi. Wewe nadhani ni mtoto ambaye huyajui na unajaribu kuyaweka jinsi yanavyotakiwa kukaa lakini unashangaa kwa nini yamewashinda hata Wazee. Akilini kwako unadhani hii mizee haina akili, imekomaa na haina uelewa wa mambo, wewe ni "fresh from School" na unataka kuielimisha mikubwa hii. Sikulaumu kwa sababu maisha huwa hivyo. Lakini…………………………………….
Imani ya Mwalimu Nyerere kuwaamini Wazenj haikuwa ndogo. Alikubali Muungano wa Serikali moja kwake na Serikali mbili kwa Wazenj, wasije wakajisikia wamemezwa na Muungano. Wao wakasherehekea ujinga wa Bara. Mwalimu akafikia kuwaalika katika Muungano na kumpa Mwinyi Urais wa Muungano. Hapo ndipo "Ngamia kajihisi ameingia ndani ya hema la Bwana Mkubwa". Mwinyi kwa kauli yake mwenyewe aliwahi kuwaambia BBC kuwa alikuwa amepewa kutawala Bara. Bunge la Bara (la Muungano) likiwa limejazwa Wazanzibari kwa wingi sawa na Bara, likalipuka na hadi lugha ya "Kunguru wa Zanzibar" na "Panya wa Zanziba". Hii yote kuficha lugha halisi kuwa baada ya kupewa Urais Bara waZenj walikuwa sasa wakiiba maliasili ya Bara. Wewe! Ilifikia mpaka akina Njelu Kasaka na G8 wakadai uhuru wa Bara na Wazenj ndiyo waliopinga kufikia kuchaniana mashati Bungeni. Imagine, Bara kudai Uhuru kutoka kwa Wazenj kwa sababu tu Mzenj ndiyo Rais, na WaZenj ndiyo wakapinga Bara kupewa Uhuru! Eti Mwinyi akaenda kuwashitaki akina Kasaka kwa Nyerere ili awakataze badala ya yeye kuelewa kuwa uovu uliokuwa ukipingwa ulikuwa wa Wazenj, aonyeshe uaminifu katika Muungano, lakini wapi!. Kuaminiana kutatoka wapi tena hapo?
Pia wakati wa Mwinyi Zanzibar hao hao walitangaza kuachana na Kilimo cha Karafuu. Zanzibar ikajitangaza imepaa kibiashara na mwaka huo sherehe ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaligharimu mara sitini (60) ya miaka mingine. Kenya hawakubahatika kuwa na mgodi hata mmoja wa dhahabu lakini wakati wa Utawala wa Mwinyi Bunge la Kenya na Kaserikali kao vilitikiswa na magendo ya dhahabu ya Ulyanhulu ambayo ilikuwa inanunuliwa na Wazenj waliokuwa wamesambazwa nchi nzima. Mtu wa Bara kwenda Zanzibar ilikuwa unaonyesha pasi, lakini Mzanzibari kuja Bara alikuwa Mtanzania anayekwenda kwake kwa hiyo hakuna pasi.
Kama Zenj kuna mafuta na Bara yapo, si chini ya bahari? Kisima Bara kikivuta mafuta chini ya bahari Mzanzibar amezuiwa na nani naye kuchimba huko kwake akachota hapo hapo? Kuna sababu ya kulifanya hili kuwa la kupigiwa makelele au ni kutafuta hoja za kubabaisha watu?
Bado unataka kuaminiana na watu wenye tabia hiyo? Mimi sitaki! Kwanza sipendi kuja baadaye kudai Uhuru kwa Zanzibar. Waje kwenye Muungano, wachague wabunge wao wengi iwezekanavyo lakini wawalipe mishahara huko huko na posho za vikao. Sitaki sitaki sitaki hatma ya Watanzania million arobaini kuamuliwa na Wazanzibar million moja kwa lugha ya ujanja ujanja kuwa Wazenj wanamezwa! Hivi milioni arobaini ni muhali kumeza milioni moja? Mbona lugha inabadilishwa kwa uongo kabisa hapa, nani afurahi? Sijakiona ambacho Bara wanakipata kutoka Zanzibar. Badala yake Bara imegeuka kuwa mgawa-fadhila za bure Zenj kuwapa umeme bure na kutuibia dhahabu.