Tanzania, Ubelgiji zakubaliana maendeleo sekta ya nishati

Tanzania, Ubelgiji zakubaliana maendeleo sekta ya nishati

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko na Waziri wa Nishati wa Ubelgiji, Tinne Van Straeten wamekubaliana kishirikiana katika sekta hiyo hususani matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katika kikao cha viongozi hao kilichofanyika Windhoek, Namibia, viongozi hao walikubaliana kutekeleza kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo ya Afrika.

Kikao hicho kilifanyika wakati wa Mkutano wa Nchi za Africa zilipokutana kujadili matumizi ya Hydrojen katika kuzalisha umeme.

Dk. Biteko amesema ili kupata maendeleo ya kweli, Tanzania inatoa kipaumbele katika matumizi ya nishati ambayo itawawezesha kupata maendeleo endelevu ikiwa ni pamoja kuondokana na magonjwa na vifo vinavyotokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi.

- Benki ya Dunia yaisadia Tanzania dola milioni 300 kuendelea kuimarisha sekta ya nishati nchini

Snapinsta.app_458286211_946675457503017_2131409359612873587_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom