Tanzania tuwe na Tume huru ya Uchaguzi

Pascal hujanijibu swali langu umekuwa so evasive.

Tuache Bunge, Mahakama, CAG, CHRAG, DPP na TAKUKURU kwa sasa, ambapo kuwa HURU kwakwe iongelewe Siku nyingine.

Itoshe tu kusema kuwa:
Tume inaundwa na katiba ya Jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 chini ya Ibara ya 74(1).

UHURU wa tume kama upo, labda unapatikana chini ya ibada 74(7) kwa maneno yafuatayo " tume ya uchaguzi itakuwa ni imara huru inayojitegemea"
Swali ni je chini ya katiba kuna guarantees gani zinazoonesha kuwa tume inayopewa huo uhuru ??? Kama ilivyo dhana za uhuru wa mahakama (independence of the judiciary) na mgawanyo wa madaraka (separation of powers) ambayo kwa kiasi kikibwa inafanya mahakama iwe huru

Inclusiveness inatokana na jinsi ambavyo muundo wa tume ulivyo. Kama tatakubali kuwa tume si huru basi itabidi kuangalia tume huru HURU inatakiwa iweje???

Pascal niambie ni kwa vipi unadhani hii tume ni huru???
 
Katiba ya nchi haiko kwa ajili ya wapinzani, katiba ni kwa ajili ya wanaichi wote bila kujali vyama, makabila na dini zao, bahati mbaya watanzania tunaihusisha katiba na vyama vya siasa tu na si vinginevyo hivyo jukumu tunawasukumia wanasiasa nasi tunakaa pembeni tukiwaangalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…