Tanzania tuwe na Tume huru ya Uchaguzi

Tanzania tuwe na Tume huru ya Uchaguzi

Sheria inayounda Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ni Tume huru, an independent institution ambayo haipaswi kuingiliwa na yeyote kama lilivyo Bunge, Mahakama, Ofisi ya CAG, Tume ya Haki za binaadam na Utawala Bora, ofisi ya DPP, Takukuru etc. Taasisi zote hizi watendaji wakuu wanateuliwa na rais.

Kama tumeikubali Mahakama kuwa iko huru, na NEC pia iko huru!.

Kitu nilichosema kuhusu NEC, kwa vile uchaguzi unahusisha vyama vingi, then NEC should be inclusive.

The electro process zina guarantee uchaguzi huru na wa haki. Ila our electoral law is a bad law na hili tumelizungumza sana humu.
P
Pascal hujanijibu swali langu umekuwa so evasive.

Tuache Bunge, Mahakama, CAG, CHRAG, DPP na TAKUKURU kwa sasa, ambapo kuwa HURU kwakwe iongelewe Siku nyingine.

Itoshe tu kusema kuwa:
Tume inaundwa na katiba ya Jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 chini ya Ibara ya 74(1).

UHURU wa tume kama upo, labda unapatikana chini ya ibada 74(7) kwa maneno yafuatayo " tume ya uchaguzi itakuwa ni imara huru inayojitegemea"
Swali ni je chini ya katiba kuna guarantees gani zinazoonesha kuwa tume inayopewa huo uhuru ??? Kama ilivyo dhana za uhuru wa mahakama (independence of the judiciary) na mgawanyo wa madaraka (separation of powers) ambayo kwa kiasi kikibwa inafanya mahakama iwe huru

Inclusiveness inatokana na jinsi ambavyo muundo wa tume ulivyo. Kama tatakubali kuwa tume si huru basi itabidi kuangalia tume huru HURU inatakiwa iweje???

Pascal niambie ni kwa vipi unadhani hii tume ni huru???
 
Imenishangaza mpaka sasa hasa wapinzani hawajadai tume huru ya uchaguzi. Hii haitakuwa nzuri kwa taifa tujiandae muhula wa pili kuwa mgumu kwa Magu. Kwanza kwasababu ya kutokuwa na tume huru jumuia za kimataifa zitatugomea kwenye mambo mengi. Pili pesa za watalii zitapungua kwa chaguzi za kenya na Tanzania kutisha wageni. Tatu CCM wataanza groups za kuwa Raisi ajaye. Vilevile kama kawaida Zanzibar kutaibiwa kura na kuleta majanga kule.
Hivyo kwa mnao ona mbali hasa CCM jueni tume huru itawasaidia kwa mengi.Bila hivyo mtawapa upinzani nguvu maana malalamiko yao kila mtu ataona wazi
Katiba ya nchi haiko kwa ajili ya wapinzani, katiba ni kwa ajili ya wanaichi wote bila kujali vyama, makabila na dini zao, bahati mbaya watanzania tunaihusisha katiba na vyama vya siasa tu na si vinginevyo hivyo jukumu tunawasukumia wanasiasa nasi tunakaa pembeni tukiwaangalia.
 
Back
Top Bottom